Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ni Senegal, Morocco fainali Afcon 2025

Morocco Pict

Muktasari:

  • Morocco itakabiliana na Senegal katika fainali ya Jumapili, ambapo Simba wa Teranga wamefika hatua hiyo baada ya kuwachapa Misri  1-0 shukrani kwa bao la Sadio Mane kwenye kipindi cha pili.

RABAT, MOROCCO: WENYEJI wa mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) 2025, Morocco wamefanikiwa kutinga fainali ya michuano hiyo baada ya kuichapa Nigeria kwa penalti 4-2 katika mchezo uliofanyika Rabat.

Baada ya sare ya bila kufungana kwa dakika 120, hatimaye mechi ilifikia kwenye hatua ya kupigiana penalti ndipo iliposhuhudiwa Super Eagles ikikosa mikwaju miwili wakati Simba wa Atlas ikikosa mkwaju mmoja.

Youssef En-Nesyri alifunga penalti ya ushindi baada ya Yassine Bounou kuokoa mikwaju miwili ya Samuel Chukwueze na Bruno Onyemaechi.

Hii inamaanisha Simba wa Atlas wamefikiwa kutinga fainali yao ya kwanza ya Afcon tangu 2004, huku wakitaka kuinua taji hilo kwa mara ya kwanza tangu 1976.

Morocco itakabiliana na Senegal katika fainali ya Jumapili, ambapo Simba wa Teranga wamefika hatua hiyo baada ya kuwachapa Misri  1-0 shukrani kwa bao la Sadio Mane kwenye kipindi cha pili.