Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MO SALAH! Kuna kitu anafundisha EPL

Muktasari:

  • Na kuwavuruga zaidi mabosi wake wa huko Anfield, winga huyo wa kimataifa wa Misri ameuwasha moto balaa, akicheza kwa kiwango bora kabisa katika michuano mbalimbali ya msimu huu akiwa chini ya kocha Arne Slot.

LIVERPOOL, ENGLAND: SUPASTAA Mohamed Salah amebakiza miezi isiyozidi sita kwenye mkataba wake wa sasa huko Liverpool.

Na kuwavuruga zaidi mabosi wake wa huko Anfield, winga huyo wa kimataifa wa Misri ameuwasha moto balaa, akicheza kwa kiwango bora kabisa katika michuano mbalimbali ya msimu huu akiwa chini ya kocha Arne Slot.

Gwiji huyo wa Liverpool anachokifanya kwa sasa ni kujiweka pazuri sokoni ili timu nyingine zitakazokuja kumsajili endapo kama ataamua kuachana na Liverpool basi zilazimike kuweka ubaoni mkwanja wa maana. Klabu kadhaa za Saudi Arabia zinahusishwa na mpango wa kumsajili staa huyo.

Mo Salah ameifanya Liverpool kushika usukani kwenye Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kwenye Ligi Kuu England kwa sasa ndiye kinara wa mabao akiwa amefunga mara 19 na akiongoza pia kwenye kuasisti, akifanya hivyo mara 13. Ameshinda Kiatu cha Dhahabu kwenye Ligi Kuu England mara tatu - msimu wa 2017/18, 2018/19 na 2021/22. Alichaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Msimu msimu wa 2017/18.

Aliwahi pia kufunga mabao yaliyoshinda tuzo ya mabao bora ya mwezi kwenye msimu wa 2020/21 na 2021/22.

Amenyakua tuzo sita za Mchezaji Bora wa Mwezi katika miezi ya Novemba 2017, Februari 2018, Machi 2018, Oktoba 2021, Oktoba 2023 na Novemba 2024.

Mavitu ya mkali huyo yamemfanya Mo Salah kuwa na takwimu za kibabe kabisa maisha yake ya soka.

*Mohamed Salah amefunga mabao 234 na kuasisti 105 katika mechi 381 alizoichezea Liverpool.

*Kunogesha hilo, Mo Salah amefunga mabao 311 ya ngazi ya klabu katika mechi 632. Ni wachezaji watatu tu ndiyo waliofunga mabao mengi kwenye kikosi cha Liverpool kumzidi Mo Salah, ambao ni Ian Rush, Roger Hunt na Gordon Hodgson.

*Gordon Hodgson (1.56) ni mchezaji pekee wa Liverpool mwenye wastani mzuri wa bao kwa mechi kumzidi Mo Salah, ambaye ana wastani wa 1.63.

*Salah ndiye mchezaji anayeongoza kwa mabao kwenye Ligi Kuu England kwa wanasoka wa Kiafrika, akiwa amefunga mara 176.

*Salah anashika namba nane kwenye vinara wa mabao wa muda wote kwenye Ligi Kuu England nyuma ya Frank Lampard (177), Sergio Aguero (184), Andy Cole (187), Wayne Rooney (208), Harry Kane (213) na Alan Shearer (260). Yeye ndiye amebaki kwenye ligi hadi sasa.

*Ndiye kinara wa mabao wa Liverpool kwenye mikikimikiki ya Ligi Kuu England.

*Amefunga mabao 74 ugenini kwenye mechi za Ligi Kuu England, ambapo hakuna mchezaji mwingine yeyote wa Liverpool wa zamani au waliopo waliowahi kufanya hivyo kwa maana ya kufunga idadi kama hiyo ya mabao au zaidi.

*Salah amefunga mabao 58 katika mechi 101 alizochezea timu ya taifa ya Misri.

*Salah alifunga bao lake la 100 la Ligi Kuu England uwanjani Anfield dhidi ya Leicester City kwenye Boxing Day, akiwa mchezaji wa nane kufikisha mabao 100 kwenye uwanja wa nyumbani wa timu yake.

*Kwa kufunga mara mbili na asisti moja wakati Liverpool ilipotoka sare ya 3-3 na Newcastle United, Desemba 4, Salah alifunga na kuasisti kwenye Ligi Kuu England kwa mara ya 37, akivunja rekodi ya muda wote ya supastaa Wayne Rooney. Amefanya mara mbili zaidi tangu wakati huo.

*Ameshinda mataji tisa katika maisha yake ya soka, (Premier League, Champions League, FA Cup, EFL Cup, UEFA Super Cup, Fifa Club World Cup).

*Ndiye mchezaji aliyefunga mabao mengi kwenye msimu wake wa kwanza kwenye klabu ya Liverpool, mabao 44 katika msimu wa 2017/18.

*Hakuna mchezaji mwingine wa Liverpool, aliyefunga mabao mengi ndani ya msimu mmoja kwenye kikosi hicho cha Anfield, mabao 34 msimu wa 2017/18.

*Salah anashikilia rekodi ya kufunga kwenye mechi mfululizo katika kikosi cha Liverpool, alipofanya hivyo kwenye mechi 10 mwaka 2021.

*Salah anashika pia rekodi tamu ya kufunga mfululizo kwenye mechi za nyumbani kuanzia mwanzoni  wa msimu, mechi 6 mwaka 2023.

*Hakuna mchezaji aliyefunga mabao mengi mfululizo kwenye mechi za Liverpool ilizocheza uwanjani Anfield, mechi 9 mwaka 2023.

*Mchezaji mwenye mabao mengi ya kimataifa (26) wakati akiwa anaichezea Liverpool: Ian Rush, Michael Owen, Mo Salah.

*Salah alishinda ubingwa wa Super League ya Uswisi kwenye misimu yake yote miwili aliyokuwa FC Basel (2012/13 na 2013/14).

*Salah alifunga hat-trick ya haraka zaidi kwenye historia ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, aliweka pia rekodi ya kufunga hat-trick ya haraka kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa anatokea benchi (dakika 6 na sekunde 12 seconds v Rangers, 2022).

*Hakuna mchezaji aliyeifungia timu ya England mabao mengi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kumzidi Mo Salah (mabao 44).

*Salah ndiye mchezaji Mwafrika mwenye mabao mengi kwenye michuano ya UEFA (61) na ndiye kinara wa mabao wa muda wote wa Kiafrika kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya (47).

*Ndiye mfungaji mengi wa michuano ya Uefa wakati akiwa anazichezea klabu za England, mabao 49.

*Supastaa huyo wa kimataifa wa Misri ndiye kinara wa mabao wa Liverpool kwenye historia ya mikikimikiki ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

*Salah amefunga mabao mengi zaidi kama mchezaji wa Kiafrika kwenye msimu mmoja wa Ligi Kuu England (mabao 32, msimu 2017/18).

*Salah ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi kwenye Ligi Kuu England mara nyingi kama mchezaji ndani ya msimu mmoja (tuzo 3, msimu 2017/18).

*Salah anashikilia rekodi ya kuzifunga timu nyingi kwenye msimu mmoja wa Ligi Kuu England wenye mechi 38, sambamba na Ian Wright na Robin van Persie (amezifunga timu 17, msimu wa 2017/18).