Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rashford afikiria kurudi Man United

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Rashford mwenye umri wa miaka 28, awali aliondoka katika viunga vya Old Trafford baada ya kupishana na Amorim ambaye alidai supastaa huyo hafanyi vile ambavyo mkufunzi huyo alikuwa anataka.

MSHAMBULIAJI wa Manchester United ambaye na timu ya taifa ya England, ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo Barcelona, Marcus Rashford anadaiwa kufikiria kurudi nyumbani mwisho wa msimu huu baada ya kufukuzwa kwa kocha Ruben Amorim.

Rashford mwenye umri wa miaka 28, awali aliondoka katika viunga vya Old Trafford baada ya kupishana na Amorim ambaye alidai supastaa huyo hafanyi vile ambavyo mkufunzi huyo alikuwa anataka.

Tangu ajiunge na Barcelona mchezaji huyo amekuwa katika kiwango bora kiasi cha kudaiwa kuwa anaweza akasaini mkataba wa moja kwa moja wa kuendelea kusalia katikatimu hiyo.

Hata hivyo, changamoto kubwa imekuwa ni kiasi cha pesa ambacho Man United inazitaka ili kumuuza mchezaji huyo kuonekana kuwa ni nyingi kwa mabosi wa Barcelona.

Mkataba wa sasa wa Rashford na Man United unatarajiwa kumalizika ifikapo 2028 na tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 25 za michuano yote na kufunga mabao saba, huku akitoa asisti 11.

Mabosi wa Atletico Madrid pia wameonyesha nia ya kumsajili staa huyo na wapo tayari kulipa zaidi ya Pauni 40 milioni kuhakikisha wanaipata huduma yake.


Matt Targett

NEWCASTLE United inafikiria kumrejesha mapema beki wa kushoto raia wa England, Matt Targett, 30, ambaye anacheza kwa mkopo Middlesbrough inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza.

Mpango wa Newcastle kutaka kumrudisha Targett ambaye alisaini mkataba wa mkopo wa msimu mmoja Middlesbrough umechochewa na majeraha ya Dan Burn, 33 ambaye atakosekana kwa muda mrefu.


Lorenzo Torriani

ARSENAL inataka kumsajili kipa wa AC Milan na timu ya taifa ya Italia, Lorenzo Torriani, 20. Maskauti wa Washika Mitutu wa London wanamwangalia staa huyo muda sasa na wameandika ripoti inayopendekeza asajiliwe baada ya kuridhishwa na kiwango chake bora. Awali, kinda huyo alionekana kama mbadala sahihi wa Mike Maignan anayeondoka mwisho wa msimu huu.


Tyler Adams

KKIUNGO wa Bournemouth na timu ya taifa ya Marekani, Tyler Adams 26, anatajwa kuwa katika rada za  Manchester United inayotaka kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Kiwango cha Tyler alichoonyesha tangu msimu uliopita akiwa na Bournemouth kiwavutia Masheta Wekundu.

Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2028 na tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 16 za michuano yote.


Conor Gallagher

MANCHESTER United bado ina mpango wa kumsajili kiungo wa Atletico Madrid, Conor Gallagher katika dirisha hili la usajili la Januari licha ya kumfukuza kocha Ruben Amorim.

Gallagher, 25, anatajwa kuwa kwenye orodha ya Man United. Hata hivyo, baadhi ya taarifa zinadai Atletico haitaki kumwachia nyota huyo.

Staa huyo wa kimataifa wa England, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2029.


Jamie Leweling

BOURNEMOUTH inajipanga kulipa Euro 40 milioni kwa ajili ya kumsajili winga wa Stuttgart na timu ya taifa ya Ujerumani, Jamie Leweling ili akawe mbadala wa winga wa kimataifa wa Ghana, Antoine Semenyo, 25, ambaye yupo karibu kujiunga na Manchester City.

Hata hivyo, mabosi wa Stuttgart wamekataa ofa hiyo na kusisitiza kwamba wanahitaji kiasi kisichopungua Euro 50 milioni kwa ajili ya kumuuza.


Federico Chiesa

JUVENTUS imeanza mazungumzo na Liverpool kwa ajili ya kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa timu hiyo na Italia, Federico Chiesa mwenye umri wa miaka 28.

Chiesa ameonyesha nia ya kutaka kurejea Juventus aliyowahi kuitumikia kati ya 2022 hadi 2024 kwa sababu hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha Liverpool.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 yupo tayari hata kupunguza mshahara wake wa sasa ili kuhakikisha dilo hilo linafanikiwa.


Kobbie Mainoo

KIUNGO wa Manchester United na timu ya taifa ya England, Kobbie Mainoo, 20, huenda akabaki.

Mshambuliaji wa timu hiyo na Uholanzi, Joshua Zirkzee, 24, na kiungo wa kimataifa wa  Uruguay, Manuel Ugarte, 24, wote walikuwa wanapanga kuondoka katika dirisha hili la majira ya baridi ikiwa kocha Ruben Amorim angeendelea kusalia katika kikosi hicho.

Inaelezwa mastaa hao walichoshwa na namna Amorim alivyokuwa akiwachukulia kwa kuwasugulisha benchi.