Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Page aachwa kikosi cha Leicester, Man United yamuwania

PAGE Pict

Muktasari:

  • Page hakujumuishwa kwenye kikosi hicho licha ya kuwa fiti, hali inayozua zaidi maswali kuhusu mustakabali wake ndani ya Leicester.

LEICESTER, ENGLAND: MANCHESTER United imepata matumaini zaidi katika harakati zake za kumsajili kinda wa Leicester City, Louis Page, baada ya mchezaji huyo kuachwa nje ya kikosi kilichokutana na Notts County.

Page hakujumuishwa kwenye kikosi hicho licha ya kuwa fiti, hali inayozua zaidi maswali kuhusu mustakabali wake ndani ya Leicester.

Kocha wa Leicester, Russell Martin, aliwahi kuthibitisha kuwa klabu hiyo ilikataa ofa kutoka kwa moja ya klabu za Ligi Kuu England iliyokuwa ikimwania Page.

Hata hivyo, uamuzi wa kumuacha nje katika mchezo huo umeongeza tetesi kwamba huenda mchezaji huyo yuko mbioni kuondoka Leicester.

Taarifa zinaeleza kuwa Page ameamua kujiunga na Manchester United licha ya pia kuvutiwa na Arsenal.

United imekuwa ikifuatilia kwa karibu maendeleo ya kinda huyo, ambaye sasa anaonekana kuwa karibu kuanza ukurasa mpya wa maisha yake ya soka ikiwa makubaliano kati ya klabu hizo yatakamilika.