Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ngoma imehama… Burudani sasa ipo huku

IMEHAMA Pict

Muktasari:

  • Timu kubwa za Ligi Kuu England zimeingia katika maandalizi makali ya msimu mpya wa 2025/26 kwa kucheza mechi za kirafiki katika mataifa tofauti duniani.

LONDON, ENGLAND: BAADA ya kumalizika kwa burudani ya michuano ya Kombe la Dunia la Klabu sasa, macho na masikio yanageuziwa katika mechi za maandalizi ya msimu ya timu mbalimbali kubwa duniani.

Timu kubwa za Ligi Kuu England zimeingia katika maandalizi makali ya msimu mpya wa 2025/26 kwa kucheza mechi za kirafiki katika mataifa tofauti duniani.

 Hii ni hatua muhimu kwa makocha kujaribu mifumo yao ya uchezaji, kuwapa nafasi wachezaji wapya kwa ajili ya kuhakikisha zinafanya vizuri msimu ujao.

Manchester United imepanga kuweka kambi Marekani ambako inatarajiwa kucheza mechi dhidi ya West Ham, Bournemouth na Everton katika miji ya Las Vegas, San Diego na Orlando kuanzia Julai 23 hadi 30.

Hata hivyo, kabla ya kuondoka Ulaya, itacheza pia dhidi ya Leeds United Julai, 19,  jijini Stockholm, Sweden kwenye Uwanja wa Friends.

Mechi ya mwisho ya maandalizi ya msimu kwa mashetani wekundu itapigwa jijini Manchester dhidi ya Fiorentina Agosti, 9  kwenye Uwanja wa Old Trafford.

Kocha Ruben Amorim anatarajiwa kutumia mechi hizi kujaribu kujenga upya kikosi baada ya kufanya vibaya sana msimu uliopita.

Chelsea ambayo jana ilicheza fainali ya Kombe la Dunia la Klabu, kambi yao ya maandalizi ya msimu pia itakuwa huko huko Marekani.

Wataanza kwa kukabiliana Club America ya Mexico, Julai, 21 jijini Atlanta kwwenye Uwanja wa Mercedes-Benz, kabla ya kuvaana na Celtic ya Scotland Julai, 24,  jijini Chicago katika Uwanja wa Soldier .

Mechi nyingine ni dhidi ya Real Madrid Julai, 27, itakayopigwa New Jersey kwenye Uwanja MetLife na mwisho itamaliza na AC Milan Agosti 1.

Liverpool pia ipo Marekani chini ya kocha wake Arne Slot.

Kikosi hicho kitaanza kampeni ya maandalizi ya msimu dhidi ya Real Betis Julai, 23, jijini Pittsburgh, kwenye Uwanja wa Acrisure, kisha kitavaana na Sevilla Julai, 27,  jijini Philadelphia, kabla ya kumalizia kwa Bayern Munich Agosti 01, jijini New Jersey.

Kwa upande wa Arsenal, itaanza ziara yake Marekani kwa mchezo dhidi ya Manchester City Julai, 22, jijini Los Angeles, na baadaye itakutana na Inter Milan Julai, 27, jijini  Miami katika dimba la  Hard Rock kabla ya kwenda Singapore kwa ajili ya kucheza dhidi ya Bayer Leverkusen Agosti 02, kwenye Uwanja wa Taifa wa Singapore (National Stadium).

Manchester City nayo pia haiko nyuma. Matajiri hawa wa jiji la Manchester, wanatarajiwa kucheza dhidi ya Arsenal  Julai, 22, huko Los Angeles kisha watasafiri San Francisco kuvaana na Barcelona Julai 28, kwenye dimba la Levi’s.

 Mechi yao ya mwisho itakuwa dhidi ya Melbourne City nchini Australia Agosti 05, Melbourne Rectangular Stadium.

Tottenham Hotspur imeamua kwenda Asia kwa ajili ya maandalizi ya msimu ambapo itacheza dhidi ya timu ya kombaini ya Ligi Kuu Korea Kusini Julai, 23, jijini Seoul, kwenye Uwanja wa Seoul World Cup kisha wataenda Tokyo, Japan kumenyana na Yokohama F. Marinos Julai, 27, kwenye Uwanja wa Ajinomoto.

Mechi yake ya mwisho itakuwa dhidi ya Bayern Munich Agosti 03 kwenye Uwanja wa Allianz.