Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rekodi 10 ngumu kuvunjika Kombe la Dunia 2026

Muktasari:

  • Baadhi ya rekodi za Kombe la Dunia zinaweza kuvunjwa mwaka 2026 kutokana na kuongezeka kwa idadi ya timu na mechi. Hata hivyo, rekodi za wachezaji kama Pele, Just Fontaine na Roger Milla zinaonekana kuwa miongoni mwa zile ambazo huenda zikabaki milele katika vitabu vya historia ya soka.

MIAMI, MAREKANI: WAKATI nyota kama Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na Kylian Mbappe wakitarajiwa kuweka rekodi mpya katika Kombe la Dunia 2026, zipo baadhi ya rekodi ambazo zinaonekana kuwa ngumu  kuvunjwa kabisa.

Baadhi ya rekodi za Kombe la Dunia zinaweza kuvunjwa mwaka 2026 kutokana na kuongezeka kwa idadi ya timu na mechi. Hata hivyo, rekodi za wachezaji kama Pele, Just Fontaine na Roger Milla zinaonekana kuwa miongoni mwa zile ambazo huenda zikabaki milele katika vitabu vya historia ya soka.


Rekodi hizo 10 ambazo zinaonekana zitadumu milele katika historia ya mashindano hayo ni pamoja na:


1. MCHEZAJI MMOJA KUTWAA MATAJI MENGI

Gwiji wa soka wa Brazil, Pele ndiye mchezaji pekee aliyewahi kushinda ubingwa wa Kombe la Dunia mara tatu (1958, 1962 na 1970). Hadi leo hakuna mchezaji aliyefikia idadi hiyo, sembuse kuivuka.


2. MABAO MENGI ZAIDI KATIKA KOMBE MOJA LA DUNIA

Katika Kombe la Dunia la mwaka 1958, mshambuliaji wa Ufaransa, Just Fontaine aliweka rekodi ya kufunga mabao 13.

Aliweka rekodi hiyo kwa kufunga hat-trick moja, mabao mawili mara mbili na mabao manne dhidi ya Ujerumani Magharibi katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu. Rekodi hiyo imesimama kwa karibu miaka 70. Rekodi hiyo inaweza kutishiwa kuvunja kutokana na kuongezaka kwa idadi ya mechi.


3. KUFUNGA MABAO MENGI NA TIMU YAKO KUFUNGWA

Mpoland Ernst Wilimowski alifunga mabao manne dhidi ya Brazil katika Kombe la Dunia la 1938.

Cha kushangaza, Poland ilipoteza mchezo huo kwa mabao 6-5 baada ya muda wa nyongeza.

Hadi leo hakuna mchezaji aliyewahi kufunga mabao manne katika mechi ya Kombe la Dunia na bado akatoka akiwa ameshindwa.


4. MFUNGAJI MKONGWE ZAIDI WA KOMBE LA DUNIA

Roger Milla aliweka rekodi hii mwaka 1994 alipofunga akiwa na miaka 42 na siku 39.

Bao lake dhidi ya Russia lilimfanya kuwa mfungaji mwenye umri mkubwa zaidi katika historia ya mashindano hayo.

Hadi sasa hakuna aliyekaribia kuivunja rekodi hiyo.


5. MCHEZAJI MKONGWE ZAIDI KUCHEZA KOMBE LA DUNIA

Kipa wa Misri, Essam El-Hadary aliingia uwanjani katika Kombe la Dunia 2018 akiwa na miaka 45. Katika mechi hiyo hata aliokoa penalti. Rekodi hiyo bado inaonekana ipo salama kwa sasa. Hakuna mchezaji wenye miaka zaidi ya 45 atashiriki Kombe la Dunia 2026.


6. Kuchezea mataifa matatu tofauti

Dejan Stankovic alicheza Kombe la Dunia akiwa na na timu ya taifa ya Yugoslavia (1998), baadaye alibadilisha uraia na kuichezea Serbia na Montenegro (2006) na miaka minne baadaye alichezea Serbia (2010).

Mabadiliko ya kisiasa yaliyotokea Balkans ndiyo yaliyowezesha rekodi hiyo. Sheria za sasa za FIFA zinaifanya rekodi hiyo haiwezekani kurudiwa.


7. Kucheza fainali kwa mataifa mawili tofauti

Mchezaji Luis Monti alipoteza ubingwa katika fainali ya mwaka 1930 akiwa na Argentina kabla ya kutwaa taji hilo katika fainali ya mwaka 1934 akiwa na Italia.

Ni rekodi ambayo mazingira ya soka la kisasa hayawezi kuruhusu irudiwe.


8. Kushiriki Kombe la Dunia mara nyingi akiwa Kocha

Carlos Alberto Parreira ameshiriki Kombe la Dunia mara sita akiwa kocha.

Mbrazili huyo alianza kibarua chake kwa kuiongoza Kuwait (1982), baadaye akawa kocha wa United Arab Emirates (1990). Akaiongoza Brazil mara mbili (1994 na 2006), kabla ya kuchukua jukumu hilo kwa Saudi Arabia (1998) na kumaliza na Afrika Kusini (2010).

Hakuna kocha mwingine aliyefikia idadi hiyo hadi sasa hata makocha wote waliopo Marekani, Canada na Mexico hakuna anayesogelea rekodi hiyo.


9. Kadi za njano nyingi kupewa mchezaji moja

Mwamuzi Graham Poll aliandika historia mwaka 2006 alipompa Josip Simunic kadi ya njano mara tatu kabla ya kumtoa nje.

Tukio hilo lilitokana na makosa ya mwamuzi na linaonekana haliwezi kutokea tena katika enzi hizi za VAR na teknolojia za kisasa.


10. Idadi Ndogo zaidi ya mashabiki

Katika Kombe la Dunia la kwanza mwaka 1930 nchini Uruguay, inakadiriwa kuwa watu 300 tu walihudhuria mechi kati ya Romania na Peru.

Kwa ukubwa wa Kombe la Dunia la kisasa, rekodi hiyo inaonekana haiwezi kuguswa tena.