Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mpo? Man United inakuja mjue!

MAN Pict

Muktasari:

  • Lakini, Man United inaweza kupanda hadi nafasi ya pili katika msimamo wikiendi hii na hivi ndivyo itakavyokuwa.

LONDON, ENGLAND: MSIMAMO unasoma, Manchester United ipo kwenye nafasi ya sita, ikiwa imekusanya pointi 16 katika mechi tisa, ikishinda tano, sare moja na vichapo vitatu.

Lakini, Man United inaweza kupanda hadi nafasi ya pili katika msimamo wikiendi hii na hivi ndivyo itakavyokuwa.

Man United itakipiga na Nottingham Forest, Jumamosi, Novemba 1 na kama itashinda mechi hiyo, itapanda kwenye msimamo hadi nafasi ya pili, bila ya kujali matokeo ya Arsenal, kwa sababu tayari imeshaweka pengo la pointi sita dhidi ya Man United.

Ushindi wa Man United utawahakikishia kukamata nafasi hiyo ya pili, kwa sababu timu ambazo zinaweza kuishusha, hazitakuwa na mechi Jumamosi.

MA 01

Man United bado ina nafasi ya kubaki kwenye nafasi hiyo ya pili hata baada ya mechi za Jumapili na Manchester City itakipiga na Bournemouth inayoshika nafasi ya pili kwa sasa.

Mechi za Jumamosi ambazo hazitakuwa na madhara yoyote kwa Man United endapo kama itashinda mechi yake dhidi ya Forest, Brighton itakipiga na Leeds United, Burnley na Arsenal, Crystal Palace na Brentford na Fulham itakipiga na Wolves.

Spurs itakuwa na kibarua kigumu cha kuikabili Chelsea na hapo watamalizana wenyewe, huku Liverpool ikiwa na kasheshe mbele ya Aston Villa uwanjani Anfield, ikiwa ni mechi nyingine ya kumalizana wenyewe kwa wenye.

Jumapili, West Ham itakipiga na Newcastle, wakati Man City itashuka uwanjani Etihad kucheza na Bournemouth, mechi ambayo miamba hiyo itamalizana yenyewe kwenye vita ya kusaka nafasi za juu kwenye msimamo.

MA 02
MA 02

Sunderland, ambayo ipo nafasi ya nne kwa sasa, itasubiri Jumatatu, Novemba 3 itakapocheza na wagumu Everton na hivyo kuzidi kuiweka Man United kwenye matumaini ya kudumu kwa muda mrefu kwenye nafasi ya pili endapo kama itaichapa Forest.

MECHI ZIJAZO ZA MAN UNITED

-Novemba 1 vs Nottm Forest (ugenini)

-Novemba 8 vs Tottenham (ugenini)

-Novemba 24 vs Everton (nyumbani)

-Novemba 30 vs Crystal Palace (ugenini)

-Desemba 4 vs West Ham (nyumbani)

-Desemba 8 vs Wolves (ugenini)

-Desemba 15 vs Bournemouth (nyumbani)

-Desemba 21 vs Aston Villa (ugenini)

-Desemba 27 vs Newcastle (nyumbani)

-Desemba 30 vs Wolves (nyumbani)