Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ngapi huko? Mashabiki wataulizana

NGAPI Pict

Muktasari:

  • Chelsea itakabiliana na Paris Saint-Germain katika fainali ambayo imetabiriwa kuwa na mabao mengi, huku kila timu ikijaribu kutengeneza historia yake ya kibabe.

NEW JERSEY, MAREKANI: NGAPI huko? Bila shaka ni swali watakalokuwa wakiulizana mashabiki wa soka hiyo Jumapili, wakati kipute cha fainali ya Kombe la Dunia la Klabu litakapopigwa uwanjani MetLife, Marekani.

Chelsea itakabiliana na Paris Saint-Germain katika fainali ambayo imetabiriwa kuwa na mabao mengi, huku kila timu ikijaribu kutengeneza historia yake ya kibabe.

Chelsea iliichapa Fluminense kwenye nusu fainali, Jumanne iliyopita, shukrani kwa mabao mawili ya staa wao mpya, Joao Pedro, wakati PSG iliifundisha mpira Real Madrid, Jumatano iliyopita na kukamatia tiketi yao ya kucheza fainali hiyo ya wikiendi hii kwa idadi ya mabao 4-0.

Chama la Enzo Maresca, Chelsea litapambana kufukuzia rekodi ya kuwa timu ya kwanza ya England kubeba ubingwa wa dunia mara mbili, baada ya kufanya hivyo mwaka 2021 ilipoichapa Palmeiras.

PSG, kwa upande wao huu utakuwa ubingwa wa kwanza, licha kwenye kikosi chao kutakuw ana watu watakaokuwa wameboresha zaidi rekodi zao za ubingwa wa taji hilo, akiwamo Kocha Luis Enrique. Na ushindi wa Chelsea, ambao walichapwa 2012, utawafanya kuingia kwenye chungu kimoa na timu zilizowahi kubeba mara mbili; Bayern Munich (2x: 2013 na 2020), Corinthians (2x: 2000 na 2012), Barcelona (3x: 2009, 2011 na 2015) na Real Madrid (5x). Lakini, kama Chelsea itapoteza, basi itakuwa timu ya kwanza kuchapwa mara mbili kwenye fainali ya michuano ya dunia.

Kocha Maresca atakuwa na wakati mgumu kwenye uteuzi wa kikosi chake hiyo Jumapili, kwa sababu Liam Delap na Levi Colwill wote watakuwa tayari kucheza baada ya kukosa mechi ya nusu fainali. Kabla ya kukosa mechi ya Fluminense, Delap alikuwa akianza katika kila mechi kuanzia mechi ya pili, alipombadili Nicolas Jackson, aliyeonyeshwa kadi nyekundu dhidi ya Flamengo.

Joao Pedro naye aling'ara kwenye mechi ya nusu fainali, akiingia kwa sababu Delap hakuwapo, hivyo jambo hilo sasa linamfanya Maresca kuwa njiapanda, aanze na nani. Kwenye safu ya ulinzi pia, Colwill, aliyeanzishwa kwenye mechi nne kati ya tano, yupo tayari kwa mechi hiyo na kufanya eneo hilo la ulinzi pia kumpasua kichwa Maresca, aanze na mchezaji gani.

Kiungo Moises Caicedo alikimbizana na muda baada ya kuumia enka, lakini kwenye fainali hiyo, Maresca anaweza kuanza naye ili kuwawekea ubishi viungo wa PSG, ambao ni wasumbufu sana.

PSG itaendelea kukosa huduma ya Willian Pacho na Lucas Hernandez kutokana na kutumikia adhabu. Lakini, Ousmane Dembele ana nafasi kubwa ya kuanza baada ya kuonekana kupona vyema majeraha yake, huku Bradley Barcola anatazamiwa kuanzia benchi, wakati Khvicha Kvaratskhelia atakuwa kushoto na Desire Doue kulia.

Kinyume cha hapo, PSG itakuwa na kikosi chake kilekile matata, viungo Joao Neves, Vitinha na  Fabian Ruiz, wanatazamiwa kuendeleza balaa lao, wakati beki wa kulia yupo Achraf Hakimi, kati yupo Marquinhos na kushoto Nuno Mendes, huku golini ataendelea kipa ngongoti Gianluigi Donnarumma.

Rekodi zinaonyesha, Chelsea na PSG hazijawahi kukutana tangu 2016, wakati timu hizo zilipokutana kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Les Parisiens ilishinda mechi zote mbili 2-1 huku ikiwamo kuitupa nje Chelsea kwa faida ya bao la ugenini msimu mmoja uliotangulia. Kwa jumla, Chelsea imewahi kushinda mara mbili dhidi ya PSG, wakati wababe hao wanaonolewa na Luis Enrique yenyewe wameshinda mara tatu, huku mechi tatu zikimalizika kwa sare.