Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

PRESHA: Guardiola aulizia kama Mourinho anatua Trafford

Pep Guardiola (kushoto) na Jose Mourinho

Muktasari:

KWANI Pep Guardiola vipi? Kulikoni, anamwogopa Jose Mourinho? Maana ukisikia stori yake, utakuwa na maswali mengi bila majibu.

KWANI Pep Guardiola vipi? Kulikoni, anamwogopa Jose Mourinho? Maana ukisikia stori yake, utakuwa na maswali mengi bila majibu.

Kocha huyo mtarajiwa wa Manchester City ameripotiwa kuwatuma watu kufuatilia kama mpinzani wake wa siku nyingi, Mourinho atakuwa kocha mpya wa Manchester United mwishoni mwa msimu huu.

Kwa mujibu Phil Cadden, swahiba wa kocha huyo, Pep amekuwa akiwauliza marafiki zake kutaka wafuatilie na kupeleleza kwa umakini kutambua kama Mourinho atatua Old Trafford mwishoni mwa msimu huu.

Guardiola anafahamu vita ya Mourinho ilivyo baada ya awali kumenyana jino kwa jino walipokuwa Hispania, mmoja akiinoa Barcelona na mwingine akiwa na mahasimu wao, Real Madrid.

Kama Mourinho atachukua kibarua cha kuinoa Man United, jambo hilo litawafanya makocha hao wawili wenye upinzani mkali kupambana kwenye mechi za mahasimu wengine ndani ya Ligi Kuu England kwenye Manchester derby.

Cadden alisema: “Pep anataka kufahamu kama Mourinho amekubaliana na Manchester United. Sidhani kama anahofia, bali anaamini maisha yatakuwa matamu sana kama Jose atakuwa Man United.”

Makocha hao wawili walichuana vikali kwa misimu miwili kwenye La Liga na Barcelona ikiwa chini ya Guardiola iliitambia Real Madrid kwa kubeba ubingwa wa ligi kwenye msimu wa kwanza kabla ya Mourinho kujibu mapigo msimu uliofuatia.

Upinzani wa Mourinho na Guardiola umeripotiwa si wa uwanjani tu, bali makocha hao wamekuwa wakirushiana maneno ya kutambiana hadi kwenye vyombo vya habari.

Halitakuwa jambo la kushangaza kama Mourinho atakubali kibarua cha kuinoa Man United mwishoni mwa msimu huu baada ya mambo kwenda kombo chini ya Louis van Gaal na wakielekea kukosa nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu mwingine.

Mwandishi wa soka, Liam Canning amebanisha kuwa na uhakika mkubwa kwamba makocha hao wenye viwango vikubwa watachuana vikali jijini Manchester msimu ujao. Guardiola ameshasaini mkataba wa kuinoa Man City na kitu kinachosubiriwa kwa sasa ni Mourinho tu kumalizana na Man United.

Wachambuzi wengi wa mchezo wa soka nchini England wanahitaji Mourinho atue kwenye kikosi cha Man United ili kupata nafasi ya kushuhudia mpambano mkali dhidi ya Guardiola wakati timu zao zitakapomenyana kwenye Manchester derby.

Hata hivyo, kitu ambacho mabosi wa Old Trafford hawaoni kama Mourinho atamuweza Guardiola ni rekodi zake, ambapo Mreno huyo ameshinda mara tatu tu katika mechi 15 alizocheza dhidi ya mpinzani wake. Kinyume chake, Guardiola ameshinda mara saba.

Katika msimu ambao mambo yanaonekana kuwa magumu, huku Man United ikiwa bado haina uhakika wa kubeba taji lolote, mashabiki wa timu hiyo wanatarajia kuwapa presha mabosi wao kuhakikisha wanambadilisha kocha wa sasa, Mdachi Van Gaal na kumpa kibarua Mourinho.

Mashabiki wa pande zote, Man United na Man City watapenda kurudisha upinzani mkali kwenye mechi zao na hilo litanoga zaidi kama upande mmoja atakuwa Mourinho na mwingine Guardiola.