Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ferdinand amshauri Kobbie Mainoo, amtaka kuiga mfano wa Casemiro

Ferdinand Pict
Ferdinand Pict

Muktasari:

  • Ferdinand amemtaka kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20 kuendelea kuwa na uvumilivu na kujituma kufanya kazi kwa bidii, kama alivyofanya Mbrazil huyo alipokutana na changamoto chini ya kocha Ruben Amorim.

Beki wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand, amemshauri kiungo Kobbie Mainoo kuiga mfano wa mchezaji mwenzake Casemiro wakati akipitia kipindi kigumu katika klabu hiyo. 

Ferdinand amemtaka kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20 kuendelea kuwa na uvumilivu na kujituma kufanya kazi kwa bidii, kama alivyofanya Mbrazil huyo alipokutana na changamoto chini ya kocha Ruben Amorim.

Akizungumza kwenye podcast yake Rio Ferdinand Presents, Ferdinand amegusia hali ya Mainoo na kumshauri kijana huyo kuiga mfano wa Casemiro.

Casemiro, ambaye aliwahi kutemwa na kocha msimu uliopita na kuhusishwa kuondoka Old Trafford majira ya kiangazi, aliendelea kuwa mvumilivu huku akifanya kazi kwa bidii hadi akafanikiwa kurejea kwenye kikosi cha kwanza.

FER 02

“Tazama na ujifunze. Kulikuwa na mchezaji aliyeambiwa hana kiwango cha kuchezea Manchester United, kwangu ninaifananisha hali hii kama anayoipitia Mainoo. Nafikiri kwa upande wa tabia na utu, kuna mengi ya kujifunza kutoka kwa Casemiro. Ndiyo, pia kwa upande wa kiufundi, lakini wachezaji hawa ni wa aina tofauti,” amesema Ferdinand.

“Ukiangalia Casemiro yuko kwenye kiwango kizuri na Bruno ndiye mchezaji wetu mwenye ubunifu mkubwa zaidi kwa sasa, itakuwa ngumu kwa Kobbie kupata nafasi ya kuanza,” ameongeza.

Mainoo amekuwa na wakati mgumu kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara msimu huu chini ya Amorim. Hadi sasa, amepata dakika 228 pekee katika mechi nane katika mashindano yote. Bado hajaanza mchezo wowote wa ligi, huku mechi pekee aliyoanza na kucheza dakika zote 90 ikiwa ni kwenye Kombe la Kombe la Ligi (Carabao Cup) dhidi ya Grimsby Town mwezi Agosti 2025.

Mainoo aliingia kama mchezaji wa akiba katika ushindi wa 4-2 ilioupata Man United dhidi ya Brighton & Hove Albion, akichukua nafasi ya Casemiro dakika ya 70. Hata hivyo, baada ya kuingia kwake, timu ilipoteza nguvu na kuruhusu mabao mawili.

FER 01

Mchezaji huyo aliyekuzwa na Manchester United, ambaye alivunja rekodi na kuingia timu ya wakubwa misimu mitatu iliyopita, amekuwa akionyesha kutoridhika na ukosefu wa muda wa kucheza. 

Imewahi kuripotiwa kuwa aliomba kuondoka kwa mkopo wakati wa dirisha la usajili la majira ya kiangazi, lakini ombi hilo lilikataliwa na klabu, na kumlazimisha kubaki, ili aendelee kuwania nafasi kwenye kikosi cha kwanza chini ya kocha Amorim.

Mainoo alipata nafasi yake ya kwanza kwenye kikosi cha wakubwa msimu wa 2022–23 chini ya aliyekuwa meneja Erik ten Hag, na tangu wakati huo ameshacheza mechi 80 akiwa na Manchester United, akifunga mabao 7 na kutoa asisti 3.