Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mac Allister afunguka mrithi wa Messi Argentina

JEZI Pict

Muktasari:

  • Hivyo, wakati safu ya uongozi wa timu ikiwa tayari imepata mrithi, bado haijafahamika nani atabeba jukumu la kuvaa jezi namba 10 baada ya Messi, huku pendekezo la Mac Allister likitaka kuwe na kipindi cha mpito kabla ya kumpata mrithi wa kudumu.

BUENOS AIRES,ARGENTINA: ALIYEKUWA mchezaji wa Argentina, Carlos Mac Allister, amependekeza jezi namba 10 ya timu hiyo ya taifa isipewe mrithi wa moja kwa moja wa Lionel Messi mara baada ya nyota huyo kumaliza kuitumikia timu hiyo, bali izunguke kwa wachezaji kadhaa kwa kipindi cha miezi nane hadi tisa kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho.

Mac Allister amesema haoni sababu ya kumteua mchezaji mmoja mara moja kuvaa jezi hiyo ambayo imekuwa alama kubwa ya soka la Argentina kwa miaka mingi chini ya Messi.

Akizungumza katika kipindi cha ESPN, Mac Allister amesema: “Nisingempa mtu yeyote jezi namba 10.”

JEZ 01

Hata hivyo, pendekezo lake halimaanishi kuiondoa kabisa jezi hiyo au kuiacha bila kutumiwa. Badala yake, anataka wachezaji kadhaa wapewe nafasi ya kuivaa kwa zamu katika kipindi cha mpito, ili benchi la ufundi lipate muda wa kutathmini nani anayestahili kupewa jukumu hilo la kihistoria.

Miongoni mwa wachezaji aliowataja kuwa wanaoweza kupewa nafasi hiyo ni Enzo Fernandez, Julian Alvarez, Lautaro Martinez, Alexis Mac Allister na Nico Paz.

Kwa mujibu wa pendekezo hilo, kila mmoja angeweza kuvaa jezi hiyo kwa kipindi fulani kabla ya uamuzi wa mwisho kufanywa, baada ya kutathmini namna mabadiliko hayo yatakavyokwenda.

JEZ 02

Mac Allister amependekeza miezi minane au tisa ipite kabla ya kumteua mchezaji atakayepewa rasmi jezi hiyo iliyogeuka kuwa moja ya alama kubwa za timu ya taifa ya Argentina.

Amehusisha mtazamo wake na kipindi cha mpito kilichofuata baada ya Diego Maradona kuondoka katika timu ya taifa, mabadiliko aliyoyashuhudia akiwa sehemu ya kikosi cha Argentina.

Wakati mjadala wa mrithi wa jezi namba 10 ukiendelea kusubiriwa, suala la unahodha tayari linaonekana kuwa na mwelekeo tofauti baada ya kocha Lionel Scaloni kumtaja beki Cristian ‘Cuti’ Romero kuwa mrithi wa Messi katika jukumu hilo.

JEZ 03

“Cuti ndiye atakuwa nahodha,” amesema Scaloni, akieleza kuwa Romero alikuwa tayari chaguo la tatu katika orodha ya manahodha, nyuma ya Messi na Nicolas Otamendi.

Hivyo, wakati safu ya uongozi wa timu ikiwa tayari imepata mrithi, bado haijafahamika nani atabeba jukumu la kuvaa jezi namba 10 baada ya Messi, huku pendekezo la Mac Allister likitaka kuwe na kipindi cha mpito kabla ya kumpata mrithi wa kudumu.