Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa kutafuta maisha Ulaya, mwanasoka afariki majini

Muktasari:

  • Sasa kama ilivyo kwa watu wengine, safari ya kutafuta maisha bora kwa Faten Ben Amar El Aziz imegeuka kuwa mauti baada ya mwanasoka huyo chipukizi mwenye miaka 20 kufariki dunia wakati akijaribu kuvuka baharini kuelekea Ceuta, eneo linalosimamiwa na Hispania.

MAISHA yanatafutwa kwa tabu sana. Wapo hadi wanaoweka rehani roho zao, kukimbia familia zao ilimradi kupata maisha bora.

Sasa kama ilivyo kwa watu wengine, safari ya kutafuta maisha bora kwa Faten Ben Amar El Aziz imegeuka kuwa mauti baada ya mwanasoka huyo chipukizi mwenye miaka 20 kufariki dunia wakati akijaribu kuvuka baharini kuelekea Ceuta, eneo linalosimamiwa na Hispania.

Faten, aliyekuwa akiichezea Maghreb Athlétique Tétouan ya Morocco, alikuwa na ndoto kama vijana wengine wanaotamani kubadili maisha yao kupitia fursa za soka. Lakini ndoto hiyo imekatizwa ghafla baada ya safari yake kuelekea upande wa Hispania kuishia njiani, huku taarifa za tukio hilo zikisambaa na kuacha huzuni katika familia, klabu na jamii ya soka ya Tétouan.

Baadhi ya taarifa zinaeleza chipukizi huyo alikuwa anakwenda Hispania kutafuta angalau timu au akademi ya kujiunga nayo ili kutimiza ndoto ya kucheza Ulaya kama ilivyo kwa wachezaji wengine kutoka Morocco akiwemo Achraf Hakimi anayekipiga PSG na Brahim Diaz wa Real Madrid.

Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa nchini Morocco, Faten alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakijaribu kufika katika nchi ya Hispania, kupitia baharini na kuogelea kuelekea upande wa Ceuta.

Ceuta ni eneo la Hispania lililopo kwenye pwani ya Afrika Kaskazini na linapakana na Morocco. Eneo la Tarajal ni miongoni mwa maeneo yanayotajwa kuwa wananchi wengi huvuka mpaka huo.

Lakini hivi karibuni, idadi kubwa ya watu ilijaribu kuingia Ceuta kutoka Morocco, huku baadhi wakitumia njia ya baharini ambayo inadaiwa sio salama. Kati ya hao, Faten alikuwemo na ndipo akakumbwa na tukio hilo.