Real Madrid yaweka Pauni 120 Bilioni kwa Diomande
Muktasari:
- Nyota huyo wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 19 anatarajiwa kuwa mmoja wa usajili mkubwa zaidi wa majira haya ya kiangazi, huku ada hiyo ikimfanya kuwa miongoni mwa wachezaji ghali zaidi kuwahi kusajiliwa na miamba hiyo ya Hispania.
MADRID, HISPANIA: REAL Madrid imefikia makubaliano ya kumsajili winga chipukizi wa RB Leipzig, Yan Diomande, katika dili linaloweza kufikia euro 140milioni (takribani Pauni milioni 120), baada ya mazungumzo ya muda mrefu kati ya klabu hizo.
Nyota huyo wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 19 anatarajiwa kuwa mmoja wa usajili mkubwa zaidi wa majira haya ya kiangazi, huku ada hiyo ikimfanya kuwa miongoni mwa wachezaji ghali zaidi kuwahi kusajiliwa na miamba hiyo ya Hispania.
Diomande amekuwa akifuatiliwa kwa karibu na Real Madrid kutokana na kiwango chake bora akiwa RB Leipzig, ambapo ameonyesha uwezo mkubwa wa kucheza pembeni kwa kasi, ubunifu na uwezo wa kufunga mabao.
Endapo dili hilo litakamilika rasmi, Real Madrid itakuwa imeongeza silaha nyingine muhimu kwenye safu yake ya ushambuliaji, ikiendelea na mkakati wa kusajili vipaji bora vya dunia kwa ajili ya kujenga kikosi cha muda mrefu.
Wakati huo huo, Liverpool inaendelea kuchunguza uwezekano wa kumsajili mshambuliaji kijana Ibrahim Mbaye, huku Aston Villa ikiripotiwa kufikia makubaliano ya kumsajili beki wa kushoto Matteo Ruggeri, katika harakati za kuimarisha vikosi vyao kabla ya kuanza kwa msimu mpya.