Newcastle, Bayern Munich jino kwa jino kwa Jackson
Muktasari:
- Chelsea inahitaji takribani Pauni 48 milioni ili kumuuza Jackson katika dirisha hili la usajili huko Ulaya ambaye alifunga mabao 14 katika mechi 44 msimu uliopita.
BAYERN Munich imeingia katika vita dhidi ya Newcastle United kumuwinda mshambuliaji wa Chelsea na timu ya taifa ya Senegal, Nicolas Jackson, mwenye umri wa miaka 24.
Chelsea inahitaji takribani Pauni 48 milioni ili kumuuza Jackson katika dirisha hili la usajili huko Ulaya ambaye alifunga mabao 14 katika mechi 44 msimu uliopita.
Mkataba wa staa huyo aliyejiunga na Chelsea 2023, unamalizika Juni 2031.
Newcastle imehamia kwake baada ya kupigwa bao na Man United katika harakati za kuwania saini ya Benjamin Sesko.
Hata hivyo, katika dili hilo pia inaonekana kuwa na nafasi ndogo ya kumpata kutokana na ofa ambayo Bayern inadaiwa kuweka mezani.
Licha ya mchango wake katika msimu uliopita, Chelsea na Jackson mwenyewe wamefikia makubaliano ya kuachana ikielezwa mchezaji anataka kutafuta changamoto mpya.
Bayern inataka kuboresha eneo la ushambuliaji ambalo limeondokewa na mchezaji tegemeo, Thomas Muller aliyetimkia Marekani.
Upande wake Newcastle inapambana kutafuta mshambuliaji ili akawe mbadala wa Alexander Isak ambaye ameshawaambia mabosi wa timu hiyo kuwa anataka kuondoka na kutua Liverpool katika dirisha hili.
Kabla ya kumpata Sesko, Man United pia ilimuweka Jackson katika mipango yake kama mbadala ikiwa mambo yangefeli.
Uwezekano wa Jackson kuondoka Chelsea pia unachagizwa na timu hiyo kusajili wachezaji wengi wenye uwezo wa kucheza nafasi yake.
Milan van Ewijk
COVENTRY City inataka Pauni 15 milioni ili kumuuza beki wa kulia Mholanzi Milan van Ewijk, 24. Timu mbalimbali za England ikiwemo Wolves na Wolfsburg zimeonyesha nia ya kumsajili. Van Ewijk alikuwa na msimu bora uliopita akiwa Coventry katika Championship. Alijiunga na timu hiyo akitokea Heerenveen. Mchezaji huyo ana kasi na uwezo mkubwa wa kupandisha mashambulizi. Mkataba wake na Coventry unamalizika Juni 2027.
Marc Guehi
NEWCASTLE United inajiandaa kuwasilisha ofa Crystal Palace ya Pauni 45 milioni kwa ajili ya kumnunua beki wa kati wa klabu hiyo na timu ya taifa ya England, Marc Guehi. Hata hivyo, Palace inahitaji kiasi kisichopungua Pauni 50 milioni ili kumuuza Guehi mwenye umri wa miaka 25 ambaye ameonyesha ubora tangu ajiunge na Palace akitokea Chelsea 2021 na tayari amecheza mechi zaidi ya 100.
Marc Casado
TOTTENHAM Hotspur imekubali kulipa Euro 30 milioni Barcelona ili kuipata saini ya kiungo raia wa Hispania, Marc Casado, 21, katika dirisha hili. Casado ambaye kwa sasa ni nahodha wa kikosi cha pili cha Barcelona na tayari ameanza kuingia katika mipango ya timu ya wakubwa. Spurs inamtazama kama mbadala wa muda mrefu wa Pierre-Emile Hijbjerg anayetajwa kuwa ataondoka mwisho wa msimu ujao.
Ross Barkley
KOCHA wa Everton, David Moyes, anapanga kusajili wachezaji wapya wasiopungua sita ili kuimarisha kikosi chake na miongoni mwa wachezaji wao wawili watakuwa viungo wa kati na wawili mawinga. Everton iliepuka kushuka daraja kwa shida msimu uliopita na sasa inataka kujenga kikosi thabiti kitakachoweza kupambana kumaliza nafasi za juu zaidi. Hadi sasa imemsajili kwa mkopo Ross Barkley.
Jadon Sancho
MABOSI wa Juventus wametuma wawakilishi Manchester kwa ajili ya mazungumzo na Man United juu ya winga wa timu hiyo na England, Jadon Sancho,25, ili kumsajili katika dirisha hili. Juventus inataka kumsajili Sancho baada ya kumuuza mshambuliaji wa kimataifa wa Marekani, Timothy Weah, 25. Benchi la ufundi la Juventus linadawa kumuona Sancho kuwa mbadala sahihi wa Weah.
Renato Veiga
ATLETICO Madrid inataka kutoa Pauni 30 milioni ili kumsajili beki wa kati wa Chelsea, Renato Veiga ,21, katika dirisha hili. Chelsea ipo tayari kumuuza staa huyo wa kimataifa wa Ureno, lakini inahitaji takribani Pauni 35 milioni. Atletico haipo tayari kutoa kiasi hicho cha pesa na badala yake inafanya mazungumzo ili kupunguziwa
Alejandro Garnacho
CHELSEA inatajwa kuwa katika hatua nzuri ya mazungumzo na Manchester United juu ya uwezekano wa kumpata winga Alejandro Garnacho licha ya Aston Villa kumtaka pia. Inaaminika kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina anaweza kupatikana kwa Pauni 40 milioni. Garnacho ni miongoni mwa wachezaji ambao kocha wa Man United, Ruben Amorim amewaruhusu kuondoka.