Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal ilipoishia njiani rekodi ya kutoruhusu mabao

ARSENAL Pict

Muktasari:

  • Hapo, Sir Alex alikuwa na maana wachezaji wa kwenye safu ya ushambuliaji watafunga mabao ili kusaidia timu kushinda mechi zake, lakini ukuta imara kwenye mabeki, utalinda ushindi huo uliopatikana na hilo likifanyika kwa msimu mzima, basi timu husika itakuwa imetimiza lengo ya kubebe taji.

LONDON, ENGLAND: “WASHAMBULIAJI wanashinda mechi, mabeki wanashinda mataji.” Hayo ni maneno ya gwiji, Sir Alex Ferguson.

Hapo, Sir Alex alikuwa na maana wachezaji wa kwenye safu ya ushambuliaji watafunga mabao ili kusaidia timu kushinda mechi zake, lakini ukuta imara kwenye mabeki, utalinda ushindi huo uliopatikana na hilo likifanyika kwa msimu mzima, basi timu husika itakuwa imetimiza lengo ya kubebe taji.

Arsenal ya msimu huu, baada ya kukaribia kulibeba taji la Ligi Kuu England kwa misimu mitatu mfululizo, ikikomea nafasi ya pili, huku mambo yakitibuka kwenye dakika za mwisho, ilionekana kuwa siriazi kwenye hilo baada ya kuunda safu imara kabisa ya mabeki kwenye mechi zake.

Arsenal ilicheza mechi nane bila ya kuruhusu bao kwenye nyavu zao katika mechi za michuano yote ilizocheza msimu huu. Kwenye Ligi Kuu England, ilicheza mechi nne mfululizo bila ya kuruhusu bao kwenye nyavu zao.

Jambo hilo lilimwibua kocha wa wapinzani wa Arsenal kwenye mbio za ubingwa, Pep Guardiola wa Manchester City, aliposema Arsenal ya Mikel Arteta imekuwa na beki bora, hairuhusu bao kabisa, kisha akaomba dua mbaya, akiamini wataruhusu bao tu.

Na hakika, dua hiyo ya Guardiola ni kama imejibu haraka, baada ya wikiendi iliyopita, Arsenal kutibua rekodi yake ya kucheza mechi nyingi bila ya kuruhusu bao kwenye nyavu zao baada ya kumfanya kipa wao, David Raya kuokota mipira nyavuni mara mbili katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Sunderland, uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Mechi hiyo si tu Arsenal imedondosha pointi, bali imetibua rekodi yao ya kutoruhusu bao. Mambo yametibuka.

Hata hivyo, kwenye Ligi Kuu England kuna timu kadhaa zilizowahi kuweka rekodi ya kucheza mechi nyingi bila ya kuruhusu mpira kugusa kwenye nyavu zao.


Everton – (msimu 1994/95, mechi 7)

Everton ilimaliza nafasi ya 15 kwenye msimamo katika msimu wa 1994/95 na ingekuwa kwenye hatari ya kushuka daraja kama si maajabu yao hayo ya kucheza mechi saba bila ya kuruhusu bao. Ikiwa chini ya kocha Mike Walker na baadaye mrithi wake Joe Royle, Everton ilicheza mechi saba bila ya kuruhusu bao kati ya Novemba 1 na Desemba 17, huku kwenye mechi hizo ikipata ushindi dhidi ya Liverpool, Chelsea na Leeds United.

ARS 01

Southampton – (msimu 2000/01, mechi 7)

Glenn Hoddle ndiye aliyekuwa kocha wa Southampton katika sehemu kubwa ya msimu wa 2000/01 na aliongoza timu hiyo kucheza mechi saba bila ya kuruhusu nyavu zake kuguswa kabla ya kuondoka. Hilo lilitokea kati ya Januari 13 na Machi 17, Hoddle aliifanya Southampton kuwa timu ngumu kufungika katika mechi hizo na hivyo kuandikisha rekodi hiyo ya kibabe kabisa katika historia ya Ligi Kuu England.


Middlesbrough – (msimu 2003/04, mechi 7)

Kocha Steve McClaren alishuhudia akikiongoza kikosi chake kucheza mechi saba bila ya kuruhusu bao wakati alipokuwa akiinoa Middlesbrough katika msimu wa 2003/04. Licha ya kuambulia pointi moja tu kati ya 15 za kwanza, kiwango cha Boro kiliimarika kwenye safu yake ya ulinzi na kucheza kucheza mechi kibao bila ya kuruhusu bao, ilipocheza mechi saba kati ya Oktoba 26 na Desemba 13. Ilimaliza ya 11.


Liverpool – (msimu 2019/20, mechi 7)

Chini ya kocha Jurgen Klopp, Liverpool ilikuwa kwenye kiwango bora sana na si tu kwenye kufunga mabao, bali kwenye kuwadhibiti pia wapinzani wasiguse nyavu zao, hasa msimu wa 2019/20 iliponyakua taji hilo. Katika msimu huo, Liverpool ilicheza mechi saba mfululizo bila ya kuruhusu nyavu zake kuguswa kati ya Desemba 7 na Januari 19 na kuvuna pointi 99 zilizowapa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huo.

ARS 02

Man United – (msimu 1996/97 & 1997/98, mechi 7)

Hiki ni kipindi cha kwanza kwa Manchester United mara mbili kuingia kwenye rekodi hiyo ya kibeba ya kucheza mechi nyingi mfululizo bila ya kuruhusu bao kwenye nyavu zao. Sir Alex Ferguson aliongoza timu yake kuweka rekodi hiyo kwa misimu miwili tofauti na ilianzia mwishoni mwa msimu wa 1996/97 na kuendelea msimu mwingine, mechi saba bila ya kuruhusu bao. Hata hivyo msimu wa 1997/98 ilikosa taji.

ARS 04

Arsenal – (msimu 1997/98, mechi 8)

Katika msimu wake wa kwanza mzima katika kikosi cha Arsenal, kocha Arsene Wenger alifanikiwa kuipa timu hiyo taji la ubingwa wa Ligi Kuu England ilipomaliza kileleni mbele ya Manchester United ya Sir Alex Ferguson. Katika msimu huo, Arsenal ilicheza mechi nane bila ya kuruhusu bao kati ya Januari 31 na Machi 31 na kufanikiwa kwenda kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu England kibabe kabisa huku ikicheza soka la kuvutia.


Liverpool – (2005/06, mechi 8)

Ikitokea kwenye historia ya kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kupindua matokeo kibabe kabisa dhidi ya AC Milan, Liverpool chini ya kocha Rafael Benitez ilikwenda kwenye Ligi Kuu England na kumaliza nafasi ya tatu msimu wa 2005/06, pointi tisa nyuma ya mabingwa, Chelsea. Lakini, katika msimu huo, kati ya Oktoba 29 na Desemba 26, Liverpool ilicheza mechi nane bila ya kuruhusu bao.

ARS 03

Chelsea – (msimu 2006/07, mechi 8)

Huu ulikuwa msimu wa tatu kwa José Mourinho katika awamu yake ya kwanza ya kuinoa Chelsea na miamba hiyo ilicheza mechi nane bila ya kuruhusu bao kati ya Januari 31 na Aprili, huku moja ya ushindi muhimu katika kipindi hicho ulikuwa dhidi ya mahasimu wa London, Tottenham alipowachapa 1-0. Hata hivyo, licha ya kuwa na ngome imara ya mabeki, Chelsea ilipoteza ubingwa kwa Man United.


Chelsea – (msimu 2004/05, mechi 10)

Katika mkutano wake wa kwanza wa waandishi wa habari baada ya kutua Chelsea, Jose Mourinho alijitambulisha kwa jina la “The Special One” katika majira ya kiangazi 2004 na hakika jina hili lilikuwa na maana Stamford Bridge alipowapa taji la ubingwa wa Ligi Kuu England na kuiongoza timu hiyo ikicheza mechi 10 mfululizo bila ya kuruhusu bao. Hiyo ilikuwa kati ya Desemba 18 na Februari 12.


Man United – (msimu 2008/09, mechi 14)

Si kitu kinachoshangaza kuona Manchester United inashikilia rekodi ya kuwa timu iliyocheza mechi nyingi mfululizo bila ya kuruhusu bao kwenye Ligi Kuu England. Kipindi hicho kipa wao akiwa Mdachi, Edwin van der Sar katika msimu wa 2008/09, Man United ilicheza mechi 14 mfululizo bila ya kuruhusu nyavu zao kuguswa, huku jambo hilo likiwatokea kati ya Novemba 15 na Februari 18.