Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mchongo wa Napoli kwa Mainoo upo hivi

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Mainoo amekuwa akihusishwa kuondoka tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi kwa sababu hapati nafasi ya kutosha ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Man United.

NAPOLI bado imeendelea kuonyesha nia ya kumsajili kiungo wa Manchester United na timu ya taifa ya England, Kobbie Mainoo, 20, lakini dili hilo litawezekana tu ikiwa winga wa kimataifa wa Uholanzi, Noa Lang, 26, ataondoka ndani ya klabu hiyo ya Italia.

Mainoo amekuwa akihusishwa kuondoka tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi kwa sababu hapati nafasi ya kutosha ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Man United.

Napoli inahitaji kwanza kumuuza Lang ili kupata fedha kabla ya kuanza mazungumzo rasmi na Man United.

Hadi sasa, Manchester United haijaweka wazi msimamo wake kuhusu kumuuza Mainoo, na mara kadhaa ambapo timu zimekuwa zikiwasilisha ofa imekuwa ikikataa.

Mkataba wa Mainoo na Man United unatarajiwa kumalizika mwaka 2027 na tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 12 za michuano yote na kutoa asisti moja.

Mchezaji huyo zao la akademia ya Manchester United hajaanzishwa hata katika mechi moja ya Ligi Kuu England msimu huu.


Federico Chiesa

ROMA imepanga kufanya mabadiliko makubwa katika safu yao ya ushambuliaji ndani ya madirisha mawili yajayo ya usajili na winga wa Liverpool na timu ya taifa ya Italia, Federico Chiesa, 28, ni miongoni mwa malengo yao.

Chiesa ana uzoefu mkubwa katika Serie A jambo linalomfanya kuwa chaguo linalovutia kwa klabu hiyo ya Roma. Liverpool bado hawajaweka wazi kama wako tayari kumuuza.


Matteo Guendouzi

KIUNGO wa Lazio na timu ya taifa ya Ufaransa, Matteo Guendouzi, 26, ameingia kwenye rada ya klabu mbili za Ligi Kuu England, huku Fenerbahce ya Uturuki ikiwa nayo imewasilisha ofa ili kumsajili.

Ripoti zinaeleza mabingwa hao wa Uturuki wamewasilisha ofa ya takribani Euro 27 milioni ili kumununua. Guendouzi amekuwa mchezaji tegemeo katika kikosi cha Lazio.


Dusan Vlahovic

BARCELONA inaripotiwa kuwa inaongoza katika mbio za kumsajili straika wa Juventus na timu ya taifa ya Serbia, Dusan Vlahovic, 25, ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Vlahovic amekuwa akifuatiliwa pia na AC Milan pamoja na Bayern Munich, klabu ambazo zinafikiria kuwasilisha ofa mwisho wa msimu.Juventus inataka kumuuza Januari hii ili kuepuka kumpoteza bure mwisho wa msimu.



Morgan Rogers

CHELSEA inadaiwa kuwa katika maandalizi ya kuwasilisha ofa nono ya Euro 150 milioni kwa ajili ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa Aston Villa na timu ya taifa ya England, Morgan Rogers, 23. Rogers amevutia klabu nyingi kubwa baada ya kuonyesha kiwango bora akiwa na Villa na Chelsea wanamwona kama sehemu muhimu ya mradi wao mpya wa kujenga kikosi chenye wachezaji wengi vijana.

Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2031.


Omar Marmoush

ASTON Villa imeonyesha nia ya kumsajili winga wa kimataifa wa Misri, Omar Marmoush, 26, ambaye amekuwa akipata wakati mgumu wa kucheza mara kwa mara ndani ya kikosi cha Manchester City.

Marmoush ameshindwa kupata namba ya uhakika kutokana na ushindani mkubwa uliopo Man City chini ya kocha Pep Guardiola. Manchester City inadaiwa kuwa ipo tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya kumuuza fundi huyo.


Sandro Tonali

CHELSEA inaendelea kumfuatilia kwa karibu kiungo wa Newcastle United na timu ya taifa ya Italia, Sandro Tonali, 25, kwa lengo la kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Tonali, ambaye alijiunga na Newcastle akitokea AC Milan, bado anatajwa kuwa kwenye rada ya klabu kadhaa kubwa barani Ulaya kutokana na ubora wake. Hata hivyo, Newcastle hawako tayari kumuachia kirahisi staa huyo isipokuwa kama itapewa dau kubwa.


Rodri

REAL Madrid inaendelea kuangalia uwezekano wa kumsajili kiungo wa Manchester City na timu ya taifa ya Hispania, Rodri, lakini hawana mpango wa kufanya dili hilo katika dirisha hili.

Madrid wanatarajia kusubiri hadi katika dirisha la majira ya kiangazi wakati ambapo Rodri, 29, ataingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake na Man City, hali itakayoweza kushusha bei yake.

Rodri ni mhimili muhimu katika mafanikio ya Manchester City.