EPL iliyoacha mambo 10
Muktasari:
- Licha ya wasiwasi unaoikabili Manchester United, mchezaji mmoja ambaye hakuna anayemtilia shaka ni Senne Lammens. Kipa huyo alifanya sevu muhimu katika kipindi cha kwanza dhidi ya Ipswich, akiisaidia timu yake kubaki mchezoni katika mazingira magumu.
LONDON, ENGLAND; MWISHONI mwa wiki iliyopita kulikuwa na mechi kibao katika Ligi Kuu England, lakini kuna mambo 10 ambayo ni kama yaliacha mijadala mingi kutokana na namna timu zilivyoingia viwanjani katika michezo hiyo ya pili ya mashindano hayo. Twende pamoja!
1. LAMMERS UTULIVU OLD TRAFFORD
Licha ya wasiwasi unaoikabili Manchester United, mchezaji mmoja ambaye hakuna anayemtilia shaka ni Senne Lammens. Kipa huyo alifanya sevu muhimu katika kipindi cha kwanza dhidi ya Ipswich, akiisaidia timu yake kubaki mchezoni katika mazingira magumu.
Akiwa mtu mwenye utulivu, Mbelgiji huyo amekuwa akileta hali ya amani kikosini katika mazingira yenye hisia kali, hasa kutokana na safu ya ulinzi iliyoonekana kuwa na panda shuka.
Wakati Julio Enciso wa Ipswich alipopenya na kubaki katika nafasi nzuri ya kufunga, Lammens alilazimika kuamua wakati sahihi wa kutoka golini na umbali gani wa kufanya hivyo.
Alifanya hivyo kwa usahihi mkubwa, akitumia vizuri umbali na pembe ili kuhakikisha mshambuliaji huyo wa Paraguay anazuiwa. Usambazaji wake wa mipira pia ulikuwa bora, akianzisha mashambulizi ya haraka na kuleta kasi inayohitajika kutoka kwa makipa wa kisasa.
2. LIVERPOOL INADAIWA
Kocha wa Nottingham Forest, Oliver Glasner anasema atasherehekea kufungwa kwa dirisha la usajili kwa kunywa bia moja kesho, Jumatano usiku. Andoni Iraola, kocha wa Liverpool huenda naye akafanya hivyo.
Hilo linaonyesha jinsi mkakati wa hivi karibuni wa Liverpool katika usajili ulivyo wa kushangaza. Furaha inayoletwa na ujio unaotarajiwa wa Bradley Barcola kutoka PSG kwa ada ya Pauni 123 milioni inaambatana na wasiwasi kuhusu mapengo katika kikosi cha Iraola ambayo hayajajazwa.
Eneo la winga wa kulia, beki wa kulia na kiungo wa kati ndiyo upungufu ulio wazi zaidi. Haja ya kuimarisha maeneo yote matatu ilionekana wakati Liverpool ilipolazimika kupambana ili kupata sare ya mabao 2-2 katika dakika za mwisho, ikiwa ni mchezo wa pili mfululizo wa ligi waliomaliza kwa matokeo hayo.
“Hatufahamu kikosi kitakuwaje Septemba 2,” anasema Iraola, huku akitarajia kwamba mawinga siyo wachezaji pekee watakaosajiliwa kabla ya leo usiku Jumanne. “Naona uchambuzi wowote ninaoweza kufanya utakuwa pale nitakapojua kila kitu kitakapokamilika, nitakapofahamu nani atakayekuwa hapa kwa msimu mzima au hadi Januari,” anasema kocha huyo.
3. ALONSO HANA PRESHA KUTAWALA GEMU
Chelsea waliweka kipaumbele katika kudhibiti mchezo chini ya Enzo Maresca, lakini chini ya Xabi Alonso wamekuwa wakitegemea zaidi mashambulizi ya kushtukiza.
Katika mechi mbili za kwanza za ligi chini ya kocha huyo Mhispaniola, Chelsea wamekuwa na umiliki mdogo wa mpira. Walikuwa na asilimia 38.1 ya umiliki katika ushindi wa wiki iliyopita dhidi ya Fulham na asilimia 25 walipoifunga Brighton, Jumapili.
Hata hivyo, Alonso anasisitiza kwamba huo siyo mkakati maalumu. “Unahitaji kuangalia muktadha wa takwimu,” anasema baada ya mchezo dhidi ya Brighton na kuongeza: “Baada ya dakika 30 tulikuwa tumefunga [na kuwa] 3-0. Pengine wakati huo tulianza kucheza sana tukizingatia matokeo badala ya kuendelea kucheza. Lakini huo siyo mtazamo wetu. Sisemi kwamba tunahitaji kuwa na asilimia 60 au 20 ya umiliki wa mpira.”
4. ARMSTRONG AFICHUA JAMBO EVERTON
Uamuzi wa kutomuuza Harrison Armstrong unaweza kutuliza hali ya sintofahamu ndani ya Everton kwa sasa, lakini huenda usidumu kwa muda mrefu. Makundi tofauti tayari yanaonekana. Kocha David Moyes amekuwa akijitetea tangu mkurugenzi mtendaji Angus Kinnear aliposema kwamba wamiliki wa Friedkin waliona msimu uliopita kama ‘kushindwa’.
Moyes alijiunga na mashabiki waliokuwa Bournemouth waliotishia kufanya maandamano iwapo Armstrong angeuzwa kwenda Nottingham Forest. Kumuuza mtoto huyo wa nyumbani kwa lengo la kupata “faida’ kulionekana kuwa jambo lisilokubalika.
5. JAISSLE AANZA KUIJENGA NEWCASTLE
Kocha Matthias Jaissle alicheka alipoulizwa kama anahisi ana wajibu wa kuwaendeleza wachezaji waliosajiliwa na klabu kabla hajafika.
“Kazi ya kocha ni kupata kilicho bora zaidi kutoka kwa wachezaji wako,” alijibu kocha huyo wa Newcastle. Wakati maandalizi ya mchezo wa Jumamosi iliyopita yalitawaliwa na mjadala kuhusu matumizi makubwa ya fedha katika usajili wa majira ya kiangazi na vikosi vilivyokuwa katika kipindi cha mabadiliko, Jaissle aliipata ushindi dhidi ya Spurs kupitia uchezaji mpya wa wachezaji ambao walikuwa wameonekana kutokuwa na nafasi baada ya misimu mibaya.
Yoane Wissa aliongoza safu ya ushambuliaji, huku Anthony Elanga akitumia nafasi yake kwa utulivu na kufungua ukurasa wa mabao. Joe Willock pia alionyesha kiwango bora, huku Nick Woltemade, ambaye amekuwa akikosolewa akitoa asisti.
Wachezaji wapya pia walivutia hasa Nico Gonzalez na uwezo wake wa kupiga pasi za aina mbalimbali ilhali bado kukiwa na wengine wanaohitaji kuzoea timu.
Lakini, Jaissle ameonyesha kwamba anaweza kujenga timu kwa kutumia wachezaji alionao, jambo linalofanya ushindi kuwa mtamu zaidi. Inashangaza pia kuona kwamba mashabiki wa Newcastle, maarufu kama Toon Army, tayari wameonekana kumkubali sana kocha wao Mjerumani.
6. HULL WANAVYOTUMIA NGUVU
Mechi mbili, ushindi mara mbili, mabao mawili bila kufungwa; siri ya mafanikio ya Hull City ni ipi? Wana kikosi chenye mchanganyiko wa aina mbalimbali ya wachezaji, na kocha Sergej Jakirovic hadi jana alikuwa anataka kuongeza angalau beki mmoja wa kulia na kipa mwingine kabla ya dirisha la usajili kufungwa kesho, Jumanne.
Jakirovic anasema kichwa chake kilikuwa hoi kutokana na shughuli nyingi za dirisha la usajili, huku akitania kwamba mkataba wake mpya wa miaka mitatu haujasainiwa kwa sababu wino katika ofisi yake umekwisha kutokana na usajili wa wachezaji 13 katika majira haya ya kiangazi.
Katika mchezo dhidi ya Coventry Jumamosi, Hull walipiga mashuti machache kuliko timu ya Frank Lampard na waligusa mpira mara chache zaidi ndani ya eneo la hatari la wapinzani. Pia walipiga pasi 182 dhidi ya 501 za wapinzani wao.
Bao la ushindi la Liam Millar lilitokana na shambulizi bora la kushtukiza, huku Hull wakicheza kwa kutumia nguvu zaidi.
“Tunapendelea kuiacha timu nyingine iwe na mpira na sisi kujilinda tu,” anasema mshambuliaji wa Hully City, Oli McBurnie. “Tumeona timu zikidhibiti mpira katika Championship, zinapokuja Ligi Kuu England zinajaribu kutumia mtindo huohuo na inakuwa ngumu sana. Siyo kila kitu ni kuonekana mzuri na kupiga pasi milioni moja.”
7. CRYSTAL PALACE MAMBO BADO
Crystal Palace wako katika hali ngumu. Hadi jana, Daniel Munoz alikuwa anaonekana kuwa tayari kujiunga na Nottingham Forest, Galatasaray walikuwa wanamtaka Ismaila Sarr na Jean-Philippe Mateta ni majeruhi.
Sarr na Mateta, ambao kwa pamoja walifunga sehemu kubwa ya mabao ya Palace msimu uliopita walikosekana katika kipigo dhidi ya Manchester City na kutokuwepo kwao kulionekana wazi katika safu ya ushambuliaji.
Eddie Nketiah alikosa nafasi kadhaa, huku Jorgen Strand Larsen akiwa hafanyi vizuri. Kocha Pierre Sage, ambaye amepoteza mechi zake mbili za kwanza tangu kuchukua nafasi ya Oliver Glasner, anahitaji kuongezewa wachezaji kabla ya dirisha la usajili kufungwa leo usiku.
Axel Disasi anatarajiwa kuleta tofauti baada ya kuingia kikosini katika safu ya ulinzi iliyodhoofishwa na kuondoka kwa Maxence Lacroix. Hata hivyo, mwanzo wa Cystal Palace umeleta wasiwasi.
8. UWEZO WA FARKE KUSOMA MCHEZO
Makocha wa Ligi Kuu England mara chache hupewa sifa wakati mambo yanapokwenda vizuri, lakini Jumapili mchana ilionekana kuwa wakati sahihi wa kumpa heshima anayostahili kocha wa Leeds, Daniel Farke, baada ya timu yake kuendelea na mwanzo wa msimu bila kupoteza.
Uamuzi wa Farke kurejea kutumia mfumo wa mabeki watano Novemba iliyopita dhidi ya Manchester City ulikuwa hatua muhimu katika msimu wa Leeds na katika kipindi chake cha uongozi.
Siyo kutia chumvi kusema kwamba Farke alikuwa chini ya presha kubwa wakati huo, lakini uwezo wake wa kubadilika kimfumo hatimaye uliokoa nafasi yake. Jumapili alionyesha tena uwezo huo wa kubadilisha mbinu.
Leeds walitawaliwa na Brentford katika kipindi cha kwanza kabla Farke hajabadilisha mfumo kutoka mabeki watano kwenda wanne. Matokeo yake yalikuwa uchezaji bora zaidi katika kipindi cha pili, bao la kusawazisha lililofungwa na Dominic Calvert-Lewin na pointi ambayo Leeds waliistahili.
Leeds ni timu yenye matarajio makubwa, ambayo yanaweza kuonekana tena kabla ya dirisha la usajili kufungwa kesho, Jumanne. Dalili za mwanzo zinaonyesha kwamba wana kocha anayeweza kwenda sambamba na matarajio hayo.
9. MUKIELE MTU SANA
Soka kama maisha limejaa mambo ya kushangaza. Kwa mfano, Sunderland iliwezaje kulipa Pauni 12 milioni pekee kumsajili Nordi Mukiele kutoka PSG msimu uliopita? Na kwa nini beki huyo wa kulia au beki wa kati mwenye umri wa miaka 28 aliyekuwa kwa mkopo Bayer Leverkusen msimu wa 2024-25 amecheza mechi moja tu kwa timu ya taifa ya Ufaransa?
Mukiele alicheza kama beki wa kati wakati Sunderland ikiifunga Fulham 1-0 kwenye Uwanja wa Stadium of Light, Jumapili, na alionyesha kiwango bora, akizuia mara mbili muhimu zilizosaidia kuzuia mabao.
Alvaro Arbeloa alionekana kukata tamaa baada ya vipigo viwili katika mechi zake mbili za kwanza kama kocha wa Ligi Kuu. “Nilivutiwa sana na Nordi na nilimwambia hivyo,” anasema Regis Le Bris, kocha wa Sunderland na kuongeza:
“Nordi ametuonyesha leo kwamba ni mchezaji mkubwa.” Mchezaji huyo bora wa mechi ya Jumapili anaonekana kuwa miongoni mwa usajili wa bei nafuu zaidi Ligi Kuu England katika miaka ya hivi karibuni.
10. DAVIS KIVUTIO
Kwa kuzingatia uhaba wa mabeki wa kushoto wa England, Leif Davis wa Ipswich amekuwa kwa muda mrefu nje ya macho ya makocha wa timu ya taifa. Akiwa amerudi Ligi Kuu England na kukabiliana na baadhi ya wapinzani bora zaidi duniani, beki huyo anaonekana kuwa mwenye uwezo mkubwa katika pande zote mbili za uwanja.
Ana uwezo mzuri wa kujilinda, akisimama vyema katika nafasi yake kwa umakini na kuwapa mawinga kazi ngumu, lakini pia anaweza kupanda mbele.
Alithibitisha hilo kwa kufunga bao la kwanza dhidi ya Manchester United Old Trafford, juzi, huku pia akionyesha uwezo mzuri wa kupiga pasi za aina mbalimbali, ndefu na fupi. Iwapo Thomas Tuchel, kocha wa timu ya taifa ya England atakabiliwa na uhaba wa machaguo katika msimu huu, Davis anaweza na anapaswa kuanza kuwa miongoni mwa wachezaji anaowafikiria zaidi ikiwa ataendelea na kiwango hiki.mguu wa kulia.