Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkwe Trump kuinunua Los Angeles Lakers

TRUMP Pict

Muktasari:

  • Lakers itanunuliwa na bilione Josh Kushner, ambaye ni kaka wa Jared Kushner, mkwe wa Rais wa Marekani Donald Trump, pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Disney, Bob Iger, wamekubaliana kununua hisa zinazowapa udhibiti wa moja ya timu maarufu zaidi za michezo duniani.

LOS ANGELES, MAREKANI: KLABU ya Los Angeles Lakers inatarajiwa kuuzwa kwa thamani ya dola bilioni 12.5, ikivunja rekodi ya dunia.

Uamuzi wa kuuzwa klabu hiyo unakuja ikiwa ni chini ya mwaka mmoja tangu Mark Walter anunue hisa nyingi katika timu hiyo ya NBA.

Lakers itanunuliwa na bilionea Josh Kushner, ambaye ni kaka wa Jared Kushner, mkwe wa Rais wa Marekani Donald Trump, pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Disney, Bob Iger, wamekubaliana kununua hisa zinazowapa udhibiti wa moja ya timu maarufu zaidi za michezo duniani.

Walter alinunua hisa zake kwa familia ya Buss kwa thamani iliyokadiriwa kufikia dola bilioni 10, kiasi ambacho wakati huo kilikuwa rekodi ya thamani kubwa zaidi kwa ununuzi wa timu ya michezo. Dili hilo liliidhinishwa kwa kauli moja na Bodi ya Magavana ya NBA mwezi Oktoba 2025.

Kushner na Iger wamesema katika taarifa yao: “Kama mashabiki wa NBA wa muda mrefu, tumeheshimiwa sana kupata fursa ya kuwa wasimamizi wa Los Angeles Lakers, moja ya klabu maarufu zaidi za michezo duniani.

TRUM 01

“Tunamheshimu sana Jerry na Jeanie Buss kwa uongozi na maono yao.

“Dhamira yetu ya muda mrefu ni kujenga juu ya msingi huo, kushindana katika kiwango cha juu zaidi na kuitumikia timu hii ya kipekee, mashabiki wake pamoja na jiji la Los Angeles.”

Jerry Buss alinunua Lakers mwaka 1979 kwa dola milioni 67.5. Dili hilo lilihusisha pia timu ya mpira wa magongo ya Los Angeles Kings pamoja na uwanja wa Los Angeles, unaojulikana kwa sasa kama Kia Forum.

Baada ya kifo cha Jerry Buss mwaka 2013, umiliki wa Lakers ulihamishiwa kwa watoto wake sita kupitia taasisi ya Trust, kabla ya makubaliano ya kuuzwa kwa Walter kukamilika.

Walter pia anamiliki hisa katika Los Angeles Dodgers pamoja na Todd Boehly.

“Kuimiliki Los Angeles Lakers imekuwa moja ya heshima kubwa zaidi katika maisha yangu,” amesema Walter.

TRUM 02

“Imekuwa uwekezaji wa kipekee, lakini nitakachokumbuka zaidi ni jamii, mashabiki na jiji ambalo linaichukulia timu hii kama familia.

“Ninamshukuru Jeanie Buss, familia ya Buss, wachezaji na wafanyakazi kwa kunikaribisha katika sura hii ya historia. Lakers ni mali ya Los Angeles na nina imani kubwa kwamba mambo bora bado yako mbele.”

Lakers ina mataji 17 ya NBA, ikiwa ni moja nyuma ya rekodi ya mataji 18 inayoshikiliwa na Boston Celtics.

Ujio wa Kushner katika dili hilo umefanyika wakati jina lake likihusishwa na sakata lililomzunguka Rais wa FIFA, Gianni Infantino, kuhusu mpango uliokuwa umeandaliwa wa kuuza sehemu ya umiliki wa mashindano ya FIFA kwa wawekezaji binafsi.

Kampuni ya Thrive Eternal, inayojihusisha na uwekezaji wa mitaji na iliyoanzishwa na Kushner nchini Marekani, ilitarajiwa kuongoza kundi la wawekezaji katika mpango wa Fifa Forward Enterprise (FFE), kabla ya mpango huo kusitishwa.