Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Real Madrid yapiga kimya ishu ya Trent kuondoka

Muktasari:

  • Taarifa kutoka vyanzo vya ndani vya klabu hiyo zinaeleza kuwa bado inamchukulia Trent kama sehemu ya mipango ya baadaye, hasa kutokana na uwezo wake wa kipekee wa kupandisha mashambulizi, kupiga pasi ndefu pamoja na faulo.

BEKI wa kulia wa kimataifa wa England, Trent Alexander-Arnold, 27, hajaambiwa aondoke Real Madrid, licha ya taarifa kutoka Hispania kudai kuwa kocha mpya Alvaro Arbeloa amemtaka atafute timu nyingine dirisha hili la usajili.

Taarifa kutoka vyanzo vya ndani vya klabu hiyo zinaeleza kuwa bado inamchukulia Trent kama sehemu ya mipango ya baadaye, hasa kutokana na uwezo wake wa kipekee wa kupandisha mashambulizi, kupiga pasi ndefu pamoja na faulo.

Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2032. Tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 11. Taarifa za karibuni zilidai staa huyo anaweza kuondoka Real Madrid na kurudi England ambako timu nyingi zinahitaji huduma yake.

Miongoni mwa timu zinazomtaka ni Bayern Munich na Newcastle United, lakini inaaminika itahitajika kiasi kikubwa cha pesa ili kumpata. Trent anadaiwa kutofurahia maisha Madrid na anahitaji kuondoka ili kurudisha kiwango chake sehemu nyingine.


Julian Alvarez

ARSENAL imeanza kufuatilia kwa kina uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid na timu ya taifa ya Argentina, Julian Alvarez, 25, dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Arsenal inamuona staa huyo kama sehemu ya kuboresha safu ya ushambuliaji ambayo inaamini inaitajika kuongezewa nguvu zaidi. Hata hivyo, dili halitakuwa rahisi, kwani ni sehemu ya wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha  Atletico. Mkataba wake unamalizika 2030.


Yan Diomande

BAYERN MUNICH inakabiliwa na ushindani kutoka Liverpool katika mbio za kumsajili winga kinda wa RB Leipzig na timu ya taifa ya Ivory Coast, Yan Diomande, 19, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Diomande amezivutia timu nyingi Ulaya tangu dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana, lakini changamoto imekuwa ni kiasi kikubwa cha pesa ambacho mabosi wa Leipzig wanazitaka. Lepzig inataka mzigo wa pesa.


Lucas Paqueta

WEST HAM United imekataa dau la Pauni 32.9 milioni pamoja na Pauni 3 milioni  kama nyongeza lililowasilishwa na Flamengo kwa ajili ya kumnunua kiungo wa Brazil, Lucas Paqueta, katika dirisha hili. West Ham inaamini thamani ya Paqueta, 28, iko juu zaidi ya dau hilo, hasa kutokana na umuhimu wake katika kikosi. Flamengo inaamini Paqueta ataisaidia timu katika michuano ya kimataifa.


Joe Gomez

AC MILAN imeonyesha nia ya kumsajili beki wa Liverpool, Joe Gomez, 28, ili kuimarisha safu ya ulinzi kuelekea msimu ujao. Gomez, ambaye ana uwezo wa kucheza kama beki wa kati au pembeni ameonyesha nia ya kuondoka Liverpool kwa sababu hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza. Liverpool haijatoa msimamo ikiwa inamuuza, lakini mchezaji mwenyewe ameonyesha kuwa tayari kuondoka.


Adam Wharton

MANCHESTER United inawatazama kwa karibu Adam Wharton, 21, wa Crystal Palace pamoja na Carlos Baleba, 22, wa Brighton kama machaguo inayoyapa kipaumbele. Vyanzo vya ndani vinadai Man United inataka kuwasajili mastaa hao kutokana na umri wao mdogo ikiamini watawatumia kwa muda mrefu zaidi. Hata hivyo imepunguza matumaini ya kumsajili Elliot Anderson, 23, wa Nottingham ambaye ilikuwa inapambana kumnasa.


Kostas Tsimikas

LIVERPOOL inapanga kumrudisha beki wa kushoto raia wa Ugiriki, Kostas Tsimikas, 29, anayecheza kwa mkopo AS Roma. Majogoo wanafanya hivyo kutokana na mahitaji katika kikosi ambacho kinakumbana na uhaba wa wachezaji kutokana na majeraha. Roma bado haijathibitisha kama ina nia ya kumbakisha kwa muda mrefu, jambo linalofanya kurejea Liverpool kuwa chaguo muhimu.


Douglas Luiz

CHELSEA wamefanya mawasiliano ya awali na Juventus kujadili uwezekano wa kumsajili kwa mkopo kiungo wa timu hiyo Mbrazili Douglas Luiz, 27, ambaye kwa sasa yupo kwa mkopo Nottingham Forest akitokea Juventus. Luiz ameshaonyesha nia ya kuondoka Turin ikiwa timu hizo mbili zitafikia makubaliano. Chelsea inamwangalia staa huyo kwa jicho la tatu ikivutiwa na staili yake ya uchezaji.