Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtihani mwingine kwa Manchester City EPL

LAMPARD Pict

Muktasari:

  • Katika mchezo wake uliopita, Manchester City ilifanya kweli baada ya kuichapa Crystal Palace mabao 4-1, hivyo kuendeleza mwanzo mzuri wa msimu tofauti na jinsi ambavyo mashabiki wa soka walikuwa wanatarajia kutokana na mabadiliko ya benchi la ufundi kwenye timu hiyo.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER City itakuwa mwenyeji wa Coventry City leo Jumamosi katika Uwanja wa Etihad, mchezo wa raundi ya tatu wa Ligi Kuu England msimu wa 2026/27, mechi ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka duniani.

City inaingia kwenye mchezo huo ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na pointi sita baada ya kushinda michezo yake miwili ya mwanzo.

Katika mchezo wake uliopita, Manchester City ilifanya kweli baada ya kuichapa Crystal Palace mabao 4-1, hivyo kuendeleza mwanzo mzuri wa msimu tofauti na jinsi ambavyo mashabiki wa soka walikuwa wanatarajia kutokana na mabadiliko ya benchi la ufundi kwenye timu hiyo.

Kwa upande wa Coventry City, mambo yamekuwa magumu baada ya timu hiyo kushindwa kupata pointi katika michezo yake ya mwanzo na sasa inashika nafasi ya 17 kwenye msimamo na kuonyesha kuwa wanatakiwa kufanya kazi kubwa ili kupata pointi kwenye mchezo huu .

Coventry ilipoteza mchezo wake uliopita kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Hull City, hivyo itakuwa na kibarua kizito mbele ya City yenye rekodi nzuri katika mwanzo wa msimu.

Mchezo wa mwisho kuzikutanisha timu hizo ulimalizika kwa Manchester City kushinda 4-2.


LAMP 01

LAMPARD VS MAN CITY

Kocha wa Coventry, Frank Lampard, amewahi kukutana na Manchester City mara sita, akishinda mchezo mmoja, kutoka sare moja na kupoteza minne.

Kwa upande mwingine, kocha wa Manchester City, Enzo Maresca, amewahi kuikabili Coventry City mara mbili, akishinda mmoja na kupoteza mmoja.


LAMP 02

REKODI ZAVUTIA

Coventry City imekuwa ikiruhusu mabao katika michezo mitatu mfululizo, huku Manchester City nayo ikiwa imeruhusu mabao katika mechi tatu mfululizo hivyo kwa mashabiki ni mchezo ambao unatarajiwa kuwa na mabao mengi.

Hata hivyo, City iko kwenye kiwango kizuri zaidi kwa sasa, ikiwa haijapoteza katika michezo miwili mfululizo na pia imeshinda mechi zake mbili za mwisho.


LAMP 03

HISTORIA TIMU

Manchester City na Coventry City zimekutana mara 73 katika mashindano mbalimbali, huku City ikiwa na rekodi bora kwa kushinda michezo 34 dhidi ya 21 za Coventry.

Katika Uwanja wa Etihad, Manchester City imekuwa na ubabe zaidi, ikishinda michezo 26 kati ya 38 iliyocheza dhidi ya Coventry. Coventry yenyewe imeshinda mara saba.

Kwa upande wa Ligi ya England, timu hizo zimekutana mara 52, ambapo Manchester City imeshinda michezo 24, zimetoka sare mara 12, huku Coventry ikishinda mara 16.

Hivyo, macho yote yatakuwa Etihad leo kuona kama Manchester City itaendelea na mwanzo wake wa kuvutia wa msimu au Coventry itashtua wenyeji na kuondoka na pointi.


MECHI NYINGINE ZA LEO PREMIER

Newcastle vs Bournemouth

Nottigham Forest vs Spurs

Brentford vs Sunderland

Brighton vs Leeds

Hull vs Aston Villa

Fulham vs Palace