Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Apumzike kwa amani baba mzaa chema, Jorge Messi

PAZIA Pict


ALIZALIWA Rosario amelazwa Rosario. Jorge Messi. Baba yake Lionel Messi. Tunaweza kumuita ‘Baba mzaa chema’. Alituletea mmoja kati ya wachezaji bora kuwahi kutokea katika uso wa dunia. Subiri kwanza. Kuna lugha ambayo sisi wengine tunaweza kutumia.


Sisi wengine tunaweza kusema kwamba aliwahi kutuletea mchezaji bora zaidi kuwahi kucheza mchezo wa mpira wa miguu duniani. Hatutaenda mbali kwa sababu utatokea ubishi mwingine. Kuna ambao watasema kuhusu Pele, Diego Maradona, Johan Cruffy na wengineo. Wengine huwa tunaamini kwamba Lionel ndiye mchezaji bora kuwahi kutokea katika uso wa ulimwengu.


Achan ana Lionel. Alikuwa akimzika baba yake Jorge mapema wiki hii pale Rosario. Tunamzungumzia Jorge ambaye amelala katika makaburi ya El Prado pale Rosario. Sio kitu cha kawaida sana kwa baba wa kizungu au baba wa Kiafrika kusimamia maendeleo ya mtoto wake. Jorge alifanya hivyo.

Huku Afrika ni kama kule Amerika Kusini. Kuna Watoto wengi wa kiume au wa kike ambao wamelelewa na mama mmoja. Kisa? Baba aliacha mimba au alikimbia majukumu kwa sababu kadhaa. Ni kitu cha kawaida tu.

PAZ 01
PAZ 03

Tuna simulizi hizi kwa mastaa wengi wakubwa kutoka fani mbalimbali. Lakini kuna simulizi chache pia ambazo baba alisimama imara kando ya mama kufanya kila awezalo ili mtoto asimame. Haijalishi kama mtoto atakuwa staa au atakuwa mtu wa kawaida tu.

Hapa ndipo Jorge alipochukua majukumu yake. Na hakuyachukua kwa wepesi. Katika Watoto wake wanne, Rodrigo, Mathias, Lionel na binti pekee Maria Sol, ni Lionel pekee ambaye alizaliwa na changamoto. Alizaliwa huku akiwa na tatizo la ukuaji.

Na ndiye mtoto pekee ambaye alizaliwa na kipaji kikubwa. Kipaji cha kucheza soka. Lionel ambaye katika Makala hii atatumika zaidi kwa jina la Lionel kuliko Messi kwa ajili ya kumtofautisha na mzee Messi, ndiye ambaye alisumbuliwa na ugonjwa mbaya utotoni.

Ni historia ambayo karibu kila mpenda soka anayo. Hata wasiopenda soka wanayo. Alizaliwa huku akiwa na tatizo la ukuaji. Klabu yake ya utotoni, Newell’s boy walishindwa kulipia matibabu yake. Gharama yake ilikuwa kubwa.

Barcelona walikuwa wameambiwa habari za kinda wa ajabu wa Rosario wakaamua kuhudumia gharama za ukuaji wake pale Ulaya ili wapate huduma zake kama mwanasoka katika siku za mbele. Jorge Messi akambeba mwanae Lionel pamoja na familia nzima kwenda Barcelona.

PAZ 02
PAZ 04

Baada ya kufika Barcelona unaweza kuanza kuandika majukumu mengine mazito ya Jorge Messi. Wanafamilia wengine walirudi nyumbani Argentina na kumuacha peke yake abaki na Lionel. Kumbuka kwamba Lionel alikuwa na umri wa miaka 13 tu. Mwaka 2000.

Mke wake, Celia María Cuccittini alilazimika pia kurudi nyumbani Argentina kuwalea Watoto wengine watatu. Rodrigo, Mathias na binti pekee ambaye pia ni mtoto wa mwisho, Maria Sol. Jorge Messi alibakia na Lionel Barcelona na kumlea mwenyewe. Sio kazi rahisi sana.

Kuanzia hapo alikuwa kila kitu kwa Lionel. Alimsimamia kwa kila kitu ndani na nje ya uwanja. Kumbuka kwamba Jorge Messi alikuwa kocha kule Argentina.

Ina maana kwamba kwa kuweka makazi Barcelona akiwa na Lionel alikuwa na majukumu ya kumlea kama baba, kama kocha, lakini pia kuangalia namna ambavyo biashara ingeweza kwenda wakati jina la Lionel likichomoza Catalunya.

PAZ 03

Na baada ya jina la Lionel kuchomoza Catalunya, yeye alibakia kuwa kila kitu. Baba, Meneja, wakala, na kila kitu. Lionel alikuwa amebadilisha kila kitu katika maisha ya familia.

Lakini usisahau kwamba Jorge alikuwa nyuma ya kila kitu baada ya kuachiwa Lionel akiwa kinda na kisha Celia kurudi nyumbani Argentina na Watoto. Mara ngapi tunasikia habari mbaya kuhusu akina baba? Huwa ni mara nyingi.

Utasikia stori chache nzuri kuhusu akina baba. Labda ni kama vile Neymar ambaye amelelewa na baba na mama. Hata huku Afrika kuna habari chache nzuri kuhusu matunzo ya baba kwa mtoto.

Hapa ndipo ambapo Jorge anasimama na kuibuka shujaa. Juzi Lionel ametoa waraka wa kumkumbuka baba yake na kisha akaishia kujiuliza kama anaweza kuendelea kuch eza tena soka baada ya baba yake kuondoka duniani.

PAZ 04

Lionel anasema kwamba hakuwahi kujishughulisha na kitu chochote katika maisha yake zaidi ya kucheza soka. Kisa? Baba yake alikuwa anasimamia kila kitu kuhusu yeye.

Ndio, tangu wakati ule alipotua Hispania akiwa na umri wa miaka 13 kitu alichokifahamu yeye ni kucheza soka tu. Vinginevyo alikuwa anaangalia akaunti zake za benki zilikuwa zimeingiza kiasi gani.

Vinginevyo pia alikuwa anajua kwamba anatakiwa kwenda katika majukumu gani ya nje ya uwanja katika masuala ya mikataba ya kibiashara nje ya uwanja.

Yote hayo yalikuwa yanatimizwa na Jorge na washauri wengine. Yeye kazi yake ilikuwa ni kucheza mpira tu. Haishangazi kuona anajiuliza anawezaje kuendelea kucheza mpira bila ya marehemu baba yake.

Unapozingatia kwamba umri wake wa mpira unakaribia kwisha unaweza kukubali kitu ambacho Lionel anakifikiria. Angekuwa na miaka 24 tungemkatalia. Kwa umri alionao tutakubali maamuzi yake.

Yeye na baba yake wametoka mbali. Katika pambano la kombe la dunia dhidi ya Algeria alijikuta analia baada ya kufunga bao kwa sababu alikumbuka kuwa mtu aliyemlea na kumpambania ndani na nje ya uwanja alikuwa akipambana na maradhi wakati yeye akiipambania jezi ya Argentina.

Apumzike kwa amani Jorge Messi. Ni simanzi lakini sidhani kama ameondoka duniani huku akiwa anamdai Lionel kitu chochote kile. Tangu wakati ule alipompeleka Catalunya akiwa na miaka 13 mpaka anapoondoka duniani Lionel ameshinda kila kitu.

Hakuna kitu ambacho Lionel hajashinda. Kuanzia tuzo nyingi binafsi hasa ile ya mwanasoma bora wa dunia, kisha tuzo nyinginezo za ubingwa wa kombe la dunia na mazagazaga mengine, Lionel ameshinda kila kitu. Sio tu kwamba Jorge Messi hamdai Lionel, bali dunia haimdai Lionel Messi.

Jorge Messi anabakia miongoni mwa mifano ya mwanaume aliyeipambania familia yake. Aliyempambania kijana wake mwenye kipaji kikubwa, tena aliyeathirika na maradhi aje kubwa mtu mkubwa duniani. Apumzike kwa amani katika makaburi ya El Padro pale Rosario.