Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Riyad Mahrez aweka shilingi yake Nigeria

MAHREZ Pict

Muktasari:

  • Mahrez alicheza kwa dakika 60 akiwa katika jezi ya Algeria walipokutana na Nigeria kwenye robo fainali za mashindano hayo katika Uwanja wa Stade Marrakech, Jumamosi iliyopita.

MARRAKECH, MOROCCO: NAHODHA wa Algeria, Riyad Mahrez ameitaja timu ya taifa ya Nigeria kuwa miongoni mwa vinara wa kutwaa Kombe la Mataifa ya Afrika 2025 (AFCON).

Mahrez alicheza kwa dakika 60 akiwa katika jezi ya Algeria walipokutana na Nigeria kwenye robo fainali za mashindano hayo katika Uwanja wa Stade Marrakech, Jumamosi iliyopita.

Kabla ya mechi hiyo, nyota huyo wa zamani wa Manchester City alikuwa tayari amefunga mabao matatu na alikuwa miongoni mwa wanaowania Kiatu cha Dhahabu. Kwa hakika, ilitarajiwa angekuwa tishio kubwa kwa safu ya ulinzi ya Super Eagles.

Hata hivyo, Mahrez alipata wakati mgumu katika mechi hiyo. Yeye pamoja na wenzake walishindwa kufurukuta mbele ya wachezaji wa Nigeria.

MAH 01

Kwa hakika, alifunikwa kabisa na hakupewa nafasi ya kuonyesha ubora wake. Hata baada ya kubadilishwa, mchezaji aliyeingia kuchukua nafasi yake, Anis Hadj Moussa, hakufanya vizuri zaidi, kwani kiungo na safu ya ushambuliaji ya Algeria ilizimwa kabisa.

Ilikuwa ni onyesho la nguvu kutoka kwa kikosi cha kocha Eric Chelle, ambao waliwazidi kwa kila idara Mbweha wa Jangwani. Mechi ilimalizika kwa ushindi wa 2-0 kwa Super Eagles, ingawa matokeo yangeweza kuwa mabaya zaidi kwa Algeria.

Baada ya filimbi ya mwisho, nahodha wa Algeria, Mahrez alionekana kukata tamaa sana. Baada ya kutangaza katika mkutano wa waandishi wa habari kabla ya mchezo dhidi ya Nigeria kuwa AFCON 2025 ungekuwa mashindano yake ya mwisho ya kimataifa, kuondolewa kwa namna hiyo kulimuacha na maumivu makubwa.

Licha ya kipigo hicho, Mahrez alitoa kauli ya kushangaza, akiipa Nigeria sapoti ya kutwaa taji hilo nchini Morocco. Kiungo mshambuliaji huyo wa Al-Ahli alitaja kipaji kikubwa kilichopo kwenye kikosi cha Nigeria kuwa sababu kuu ya utabiri wake.

MAH 02

“Najivunia kuwa niliweza kushinda AFCON moja kwa ajili ya nchi yangu. Huu ni mpira wa miguu, wakati mwingine unashinda, wakati mwingine unapoteza,” amesema Mahrez na kuongeza:

“Labda huu utakuwa wakati wa Nigeria kushinda. Wana kizazi kizuri cha wachezaji. Lakini wakati mwingine unaweza kuwa na kizazi kizuri bila kushinda chochote. Ni vigumu sana kushinda, lakini nadhani wana nafasi nzuri.”