Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Real Madrid, RB Leipzig zarudi mezani

DIAMONDE Pict

Muktasari:

  • Majadiliano hayo yanaendelea baada ya kusimama kwa muda katika siku chache zilizopita, lakini taarifa za ndani zinaeleza kuwa mawasiliano kati ya klabu hizo mbili yameanza tena kwa lengo la kukamilisha moja ya usajili mkubwa wa dirisha hili la usajili.

Real Madrid na RB Leipzig zimerejea mezani kuendelea na mazungumzo kuhusu usajili wa kiungo mshambuliaji wa Ivory Coast, Yan Diomande, huku pande zote zikionyesha matumaini ya kufikia makubaliano kabla ya mwisho wa wiki.

Majadiliano hayo yanaendelea baada ya kusimama kwa muda katika siku chache zilizopita, lakini taarifa za ndani zinaeleza kuwa mawasiliano kati ya klabu hizo mbili yameanza tena kwa lengo la kukamilisha moja ya usajili mkubwa wa dirisha hili la usajili.

Akizungumza Jumatatu, Agosti 3, 2026, mkurugenzi wa michezo wa RB Leipzig, Marcel Schäfer, alikiri kuwa mazungumzo bado yanaendelea, huku akisisitiza kuwa hakuna makubaliano ya mwisho yaliyofikiwa.

"Bado hatujafikia hatua hiyo," alisema Schäfer, akimaanisha kuwa dili hilo bado halijakamilika kwa asilimia 100.

Hata hivyo, dalili zinaonyesha uhamisho huo uko katika hatua za mwisho baada ya Diomande kutosafiri na kikosi cha RB Leipzig kilichoelekea Saalfelden, Austria, kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya msimu mpya.

Kutokuwapo kwa nyota huyo kwenye safari ya timu kumeongeza uvumi kwamba anakaribia kuondoka Leipzig na kutimiza ndoto ya kujiunga na mabingwa hao wa Hispania.

Iwapo makubaliano yatakamilika kama inavyotarajiwa, Diomande atakuwa mmoja wa usajili mkubwa zaidi wa Real Madrid msimu huu na kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ya kikosi hicho kuelekea msimu wa 2026/27.