Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jaylen Brown anaiwaza Celtic akilenga ubingwa 76ers

JAMES Pict

Muktasari:

  • Hiyo haikuwa simu ya mzaha. Brown, kweli alikuwa ameuzwa kwenda Philadelphia 76ers ambako alitarajiwa kuunda kikosi cha nyota watatu pamoja na Joel Embiid na Tyrese Maxey. Hakujua LeBron James naye alikuwa njiani kumfuata Philadelphia.

PHILADELPHIA, MAREKANI: JAYLEN Brown alipigiwa simu na kuambiwa Boston Celtics, timu iliyomchagua akiwa kijana na ambayo alikulia hadi kuwa MVP wa fainali za Ligi ya Kikapu Marekani (NBA) na bingwa ilikuwa imemuuza. Na kwa hasira aliitupa simu yake upande wa pili wa chumba alichokuwamo.

Hiyo haikuwa simu ya mzaha. Brown, kweli alikuwa ameuzwa kwenda Philadelphia 76ers ambako alitarajiwa kuunda kikosi cha nyota watatu pamoja na Joel Embiid na Tyrese Maxey. Hakujua LeBron James naye alikuwa njiani kumfuata Philadelphia.

Brown ameanza taratibu kuzoea timu yake mpya, huku akikiri bado anatafakari namna uhusiano wake na Celtics ulivyovunjika kwa namna yenye utata. Kama Brown, 29, angeishi katika dunia aliyoitaka angependa kuendelea kuvaa jezi ya kijani ya Celtics msimu huu na ikiwezekana kwa maisha yake yote ya soka la kikapu, badala ya kuuzwa.

JAME 01

Hata hivyo, sasa yupo tayari kuangalia mbele na kujaribu kushinda ubingwa akiwa na Sixers, ambao wanaweza kuwa na kikosi cha kwanza bora zaidi katika NBA msimu ujao.

“Bado kwa kiasi fulani najaribu kulielewa jambo hili,” amesema Brown juzi.

“Kuna furaha ya kuhamia jiji jipya, sehemu mpya, matarajio mapya na nguvu mpya. Pia kuna kuondoka mahali ulipokaa kwa muda mrefu sana.”

JAME 02

Brown alikuwa chaguo la tatu katika drafti ya NBA 2016 na aliunda ushirikiano mkubwa wa 1-2 uwanjani na Jayson Tatum, ambao uliisaidia Celtics kutwaa ubingwa wa NBA 2024. Uhusiano wao nje ya uwanja uliendelea kuchambuliwa na vyombo vya habari vya NBA, huku swali la kama walikuwa marafiki au la likiwa moja ya mada zilizozungumziwa sana.

Brown, ambaye bado alikuwa na misimu mitatu na takribani Dola 182 milioni katika mkataba wake uliokuwa na thamani ya Dola 304 milioni kwa miaka mitano alioutia saini 2023, alizungumza kwa heshima kuhusu Tatum, lakini amesema, “hawakuwa wamezungumza sana” tangu uhamisho huo.

JAME 03

“Tulishinda ubingwa pamoja,” amesema Brown. “Mtu yeyote ambaye unashinda naye ubingwa unafikiri hilo ndilo linalounda undugu au urithi wa maisha. Lakini bila shaka, katika aina yoyote ya uhusiano kuna kupanda na kushuka.”

Kwa miaka kadhaa iliyopita, Brown amekuwa akizungumzia namna alivyohisi kutothaminiwa na vyombo vya habari pamoja na baadhi ya watu ndani ya NBA licha ya mafanikio aliyoyapata. Ingawa alitwaa tuzo za MVP wa fainali za Eastern Conference na NBA Finals katika mbio za ubingwa wa Celtics, aliachwa nje ya kikosi cha Marekani kilichoshiriki Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024.

JAME 04

Msimu uliopita, Tatum alipocheza mechi 16 pekee katika msimu wa kawaida huku akiendelea kupona jeraha, Brown alifikisha wastani bora zaidi wa maisha yake wa pointi 28.7, ribaundi 6.9 na asisti 5.1 kwa mchezo. Pia alimaliza katika nafasi ya sita katika kura za MVP.

Celtics kisha walimuweka Brown sokoni kama sehemu ya mpango wa kumtumia katika kubadilishana na Giannis Antetokounmpo wa Milwaukee, lakini mpango huo haukufanikiwa. Brown amesema, “mchakato mzima” wa namna safari yake Boston ilivyofikia mwisho ulimuumiza.

JAME 05

“Labda siku moja tutasimulia kwa undani namna kila kitu kilivyotokea na mambo yote yaliyohusika. Kumekuwapo na minong’ono na mawazo mengi; sioni sababu ya kuingia humo kwa sababu nacholenga ni kilicho mbele yangu,” amesema.