Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mngqithi ashusha sheria kuu tano Yanga

YANGA Pict


YANGA kazi imeanza na watu wa kuwauliza hilo ni wachezaji wa kikosi hicho watakwambia kwamba yule kocha Manqoba Mngqithi amekuja kikazi zaidi, akianza na mambo matano.


Yanga imeanza maandalizi yake kuelekea msimu mpya ambao utakuwa wa kwanza kwa Mngqithi na kocha huyo kabla ya kuanza kazi hiyo juzi akawapa angalizo mapema wachezaji wake juu ya mambo anayotaka.

KOCH 01

NIDHAMU

Kocha Mngqithi amewaambia wachezaji kwamba, hakuna mchezaji aliyefanikiwa duniani kama hana nidhamu ya maisha yake kwenye kila kitu.

Kocha amewataka wachezaji kujiheshimu, kuheshimu muda, kuiheshimu klabu na nidhamu ya uwanjani kama wakifanya hivyo maisha yao yatakuwa na mafanikio makubwa na kwamba hawezi kufanya kazi na mchezaji ambaye hatakuwa mfano wa nidhamu bora.

Anayeanza na anayetoka kwenye kikosi chake hakuna staa mkubwa, kila mchezaji ana nafasi ya kucheza, ambapo Msauzi huyo amewaambia wachezaji kwamba anayetaka nafasi basi ashindane mazoezi na acheze mechi kwa akili kubwa.

"Kocha anataka mchezaji anayeanza au yule atakayeingia, kusiwe na tofauti ili timu icheze kwa kiwango bora, anasema atakachofanya mazoezi atakayotupa yatatusaidia kushindana uwanjani ili tuwe sawa," amesema staa mmoja wa Yanga anayecheza nafasi ya beki.


HACHAGUI

Jambo lingine ambalo Mngqithi amewaambia wachezaji wake ni kwamba haangalii urefu wala umbo la mwili, anachotaka ni kiwango bora kwa wachezaji wake.

"Kaka kocha kashanyoosha, hata sisi ambao hatuna mwili mkubwa nafasi tunayo jukumu letu ni kujituma tu uwanjani hana lingine, yaani kauli hii imenipa moyo sana nadhani ni kocha wa tofauti kabisa na wengine sasa nitapambana, mkubwa Mungu," amesema mchezaji mwingine ambaye hakuwa anapata nafasi msimu uliopita.

KOCH 02

HAPANGIWI

Mngqithi amewaambia wachezaji wake mapema yeye sio kocha wa kupangiwa mambo na mtu mwingine, ambapo kila kitu kuhusu ufundi kitaamuliwa na yeye mwenyewe akishirikiana na wasaidizi wake.

"Tena ameongeza kuwa yeye ndio kocha mkuu, anakubali kushauriwa lakini yeye sio kocha wa kupangiwa kitu, anasema Kila kitu kitaamuliwa na benchi lake kuhusu ufundi uwanjani akishirikiana na wasaidizi wake."


TIMIZA WAJIBU WAKO

Kocha huyo amewataka wachezaji wake kutimiza majukumu yao uwanjani kwa kuipigania klabu na mengine kuhusu maslahi na mahitaji ya wachezaji wamuachie yeye atayasimamia kwenda sawa.

KOCH 03

MAZOEZI SAA TATU

Kwenye mazoezi ya kwanza juzi na yale ya jana, Mngqithi amewapa dozi nzito wachezaji wake akitumia takribani saa tatu kwa mazoezi tofauti ya kuimarisha mwili.

Hata hivyo, kocha huyo aliwashtua wachezaji 14 ambao walianza mazoezi wakiwa hoi akisema alikuwa anatamani mazoezi hayo yatumie saa nne, hatua ambayo iliwafanya wachezaji waduwae kwa mshangao.

Baada ya kumaliza mazoezi hayo ambayo yalifanyika viwanja vya Gymkhana, kila mchezaji aliingia kwenye gari lake na kuondoka haraka hakukuwa na stori wala kuagana kama ambavyo imezoeleka huko nyuma.

"Daah jamaa ameanza na gia ya juu sana hii ni hatari," alisikika mchezaji mmoja akisema baada ya mazoezi hayo.