Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal, Man city waziteka tuzo PFA

Muktasari:

  • Kikosi hicho kilitangazwa Jumanne usiku katika hafla iliyofanyika Manchester Opera House, ambapo wachezaji wenyewe ndio waliopiga kura kuwachagua wenzao waliofanya vizuri zaidi msimu uliopita.

MANCHESTER, England. ARSENAL na Manchester City wametawala kikosi bora cha msimu cha Ligi Kuu England kilichochaguliwa na Chama cha Wanasoka Kitaalamu England (PFA), huku wachezaji tisa kati ya 11 wakitokea katika klabu hizo mbili.

Kikosi hicho kilitangazwa Jumanne usiku katika hafla iliyofanyika Manchester Opera House, ambapo wachezaji wenyewe ndio waliopiga kura kuwachagua wenzao waliofanya vizuri zaidi msimu uliopita.

Arsenal waliotwaa ubingwa wa Ligi Kuu, wameingiza wachezaji watano kwenye kikosi hicho, huku Manchester City ikiwa na wawakilishi wanne.

Kipa David Raya ameingia kwenye kikosi baada ya kupata tuzo ya kipa bora 'Golden Glove' kufuatia kuweka rekodi ya kutoruhusu bao katika mechi 19 za ligi msimu uliopita.

Mbele yake wamechaguliwa mabeki watatu kati ya wanne waliokuwa sehemu ya kikosi cha Arsenal kilichotwaa ubingwa, Jurrien Timber akijiunga na mabeki wa kati Gabriel Magalhaes na William Saliba.

Beki wa Manchester City, Nico O’Reilly, anakamilisha safu hiyo akichaguliwa katika nafasi ya beki wa kushoto.

Kwenye kiungo, Arsenal imetajwa kupitia Declan Rice, huku Manchester City ikiwakilishwa na Rayan Cherki. Wawili hao wameungana na nahodha wa Manchester United, Bruno Fernandes.

Fernandes aliweka rekodi mpya ya kutoa pasi za mwisho 21 katika msimu mmoja wa Ligi Kuu England, jambo lililomfanya atwae tuzo ya Mchezaji Bora wa Msimu wa Ligi Kuu pamoja na tuzo ya Chama cha Waandishi wa Soka England (FWA).

Sasa amekamilisha mafanikio hayo kwa kutwaa pia tuzo ya PFA ya mchezaji bora.

Hakuna mshambuliaji wa Arsenal aliyeingia kwenye safu ya mbele ya kikosi hicho. Badala yake, nafasi zote tatu zimechukuliwa na wafungaji bora watatu wa msimu uliopita.

Erling Haaland wa Manchester City, aliyefunga mabao 27, anaongoza safu hiyo, akifuatiwa na Igor Thiago wa Brentford mwenye mabao 22 na Antoine Semenyo aliyefunga 17 akiwa Bournemouth kabla ya kuhamia Manchester City katikati ya msimu.


CHAMPIONSHIP

Wachezaji sita kati ya 11 waliochaguliwa kwenye kikosi bora cha Championship walitoka Coventry City, ambao walipanda daraja chini ya kocha Frank Lampard.

Beki wa Southampton, Taylor Harwood-Bellis pamoja na kiungo Hayden Hackney ambaye alifanya vizuri Middlesbrough wamekamilisha kikosi hicho.