Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Richarlison awa mkali huko Spurs

RICHALSON Pict

Muktasari:

  • ESPN Brasil iliripoti kuwa mshambuliaji huyo wa Samba ana nia ya kumaliza safari yake Kaskazini mwa London baada ya Kombe la Dunia 2026 litakalofanyika majira ya kiangazi huko Marekani, Canada na Mexico.

LONDON, ENGLAND: RICHARLISON amepuuza kabisa madai kwamba anataka kuondoka Tottenham Hotspur mwishoni mwa msimu huu, kupitia chapisho lenye lugha kali kwenye mitandao ya kijamii.

ESPN Brasil iliripoti kuwa mshambuliaji huyo wa Samba ana nia ya kumaliza safari yake Kaskazini mwa London baada ya Kombe la Dunia 2026 litakalofanyika majira ya kiangazi huko Marekani, Canada na Mexico.

Tovuti hiyo pia ilidai kuwa klabu ya Brazil,  Flamengo ni miongoni mwa timu zinazomtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, pamoja na klabu za Uturuki na Saudi Arabia.

Hata hivyo, alipotoa maoni kwenye Instagram kujibu taarifa hiyo, Richarlison mwenyewe aliandika: “Nani amesema hivyo? Ondokeni hapa!”

Richarlison amekuwa akihusishwa na kuondoka Spurs katika misimu kadhaa iliyopita. Msimu uliopita, alifichua kuwa alipokea ofa nono kutoka Saudi Arabia lakini akaamua kubaki Tottenham, akisema wazi: “Pesa ni nyingi, lakini ndoto zangu ni kubwa zaidi.”

Kulikuwa na kipindi ambapo Spurs ilikuwa tayari kumuuza Richarlison, ambaye ilimsajili kwa Pauni 60 milioni kutoka Everton mwaka 2022. Hii ilitokana na rekodi yake ya majeruhi na kiwango chake uwanjani ambacho hakikuendana na ada kubwa iliyolipwa kumnunua.

Lakini, msimu huu amekuwa mmoja wa wachezaji wa kuaminika zaidi chini ya kocha Thomas Frank, kwa upande wa dakika anazocheza na hatari yake langoni.

Kwa kuwa Dominic Solanke amekuwa nje karibu msimu mzima, isipokuwa kuingia kama mchezaji wa akiba mara tatu mwezi Agosti, jukumu la kuongoza safu ya ushambuliaji limekuwa mikononi mwa Richarlison. Tayari ameshacheza mechi 31 kwa klabu msimu huu, akifunga mabao manane.

Mchezaji huyo wa zamani wa Watford anaonekana kuwa na nafasi nzuri ya kujumuishwa kwenye kikosi cha Brazil cha kocha Carlo Ancelotti kwa ajili ya Kombe la Dunia 2026 na ana rekodi nzuri kwa taifa lake akiwa amefunga mabao 20 katika mechi 54 za kimataifa.