Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beckham aanza kuisuka MSN ile ya Barcelona

Muktasari:

  • Nyota huyo wa Brazil anadaiwa kwamba huenda akaungana tena na waliokuwa wachezaji wenzake wa Barcelona, Lionel Messi na Luis Suarez ambao wanaitumikia Inter Miami kwa sasa.

MIAMI, MAREKANI: MMOJA wa wamiliki wa Klabu ya Inter Miami ya Marekani, David Beckham anadaiwa kuanza kupambana kuuleta mojawapo wa muunganiko mkubwa zaidi katika historia ya soka kwa kumnunua Neymar JR ili kuifufua safu maarufu ya ushambuliaji ya MSN iliyokuwa Barcelona.

MSN ilimaanisha Messi, Suarez na Neymar.

Nyota huyo wa Brazil anadaiwa kwamba huenda akaungana tena na waliokuwa wachezaji wenzake wa Barcelona, Lionel Messi na Luis Suarez ambao wanaitumikia Inter Miami kwa sasa.

Kiungo wa zamani wa Brazil, Felipe Melo, amesema ameambiwa kuwa Neymar anatarajiwa kuhamia Miami baada ya kumalizika kwa mkataba wake na Santos ya nchini kwao.

Akizungumza kwenye YouTube, Melo alisema: “Nilizungumza na rafiki yangu ambaye hapo awali alinipa taarifa kuhusu Santos. Aliniambia Neymar atacheza Miami. Kuanzia Januari, Neymar atakuwa Miami. “Ikitokea hivyo, nitakuwa mtu wa kwanza kuvujisha habari hii hapa. Tusubiri tuone kitakachotokea.”

Mustakabali wa Neymar umekuwa miongoni mwa mada zinazozungumziwa zaidi katika soka la dunia, huku mkataba wake na Santos ukitarajiwa kumalizika Desemba 31, 2026.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 amekuwa akihusishwa na uhamisho wa kwenda kwa vigogo wa Uturuki, Galatasaray, lakini kauli za Melo zimeibua tena tetesi kwamba Inter Miami inaweza kuwa kituo chake kinachofuata. Na iwapo Beckham ataweza kufanikisha uhamisho huo, utakuwa muunganiko wa safu maarufu ya ushambuliaji ya MSN iliyowatesa wapinzani Ulaya wakati wa enzi zao Barcelona.

Messi, Neymar na Suarez waliunda moja ya safu hatari zaidi za ushambuliaji kuwahi kushuhudiwa katika soka kati ya 2014 na 2017, wakichanganya ufundi, kasi na umaliziaji wa kikatili. Kwa pamoja walishinda mataji tisa wakiwa Barcelona ikiwemo Ligi ya Mabingwa Ulaya, mataji mawili ya La Liga na Kombe la Dunia la Klabu. Msimu wao wa kwanza pamoja ulizaa Barcelona mataji matatu ya kihistoria chini ya kocha Luis Enrique, huku watatu hao wakifunga jumla ya mabao 122 katika mashindano yote.

Messi alikuwa kinara kwa kufunga mabao 58, Neymar akafunga 39 na Suarez akachangia 25, huku Barcelona ikiwasambaratisha wapinzani kwa kutumia moja ya safu ya ushambuliaji iliyotisha zaidi katika historia ya soka. Na sasa, Inter Miami ya Beckham inaweza kuwa mwisho ya hadithi hiyo.