Chelsea yamuandalia ofa Vinicius Jr
Muktasari:
- Hata hivyo, licha ya ofa hiyo kubwa, Real Madrid inaonekana kutokuwa tayari kumwachia nyota huyo kwa urahisi, kwani anachukuliwa kama sehemu ya msingi ya mradi wao wa muda mrefu.
CHELSEA inadaiwa kuandaa ofa nono yenye thamani ya Euro 150 milioni kwa lengo la kuishawishi Real Madrid kumuachia winga wao mahiri wa kimataifa wa Brazil, Vinicius Jr, mwenye umri wa miaka 25.
Hata hivyo, licha ya ofa hiyo kubwa, Real Madrid inaonekana kutokuwa tayari kumwachia nyota huyo kwa urahisi, kwani anachukuliwa kama sehemu ya msingi ya mradi wao wa muda mrefu.
Hadi sasa hatma ya Vinicius kuhusu kuongeza mkataba haijajulikana huku mazungungumzo yakionekana kusuasua.
Shida inayodaiwa kuwa inachelewesha mchakato huo ni madai makubwa ya mshahara ambao Vinicius anautaka jambo ambalo limewafanya vigogo wa Madrid kujipa muda wa kujadili kwa kina kabla ya kufanya uamuzi.
Chelsea inataka kuwasilisha ofa ya Euro 150 milioni ambayo Euro 125 milioni italipwa moja kwa moja kisha Euro 25 milioni zilizobakia zitalipwa kwa kuzingatia kiwango ambacho staa huyo atakionyesha pamoja na kucheza idadi fulani ya mechi au mabao.
Mabosi wa Chelsea wanaamini huu ni wakati mwafaka wa kumpata Vinicius ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2027.
Tangu kusajiliwa kwa Kylian Mbappe, ufalme wa Vini Real Madrid unaonekana kupotea, huku mshindi wa huyo wa Kombe la Dunia akiwa na Ufaransa akionekana kutawala kikosini.
Adam Wharton
REAL Madrid imejiunga na Chelsea, Liverpool, Manchester City na Manchester United katika mbio za kuwania saini ya kiungo wa kati wa Crystal Palace na timu ya taifa ya England, Adam Wharton, mwenye umri wa miaka 21.
Wharton amekuwa katika kiwango bora tangu ajiunge na Palace kwa mkataba unaomalizika mwaka 2029 na tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 27 za michuano yote. Palace haina mpango wa kumzuia kuondoka ikija ofa nono.
Maghnes Akliouche
TOTTENHAM imetuma maskauti wake kumuangalia kwa karibu winga wa AS Monaco na timu ya taifa ya Ufaransa, Maghnes Akliouche, mwenye umri wa miaka 23.
Maskauti hao walimshuhudia nyota huyo akicheza dhidi ya Lyon mwishoni mwa wiki iliyopita, ambapo aliendelea kuonyesha kiwango bora akitengeneza nafasi za kutosha.
Akliouche anatajwa kuwa mmoja kati ya wanaotazamwa na maskauti wa timu mbalimbali.
Nathan Ake
AC Milan inaendelea kufuatilia kwa karibu hali ya beki wa Manchester City na timu ya taifa ya Uholanzi, Nathan Ake, mwenye umri wa miaka 30.
Mabosi wa Milan wanahitaji sana huduma ya Ake kwa ajili ya kuboresha safu yao ya ulinzi na wanaamini uzoefu wake unaweza kuwa chachu ya kuongeza ubora kwenye kikosi chao.
Hata hivyo, bado haijulikani kama Manchester City itakuwa tayari kumruhusu kuondoka kirahisi katika kikosi cha Pep Guardiola.
William Osula
EINTRACHT Frankfurt iko kwenye mazungumzo na Newcastle United kuhusu kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Denmark, William Osula, 22.
Osula bado hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha Newcastle, hali inayofanya klabu hiyo ya Bundesliga kuona fursa ya kumsajili.
Hadi sasa hakuna makubaliano bado, lakini mazungumzo yanaendelea huku pande zote zikijaribu kufikia makubaliano ya ada ya uhamisho.
Maghnes Akliouche
TOTTENHAM imetuma maskauti wake kumuangalia kwa karibu winga wa AS Monaco na timu ya taifa ya Ufaransa, Maghnes Akliouche, mwenye umri wa miaka 23.
Maskauti hao walimshuhudia nyota huyo akicheza dhidi ya Lyon mwishoni mwa wiki iliyopita, ambapo aliendelea kuonyesha kiwango bora akitengeneza nafasi za kutosha.
Akliouche anatajwa kuwa mmoja kati ya wanaotazamwa na maskauti wa timu mbalimbali.
Fermin Lopez
BARCELONA inadaiwa kuwa inajadili ofa ya Pauni 70 milioni iliyowasilishwa na Sunderland kwa ajili ya kumnunua winga wao wa kimataifa wa Hispania, Fermin Lopez, mwenye umri wa miaka 22.
Lopez amekuwa na panda shuka nyingi katika kikosi cha Barca akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara, lakini bado ameendelea kuwa mchezaji tegemeo kwa Hans Flick ambaye anatamani aendelee kuwa naye.
Hata hivyo, Barca inaona ofa iliyowekwa ni kubwa sana hivyo inafikiria kumuuza. Mkataba wa Lopez unatarajiwa kumalizika mwaka 2029.
Omar Marmoush
WINGA wa Manchester City na timu ya taifa ya Misri, Omar Marmoush, mwenye umri wa miaka 26, huenda akatua Aston Villa au Tottenham Hotspur katika dirisha lijalo.
Hata hivyo, taarifa za ndani kutoka kwa watu wa karibu na mshambuliaji huyu zinadai, Marmoush mwenyewe anataka kubaki Etihad na kupambana ili kupata nafasi katika kikosi cha kwanza.
Raheem Sterling
WINGA wa Chelsea na England, Raheem Sterling, mwenye umri wa miaka 31, anaonekana kuwa mbioni kujiunga na Newcastle United katika dirisha la usajili la Januari.
Newcastle imeonyesha nia ya kumsajili staa huyu ambaye hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha Chelsea na imevutiwa sana na uzoefu wake. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.
Msimu uliopita alicheza mechi 28 za michuano yote.