Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rasmi Juventus yaweka mzigo mezani kwa Sancho

TETESI m

Muktasari:

  • Mkataba wa sasa wa Sancho na Man United unamalizika mwaka 2026, lakini kocha Ruben Amorim ameshaweka wazi hana mpango wa kumtumia kwa msimu ujao, hivyo atafute timu atakayoweza kujiunga nayo.

JUVENTUS imewasilisha ofa ya pauni 8.65 milioni pamoja na nyongeza kwenda  Manchester United ili kumsajili winga wa klabu hiyo na timu ya taifa ya England, Jadon Sancho, katika dirisha hili.

Mkataba wa sasa wa Sancho na Man United unamalizika mwaka 2026, lakini kocha Ruben Amorim ameshaweka wazi hana mpango wa kumtumia kwa msimu ujao, hivyo atafute timu atakayoweza kujiunga nayo.

Vigogo wa Juventus waliwasiliana na Man United Jumamosi ya wiki iliyopita na kuwasilisha ofa hiyo ambayo ipo chini ya dau ambalo Mashetani Wekundu hao wanakihitaji.

Awali Man United iliweka wazi kuwa inahitaji kiasi cha Euro 25 milioni kama ada ya uhamisho ya Sancho ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo Chelsea.

Sancho mwenye umri wa miaka 25, anaonekana kuwa mbadala sahihi wa Nico Gonzalez, ambaye kuna uwezekano mkubwa akaachana na Juventus katika dirisha hili.


Conor Gallagher

KIUNGO wa zamani wa Chelsea anayekipiga kwa sasa Atletico Madrid, Conor Gallagher, yuko tayari kurejea tena katika Ligi Kuu England baada ya Newcastle United kudaiwa kuwasilisha ofa mezani ili kumsajili katika dirisha hili. Staa huyu mwenye umri wa miaka 25, mkataba alionao na Atletico unatarajiwa kumalizika mwaka 2029. Msimu uliopita alicheza mechi 50 za michuano yote na kufunga mabao manne.


Benjamin Sesko

AL-Hilal ya Ligi Kuu Saudi Arabia na timu kadhaa kutoka Italia zimeulizia kuhusu mshambuliaji wa RB Leipzig, Benjamin Sesko, ikiwa zinaweza kumpata katika dirisha hili. Staa huyu wa kimataifa wa Slovenia ambaye anawindwa na vigogo mbalimbali barani Ulaya, alikuwa katika rada za Arsenal katika dirisha hili kabla ya washika mitutu hao kujiondoa kutokana na ada kubwa ya usajili ambayo timu yake iliihitaji.


Nayef Aguerd

WEST Ham imeiambia AS Roma kuwa ikiwa inahitaji saini ya  beki wa kimataifa wa Morocco, Nayef Aguerd (29), inapaswa kutoa ada ya uhamisho na kumnunua mazima na si kuomba kumsajili kwa mkopo. Mabosi wa West Ham wamejipanga kusuka kikosi kupitia dirisha hili kusajili mastaa wapya na inataka kutumia pesa itakayopata kwenye mauzo ya Nayef ili kuongezea fungu lao la usajili.


Vanja Milinkovic-Savic

NAPOLI kwa sasa ndio inaongoza katika harakati za kuiwania saini ya kipa wa Torino na timu ya taifa ya Serbia, Vanja Milinkovic-Savic, mwenye umri wa miaka 28, katika dirisha hili. Vanja ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwakani, msimu uliopita alicheza mechi 39 za michuano yote. Kwa mujibu wa ripoti yeye mwenyewe anatamani zaidi kutua Napoli ili kucheza michuano ya kimataifa.


Ferran Torres

KOCHA wa Aston Villa, Unai Emery amependekeza jina la mshambuliaji wa Barcelona, Ferran Torres mwenye miaka 25, na anataka asajiliwe katika dirisha hili. Ripoti zinadai Villa ipo tayari kutoa kiasi kisichopunga pauni 43 milioni kwa ajili ya kuipata saini yake kiasi ambacho kinaonekana kuwa kizuri kwa Barca.


Cristhian Mosquera

JARIBIO la Arsenal la kutaka kumsajili beki wa Valencia na timu ya taifa ya Hispania, Cristhian Mosquera, 21, limekwama baada ya timu hiyo ya La Liga kuhitaji zaidi ya pauni 20 milioni kama ada yake ya uhamisho. Mosquera ni miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Valencia na msimu uliomalizika amecheza mechi 41.


Ollie Watkins

NEWCASTLE United italazimika kukubali kutoa pauni 100 milioni katika dirisha hili ikiwa inahitaji saini ya  mshambuliaji wa Aston Villa na timu ya taifa ya England, Ollie Watkins, mwenye miaka 29. Vigogo wa Newcastle wanadaiwa kuhitaji sana huduma ya Watkins lakini ada ya hiyo ya uhamisho inayohitajika na Villa inaonekana kuwa ni kikwazo.