Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Okocha: Ile ya Osimhen, Lookman safi sana

OKOCHA Pict

Muktasari:

  • Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 52 alikuwa sehemu ya kikosi cha Nigeria kilichotwaa ubingwa wa AFCON mwaka 1994, pamoja na Medali ya Dhahabu ya Olimpiki ya Atlanta 1996, na ametoa maoni yake kuhusu mvutano uliotokea kwenye mechi ya hatua ya 16 bora dhidi ya Msumbiji.

CASABLANCA, MOROCCO: NAHODHA wa zamani wa Super Eagles na fundi wa boli, Jay-Jay Okocha amesema mvutano uliopo kati ya Victor Osimhen na Ademola Lookman una manufaa makubwa kwa timu ya taifa ya Nigeria hasa katika kipindi hiki cha mashindano ya Afcon 2025.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 52 alikuwa sehemu ya kikosi cha Nigeria kilichotwaa ubingwa wa AFCON mwaka 1994, pamoja na Medali ya Dhahabu ya Olimpiki ya Atlanta 1996, na ametoa maoni yake kuhusu mvutano uliotokea kwenye mechi ya hatua ya 16 bora dhidi ya Msumbiji.

Katika mchezo huo dhidi ya Msumbiji, wawili hao walikuwa tayari wamefunga mabao, huku Victor Osimhen akifunga mawili, kabla ya mvutano kuzuka dakika ya 63 baada ya kushindwa kupeana pasi.

Bruno Onyemaechi alijikuta katika nafasi isiyo ya kawaida pembeni mwa boksi la Msumbiji, na licha ya Osimhen kuwa huru upande wa kulia, beki huyo aliamua kupiga mwenyewe badala ya kumpa pasi mshambuliaji huyo, jambo lililomkasirisha Osimhen.

Mpira ulipomfikia Lookman, aliamua kurudisha mpira nyuma na kutuliza mchezo badala ya kuendelea kushambulia. Osimhen alifoka akimwambia mchezaji huyo wa Atalanta, “Hey, huu ni mchezo wa timu,” naye Lookman akajibu, “Lakini tayari umefunga mabao mawili.”

Juhudi za nahodha Wilfred Ndidi kumtuliza mshambuliaji wa Galatasaray, zilikutana na dharau na Osimhen alitolewa muda mfupi baadaye baada ya kukataa kushiriki kikamilifu katika mzunguko wa mchezo.

Kama alivyowahi kusema Mikel Obi, nahodha wa zamani wa Super Eagles, Okocha alisisitiza kuwa migogoro kama hiyo inaonyesha njaa ya ushindi ndani ya timu.

“Mambo kama haya hutokea na wakati mwingine napenda kuyaona,” amesema.