Messi kujifunga Barcelona

Wednesday July 14 2021
MESSI PIC
By Mwandishi Wetu

Baada ya staa wa Barcelona, Lionel Messi kufikia makubaliano ya awali ya kubaki kwenye klabu hiyo mpaka Juni 2023, sasa staa huyo anatarajiwa kusaini mkaba mpya wa miaka mitano.

Taarifa zinasema kuwa Messi hakuwa na wasiwasi kama ilivyoripotiwa wiki zilizopita, sasa ana uhakika wa asilimia 100 kubaki kwenye klabu hiyo baada ya kufikiwa makubaliano wiki zilizopita.

Awali Messi alifikia makubaliano na klabu hiyo ya kuongeza mkataba mpaka mwaka 2023 lakini atasaini mkataba wa miaka mitano ambao utambakisha hapo mpaka mwaka 2026 ambao utakuwa wa Pauni 600 milioni.

Taarifa zinasema kuwa ni suala la muda tu ambapo klabu itatoa tangazo rasmi.

Hakuna shaka, Mesi atabaki Barcelona

Advertisement