Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mourinho apendekeza jina la Rashford Fenerbahce

Muktasari:

  • Fenerbahce imekuwa ikijaribu kusuka kikosi kuelekea msimu ujao ili kuhakikisha inawapoka taji Galatasaray ambao ndio mabingwa watetezi.

KOCHA wa Fenerbahce ya Uturuki, Jose Mourinho anadaiwa kupendekeza jina la mshambuliaji wa Manchester United na timu ya taifa ya England, Marcus Rashford, 27, kwa mabosi wa timu yake na kusisitiza kwamba anahitaji asajiliwe katika dirisha hili.

Fenerbahce imekuwa ikijaribu kusuka kikosi kuelekea msimu ujao ili kuhakikisha inawapoka taji Galatasaray ambao ndio mabingwa watetezi.

Rashford ni miongoni mwa mastaa ambao Man United ipo tayari kuwauza katika dirisha hili baada ya kocha wa timu hiyo kusisitiza kuwa hahitaji kuwatumia kwa msimu ujao.

Hivi karibuni Barcelona ndio imekuwa ikitajwa sana kwamba huenda ikamsajili staa huyu ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2028 na yeye mwenyewe pia anaonekana kutamani zaidi dili hilo.

Hata hivyo, Barca haitaki kutoa kiasi cha pesa ambacho kinahitajika na Man United pia itahitajika akubali kupokea mshahara wa chini tofauti na ule ambao anaupokea sasa.

Mbali ya yote hayo, ili kumsajili kwanza wababe hao kutoka Nou Camp watatakiwa wauze kwanza baadhi ya wachezaji kutokana na kubanwa na sheria za matumizi ya fedha za La Liga. Msimu uliopita Rashford alionyesha kiwango bora akiwa na Aston Villa kwa mkopo aliyojiunga nayo kwa nusu msimu.


Ederson

GALATASARAY imewasilisha ofa ya Euro 3 milioni kwenda kwa Manchester City kwa ajili ya kuipata saini ya kipa wa klabu hiyo na timu ya taifa Brazil, Ederson mwenye umri wa miaka 31, katika dirisha hili.

Ederson ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2026, msimu uliopita alicheza mechi 40 za michuano yote na alitajwa kuwa karibu kuondoka katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana.


James Trafford

MANCHESTER City inafikiria kumsajili kipa wake wa zamani ambaye kwa sasa anaichezea Burnley, James Trafford, mwenye umri wa miaka 22, katika dirisha hili.

Katika mkataba wa mauziano wa kipa huyu, Man City iliweka kipengele cha kumnunua tena ikiwa itahitaji kufanya hivyo na iliwekwa pia kiasi maalumu cha pesa inachopaswa kutoa.


Xavi Simons

KIUNGO wa kati wa RB Leipzig na timu ya taifa ya Uholanzi, Xavi Simons, 22, amewaambia watu wake wa karibu kuwa anapendelea kwenda kucheza Ligi Kuu England kwa msimu ujao ambako Chelsea na Arsenal wanaripotiwa kuifuatilia saini yake. Simons ambaye alionyesha kiwango bora msimu uliopita akicheza mechi 33 za michuano yote na kufunga mabao 11, mkataba wake unaisha 2027.

Luis Diaz

WINGA wa Liverpool na timu ya taifa ya Colombia, Luis Diaz, 28, ameiambia klabu yake kwamba anataka kujiunga na Bayern Munich katika dirisha hili.

Inaelezwa staa huyu alichukizwa na kitendo cha Liverpool kukataa ofa ya Bayern waliyoiwasilisha mapema wiki hii na kuonyesha kuwa kama haiitaji kumuuza. Diaz awali alihusishwa na Barcelona ambayo ilijion


Douglas Luiz

JUVENTUS bado inafikiria mpango wa kubadilishana wachezaji kwa kumtoa kiungo wake raia wa Brazil, Douglas Luiz kwenda Manchester United ili kuipata saini ya mshambuliaji wa klabu hiyo na timu ya taifa ya Denmark, Rasmus Hojlund, 22, katika dirisha hili. Hii sio mara ya kwanza kwa Juventus kutaka kufanya hivyo lakini Man United imekuwa ikikataa.


Armand Lauriente

SUNDERLAND imekubali kutoa Pauni 17.5 milioni kwenda Sassuolo kwa ajili ya kumsajili winga wa timu hiyo na Ufaransa, Armand Lauriente, 25, katika dirisha hili. Taarifa za uhakika kutoka Sky Sports zinaeleza kuwa staa huyo atasafiri kwenda England wiki ijayo kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kukamilisha dili hilo.

Lauriente alishafanya makubaliano binafsi na Sunderland na kilichokuwa kinasubiriwa ni makubaliano juu ya ada ya uhamisho.


Ethan Nwaneri

KIUNGO mshambuliaji wa Arsenal na timu ya taifa ya England, Ethan Nwaneri, 18, amekubali kusaini  mkataba mpya wa miaka mitano wa kuendelea kusalia kwenye timu hiyo.

Awali, ilionekana kuwa na changamoto ya kufikia makubaliano lakini sasa staa huyo atasaini dili hilo jipya linalodaiwa kumpa zaidi ya Pauni 100,000 kwa wiki.

Arsenal ililazimika kuharakisha mchakato wa kutaka kumsainisha mkataba fundi huyu kwa sababu  timu kibao zilianza kumnyemelea.