Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Muller akutwa na corona, kuikosa fainali Qatar leo

New Content Item (1)
Mueller akutwa na corona, kuikosa fainali Qatar leo

Muktasari:

  • Mshambuliaji wa Bayern Munich, Thomas Muller anatarajiwa kuikosa mechi ya fainali ya Klabu Bingwa ya Dunia jijini Doha leo baada ya kukutwa na virusi vya corona, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Ujerumani.

Berlin, Ujerumani (AFP). Mshambuliaji wa Bayern Munich, Thomas Muller anatarajiwa kuikosa mechi ya fainali ya Klabu Bingwa ya Dunia jijini Doha leo baada ya kukutwa na virusi vya corona, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Ujerumani.

Televisheni ya Sky Sports nchini Ujerumani na gazeti la Bild, Muller, aliyekuwemo katika kikosi cha Ujerumani kilichotwaa Kombe la Dunia alikutwa na maambukizi hayo wakati alipopimwa baada ya mazoezi jana Jumatano.

Kukutwa na maambukizi kunamfanya mshambuliaji huyo asiruhusiwe kucheza fainali leo dhidi ya mabingwa wa Concacaf, Tigres katika mji huo mkuu wa Qatar ambako vigogo hao wa soka Ujerumani wanawania kuandika historia ya kutwaa mataji sita ndani ya miezi 12.

Si Bayern wala Fifa waliothibitisha taarifa hizo.