Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Neymar, Thiago waendeleza bifu la miaka sita

NEYMAR Pict

Muktasari:

  • Neymar (34), alirejea uwanjani Jumapili katika Ligi Kuu ya Brazil baada ya kuamua kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Brazil baada ya Kombe la Dunia.

SAO PAULO, BRAZIL: MSHAMBULIAJI wa Santos, Neymar ameendeleza mvutano wake wa muda mrefu na kiungo Thiago Mendes baada ya mchezaji huyo kukataa kumpa mkono nyota huyo wa Brazil kabla ya mchezo wa Ligi Kuu ya Brazil.

Neymar (34), alirejea uwanjani Jumapili katika Ligi Kuu ya Brazil baada ya kuamua kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Brazil baada ya Kombe la Dunia.

Mshambuliaji huyo alikuwa nahodha wa Santos katika mchezo dhidi ya Vasco uliochezwa Uwanja wa Sao Januario, lakini kabla ya mchezo kuanza, mvutano wa miaka sita kati yake na Mendes, 34, uliibuka tena.

Katika kusalimiana kabla ya mchezo, Neymar aliwasalimia wachezaji wenzake na wapinzani, lakini Mendes alikataa kabisa kumpa mkono.

Neymar alionekana kutabasamu kwa hali ya kulazimisha kabla ya kuendelea na zoezi hilo na kwenda kuwasalimia waamuzi.


NEY 01

Chanzo cha ugomvi

Uhasama kati ya mastaa hao wawili ulianza mwaka 2020 wakati Neymar alipokuwa akiichezea Paris Saint-Germain ya Ufaransa.

Mendes, ambaye wakati huo alikuwa Lyon, alimchezea faulo mbaya Neymar katika mchezo wa Ligue 1, kitendo kilichomsababisha nyota huyo kuondoka uwanjani akiwa kwenye machela huku akilia kwa maumivu.

Baada ya VAR kuingilia kati, Mendes alionyeshwa kadi nyekundu na baadaye alifungiwa mechi tatu.

NEY 03

Neymar alifanyiwa vipimo na kubainika kuwa amepata majeraha ya kifundo cha mguu, hali iliyomuweka nje ya uwanja kwa takribani mwezi mmoja.

Baada ya tukio hilo, baba yake Neymar, Neymar Santos Sr, alitumia mitandao ya kijamii kumshambulia Mendes, huku kiungo huyo baadaye akiomba msamaha.

Mendes pia alidai kuwa yeye pamoja na familia yake walipokea vitisho na matusi kufuatia tukio hilo.


NEY 02

Ugomvi waibuka tena

Baada ya miaka sita, uhasama huo uliibuka tena Februari mwaka huu katika mchezo ambao Santos iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Vasco kwenye Uwanja wa Vila Belmiro.

Neymar alikasirika baada ya kufanyiwa faulo na kumfuata Mendes katika kipindi cha kwanza, kabla ya wawili hao kuanza kubishana.

Muda mfupi baadaye, Mendes alimgusa usoni Neymar, ambaye akaanguka chini na kuzua mzozo zaidi.

Waamuzi waliwaonyesha wote kadi za njano, lakini mabishano yao yaliendelea katika mchezo huo uliokuwa na presha kubwa.

Neymar pia alirejea kwenye tukio la mwaka 2020, akimkumbusha Mendes faulo iliyomsababishia jeraha nchini Ufaransa.

“Kila mara anataka kuanzisha vurugu, kila mara anataka kujifanya mkali. Kwa heshima zote, ni mjinga. Alishawahi kuniumiza nilipokuwa PSG, leo amenitishia tena, hivyo tuone kama ana ujasiri wa kuniumiza tena,” Neymar amesema.

Hata hivyo, safari hii Neymar ndiye aliyeondoka na tabasamu, baada ya kuiongoza Santos kuichapa Vasco mabao 3-0, katika ushindi uliompa nafasi ya kumaliza kwa staili nyingine pambano lake na Mendes.