Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Richarlison atupwa nje Spurs

RICHALSON Pict

Muktasari:

  • Richarlison, mwenye umri wa miaka 29 mmoja kati ya wachezaji wenye mbwembwe duniani, amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake na Tottenham, huku klabu hiyo ikiwa na chaguo la kuongeza mwaka mwingine. Kwa sasa, Trabzonspor imeonyesha nia kubwa ya kumnasa nyota huyo.

LONDON, ENGLAND: MSHAMBULIAJI wa Brazil, Richarlison, ameondolewa kwenye kikosi cha Tottenham Hotspur kitakachoshiriki Ligi Kuu England msimu huu, huku mpango wa kuhamia klabu ya Trabzonspor ya Uturuki ukiwa bado haujakamilika.

Richarlison, mwenye umri wa miaka 29 mmoja kati ya wachezaji wenye mbwembwe duniani, amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake na Tottenham, huku klabu hiyo ikiwa na chaguo la kuongeza mwaka mwingine. Kwa sasa, Trabzonspor imeonyesha nia kubwa ya kumnasa nyota huyo.

Klabu hiyo ya Uturuki iliwashangaza mashabiki wa soka mapema msimu huu baada ya kumsajili kwa uhamisho huru Mohamed Salah, na sasa inataka kuwaunganisha Salah na Richarlison pamoja na kiungo Fabinho, ambaye pia ni raia wa Brazil na nyota wa zamani wa Liverpool.

Dirisha la usajili nchini Uturuki lilitarajiwa kufungwa Ijumaa, huku Richarlison akielezwa kuwa yuko tayari kuhamia Trabzonspor ili kuungana na Salah na Fabinho.

RICHA 01

Hata hivyo, Tottenham bado haijapokea ofa inayokidhi thamani waliyoweka kwa mshambuliaji huyo. Spurs wanamtaka takribani Pauni 35 milioni (Sh bilioni 126) kwa Richarlison, ambaye awali walimsajili kutoka Everton mwaka 2022 kwa kiasi cha pauni 60 milioni.

Richarlison alipewa taarifa kabla ya siku ya mwisho ya usajili nchini England kwamba hayumo kwenye mipango ya kocha mpya Roberto De Zerbi kwa msimu huu na angeweza kuondoka endapo klabu nyingine ingefika na ofa inayoridhisha.

Baada ya kumtema kwenye kikosi kilichopoteza dhidi ya Newcastle United Jumamosi iliyopita, De Zerbi amesema Richarlison, ambaye amewahi pia kuchezea Watford na Everton, alikuwa ameomba kuondoka Tottenham “mara nyingi sana.”


RICHA 02

SPURS YAMJUMUISHA SIMONS

Licha ya kumuacha Richarlison, Tottenham ilipowasilisha kikosi chake cha Ligi Kuu England Alhamisi, iliwajumuisha baadhi ya wachezaji ambao kwa sasa hawapo katika hali nzuri kiafya.

Xavi Simons aliingizwa kwenye kikosi hicho licha ya kuwa na jeraha kubwa la goti linalotarajiwa kumuweka nje hadi mwakani.

Dejan Kulusevski naye yumo kwenye kikosi, ingawa hajacheza kwa takribani miezi 19 kutokana na kufanyiwa upasuaji mkubwa wa goti. Hata hivyo, tayari ameanza kurejea mazoezini.

Wilson Odobert, ambaye pia anasumbuliwa na jeraha kubwa la goti, amejumuishwa huku sasa akitambuliwa kama mchezaji aliyelewa ndani ya mfumo wa soka la England (homegrown).


RICHA 03

RICHARLISON: “MIMI NI MHALIFU?”

Kabla ya uwezekano wa kuhamia Trabzonspor kujitokeza, Richarlison alitoa ujumbe za mafumbo kupitia mitandao yake ya kijamii baada ya kuibuka kwa taarifa kwamba angeweza kurejea Everton.

Awali kulikuwa na mpango wa Richarlison kuhusishwa kwenye dili la kubadilishana wachezaji na Everton kwa ajili ya Iliman Ndiaye. Hata hivyo, dili hilo halikufanikiwa na Ndiaye mwishowe alijiunga na Manchester City siku ya mwisho ya usajili.

Richarlison aliweka picha kwenye Instagram yenye ujumbe uliosomeka:

“Mimi ni mhalifu katika hadithi nyingi zinazosimuliwa vibaya.”

Baadaye akaongeza ujumbe akisema kuwa kama Tottenham na Everton wangekubaliana, angekuwa tayari kurejea katika klabu hiyo aliyodai kuwa aliwahi kuwa na furaha kubwa.

Hata hivyo, alisisitiza kuwa bado ana mkataba na Tottenham na yuko tayari kuitumikia klabu hiyo.

Staa huyo ambaye amekaa kwenye kikosi cha Spurs kwa misimu mitano amefanikiwa kucheza michezo 134 na kufunga mabao 32 akiwa na kiwango cha kupanda na kushuka kwa kipindi chake chote.