Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Real Madrid yapanga kumuuza Vinicius Jr

TETESI Pict

Muktasari:

  • Inaelezwa Vinicius mwenye umri wa miaka 25, anahitaji mshahara mnono zaidi ili kusaini mkataba mpya na Madrid haitaki kumpa kiasi hicho cha pesa.

REAL Madrid imempanga kumuuza  mshambuliaji wao wa kimataifa wa  Brazil, Vinicius Jr, katika dirisha hili ikiwa ataendelea kugoma kuongeza mkataba mpya katika dirisha hili.

Inaelezwa Vinicius mwenye umri wa miaka 25, anahitaji mshahara mnono zaidi ili kusaini mkataba mpya na Madrid haitaki kumpa kiasi hicho cha pesa.

Mkataba wa staa huyu unatarajiwa kumalizika mwaka 2027. Msimu uliopita alicheza mechi 30 za La Liga na kufunga mabao 11.

Tetesi za kuondoka kwa fundi huyu zimekuwa zikisambaa tangu mwaka jana hususani baada ya kukosa tuzo ya Ballon D’or na waarabu wa Saudi Arabia waliweka mzigo wa kutosha kwa ajili ya kumpata lakini ilishindikana.

Kwa sasa fundi huyu anakunja mshahara wa Euro 15 milioni baada ya makato mbalimbali na sasa anataka kupewa Euro 20 milioni baada ya makato.

Kiasi hicho cha pesa kinaonekana kuwa ni kikubwa kwa Madrid ambayo ipo tayari kumwachia ikiwa ataendelea kushikilia msimamo wake wa kuhitaji pesa zaidi.


Ademola Lookman

INTER Milan inajiandaa kuwasilisha ofa kwenda Atalanta kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa klabu hiyo na timu ya taifa ya Nigeria, Ademola Lookman, 27, katika dirisha hili. Lookman ni miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Atalanta na amekuwa akihusishwa na timu mbalimbali barani Ulaya tangu msimu uliopita. Mkataba wa Ademola unatarajiwa kumalizika mwaka 2027. Katika msimu uliopita alicheza mechi 40 za michuano yote na kufunga mabao 20.


Nick Woltemade

BAYERN Munich imewasilisha ofa ya Pauni 43 milioni pamoja na nyongeza ya Pauni 4.4 milioni kwenda Stuttgart kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa timu hiyo na Ujerumani, Nick Woltemade, 23, katika dirisha hili. Inaelezwa Bayern pia iliipa Stuttgart ofa ya kuwapa asilimia 10 ya mauzo ya staa huyu ikiwa itamuuza hapo baadae lakini bado timu hiyo ilikataa ofa hiyo. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.



Omari Hutchinson

BRENTFORD inafanya majadiliano ya ndani kwa ndani kuona ikiwa kuna ulazima wa kuwasilisha ofa kwenda Ipswich Town kwa ajili ya kumsajili winga wa timu hiyo na timu ya taifa ya vijana ya England chini ya miaka 21, Omari Hutchinson, mwenye umri wa miaka 21, katika dirisha hili. Benchi la ufundi la timu hii linamwangalia Omari kama mbadala sahihi wa Bryan Mbeumo ambaye amatarajiwa kujiunga na Manchester United katika dirisha hili.


Jhon Arias

WOLVES iko karibu kufikia makubaliano ya kutoa Pauni 15 milioni kwenda Fluminense kwa ajili ya kumsajili winga wa timu hiyo na Colombia, Jhon Arias, mwenye umri wa miaka 27.  Benchi la ufundi la Wolves limevutiwa sana na kiwango ambacho winga huyu amekionyesha katika michuano ya Kombe la Dunia la klabu iliyofanyika Marekani. Arias mweyewe hataki hata kuikosa fursa hiyo ya kutua Wolves katika dirisha hili.


Philippe Mateta

LIVERPOOL imeendelea kuzungumza na Crystal Palace kuhusu mshambuliaji wao, Jean-Philippe Mateta,28, ikiwa inaweza kuipata saini yake dirisha hili. Inaelezwa Liverpool ilikutana na wawakilishi wa staa huyu pamoja na mchezaji mwenyewe huko Paris. Katika kikao hicho cha siri Mateta na wakala wake wote walivutiwa na mipango ya Liverpool na wapo tayari kufanya nao kazi. Liverpool inapanga kukutana na wawakilishi wa Palace kujadili masuala ya ada ya uhamisho.


Harvey Elliott

WEST Ham imewasiliana na  wawakilishi wa mshambuliaji wa Liverpool, Harvey Elliott  ambaye imepanga kumsajili dirisha hili. Mastaa hawa ambao wote wana umri wa miaka 22, wamekuwa wakihusishwa kuondoka tangu dirisha lililopita la majira ya baridi lakini timu zinazohitaji kuwasajili hazijafikia bei ambayo Liverpool inaihitaji.


Daniel Muno

LICHA ya kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia Crystal Palace hadi mwaka 2028, beki kisiki wa timu hiyo, Mcolombia Daniel Munoz, 29, yupo tayari kuondoka katika kikosi hicho katika dirisha hili na timu kama Manchester City na Chelsea zinahusishwa naye. Mkataba wake una kipengele kinachoiwezesha Palace kuurefusha kwa mwaka mmoja zaidi ikiwa itahitaji kufanya hivyo.