Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Real Madrid, Konate ngoma bado mbichi, awekewa mzigo mezani

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Mabosi wa Madrid wanadaiwa kutaka kusubiri hadi mwisho wa msimu ujao na mkataba wake utamalizika, kisha ndio imsajili bure kama ilivyofanya kwa Trent Alexander Arnold.

LIVERPOOL imempa ofa nono ya mkataba mpya beki wao kisiki raia wa Ufaransa, Ibrahima Konate, 26, ili kuzuia mpango wa Real Madrid inayohitaji sana saini yake.

Mabosi wa Madrid wanadaiwa kutaka kusubiri hadi mwisho wa msimu ujao na mkataba wake utamalizika, kisha ndio imsajili bure kama ilivyofanya kwa Trent Alexander Arnold.

Vigogo wa Liverpool hawataki kuona kilichowatokea kwa Trent kinawatokea tena kwa Konate ndiyo maana inapambana kuhakikisha anasaini mkataba mpya kabla hata ya msimu ujao kuanza.

Staa huyu ni miongoni mwa wachezaji tegemeo wa kikosi cha Liverpool na majogoo hawa wanadaiwa kumpa ofa ya mshahara mpya unaofikia Pauni 250,000 kwa wiki ili tu kumshawishi abaki.

Licha ya juhudi zote ambazo zimefanywa na Liverpool hadi sasa, Konate bado hajafanya uamuzi wowote ikiwa anabaki au ataondoka mwisho wa msimu.

Awali Madrid iliripotiwa kuwasilisha ofa ili kumnunua lakini Liverpool iliwaambia beki huyo hauzwi.

Baada ya kupewa ujumbe huo inaelezwa Madrid imewageukia wawakilishi wake na kuwashawishi kutokubali ofa yoyote ya Liverpool hadi mwisho wa msimu ili wao waweze kumpata kiurahisi.

Kocha mpya wa Madrid, Xabi Alonso inadaiwa ndiye amependekeza jina la beki huyu kwani anaamini akitua atazidi kuboresha safu yao ya ulinzi ambayo msimu uliopita ilikuwa na upungufu.


Son Heung-min

TOTTENHAM inajadili ofa ya Pauni 15 milioni kutoka Los Angeles FC kwa ajili ya nahodha wao Son Heung-min dirisha hili. Staa huyo wa kimataifa wa Korea Kusini alianza kuwindwa na timu kibao tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi lakini alikataa kuondoka kwa wakati huo. Ripoti zinadai Son, 33, hadi sasa bado hajafanya uamuzi ikiwa ataondoka au atabaki ingawa Spurs imempa uhakika uamuzi wowote atakaochukua haitomzuia.


Endrick

REAL Madrid ipo tayari kumtoa kwa mkopo mshambuliaji wao, Endrick dirisha hili la majira ya kiangazi. Mabosi wa Madrid wanataka kumtoa staa huyu kwa mkopo ili kumpa nafasi ya kukua zaidi kisoka kwa kucheza mechi nyingi tofauti na ilivyo sasa ambapo hapewi nafasi kubwa ya kucheza. Hata hivyo, ripoti zinaeleza Endrick mwenyewe hataki kuondoka na anaamini bado anaweza kupambania namba na kucheza katika kikosi cha kwanza cha Madrid.


Adam Aznou

EVERTON imefikia hatua nzuri katika mchakato wao wa  kuipata huduma ya beki wa kushoto wa Bayern Munich, Adam Aznou, 19, dirisha hili. Staa huyu wa kimataifa wa Morocco ameonyesha kutamani sana kutua Everton kwa sababu hapati nafasi ya kutosha kwenye kikosi cha Bayern na hii ndio anaona ni nafasi pekee ya kucheza kwani mbali ya ongezeko la mshahara Everton pia imemhakikishia kumpa nafasi ya kucheza katika kikosi chao cha kwanza.


Alejandro Garnacho

ASTON Villa imeendelea kufanya mazungumzo na Manchester United juu ya uwezekano wa kumpata   winga wa timu hiyo Alejandro Garnacho,21, dirisha hili. Inaaminika mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina anaweza kupatikana kwa takriban Pauni 40 milioni dirisha hili. Garnacho ni miongoni mwa wachezaji ambao kocha wa Man United, Ruben Amorim amewapa ruhusa ya kuondoka kwa sababu hayupo kwenye mipango yake msimu ujao.


Samuel Lino

EVERTON imewasilisha ofa Atletico Madrid kwa ajili ya kuipata saini ya winga wao, Samuel Lino dirisha  hili. Ripoti zinaeleza staa huyo ameshawaambia hadi mabosi wa timu yake anataka kuondoka na Atletico imeonyesha kuwa tayari kumwachia. Fundi huyu mwenye umri wa miaka 25, hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha Atletico sababu ambayo inadaiwa kumsukuma sana kuomba kuondoka.


Morgan Gibbs-White

MABOSI wa Nottingham Forest wapo katika mazungumzo na Aston Villa inayohitaji saini ya kiungo wao Morgan Gibbs-White, 25, dirisha hili. Awali Forest ilikuwa katika majadiliano na Tottenham kwa ajili ya kuwauzia staa huyu lakini ilishindikana baada ya kukerwa na namna viongozi wa Spurs walivyokuwa wakitoka nje ya utaratibu.


James McConnell

INAELEZWA kiungo wa kati wa Liverpool, James McConnell, 20, atasaini mkataba mpya wa muda mrefu na klabu hiyo kabla ya wiki hii kuisha. Liverpool imepanga kumsainisha mkataba mpya, kisha kumtoa kwa mkopo kwenda timu moja wapo ya Ligi Daraja la Kwanza England ili aendelee kuimarika zaidi wakiamini atakuja kuwa tegemeo kwenye timu kwa siku za usoni.