Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Refa Msomalia aliyezuiwa Marekani kuchezesha UEFA Super Cup

Muktasari:

  • Artan alichezesha mechi ya pili ya Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya AS FAR ya Morocco na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Umoja wa Vyama vya Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA) umempanga Refa Omar Artan kuchezesha mechi ya taji la UEFA Super 2026 baina ya PSG na Aston Villa, Agosti 12, 2026.

Taarifa hiyo imetolewa leo Alhamisi, Juni 11, 2026 ikiwa ni siku nne tangu Artan alipozuiliwa kuingia Marekani kwa ajili ya kuchezesha Fainali za Kombe la Dunia zinazoanza leo.

Serikali ya Marekani ilidai kwamba ilimzuia Artan kwa sababu za kiusalama huku baadaye Shrikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) likitangaza kwamba Refa huyo hatochezesha tena mashindano hayo.

Uamuzi huo umeonekana kuzua mjadala mkubwa duniani huku FIFA na Marekani zikishambuliwa na mamilioni ya watu huku upande wa pili refa huyo mwenye umri wa miaka 34 akipokelewa kishujaa nchini mwake na kupokea jumbe nyingi za kumtia moyo kutoka nje na ndani ya Afrika.

Taarifa ya UEFA imesema kuwa uamuzi wa kumteua Artan umetokana na mahusiano mazuri baina yake ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na pia ubora wa refa huyo.

“Licha ya umri wake mdogo, Artan amejitambulisha kama miongoni mwa marefa bora zaidi duniani na amekuwa mwamuzi wa kimataifa wa FIFA tangu, 2018.

“Kwa kutambua ufanisi wake, alipokea Tuzo ya Refa Bora wa CAF wa mwaka 2025,” imesema taarifa ya UEFA.

Rais wa UEFA, Aleksander Ceferin amesema kuwa, “Artan ni kijana bora zaidi na tayari ana uzoefu ambao ameuthibitisha katika mechi za hatua kubwa za soka la Afrika.”

Rais wa CAF, Patrice Motsepe amesema, “Omar Artan ameifanya Somalia na watu wote wa bara la Afrika kuwa na fahari. Hii ni heshima kubwa kwa Afrika.”