Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bellingham aanza kumkera Mourinho

Muktasari:

  • Jumatatu asubuhi, Marc Cucurella, Kylian Mbappe na Ibrahima Konate walikamilisha vipimo vyao vya kawaida vya afya na kujiunga na kikosi cha Mourinho, hatua iliyompa kocha huyo nguvu zaidi katika maandalizi ya msimu, lakini inaelezwa ameanza kukerwa na Jude kuchelewa.

MADRID, HISPANIA: KOCHA wa Real Madrid, Jose Mourinho anaendelea kurejeshewa wachezaji muhimu kuelekea mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Hispania (LaLiga) dhidi ya Espanyol, utakaochezwa Agosti 22, lakini hadi jana jioni kiungo wa England, Jude Bellingham alikuwa hajaripoti kambini.

Jumatatu asubuhi, Marc Cucurella, Kylian Mbappe na Ibrahima Konate walikamilisha vipimo vyao vya kawaida vya afya na kujiunga na kikosi cha Mourinho, hatua iliyompa kocha huyo nguvu zaidi katika maandalizi ya msimu, lakini inaelezwa ameanza kukerwa na Jude kuchelewa.

Mchezaji pekee ambaye alikuwa bado hajaripoti ni Bellingham, ingawa alitarajiwa kuwasili jana. Hata hivyo, kocha huyo hajafurahishwa na kuchelewa kwake. Dalili zote zinaonyesha kuwa hakuna hata mmoja kati ya wachezaji hao watano atakayeambatana na timu leo kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Deportivo de La Coruna katika mashindano ya Trofeo Teresa Herrera. Badala yake, wataendelea na programu maalumu ya mazoezi binafsi iliyopangwa kuhakikisha wanafikia kiwango bora cha utimamu wa mwili kabla ya mchezo wa kwanza wa ligi. Hata hivyo, wanaweza kuwa tayari kwa mchezo wa Jumapili ijayo dhidi ya Schalke 04, ambapo huenda wakacheza mechi zao za kwanza katika maandalizi ya msimu mpya.

Cucurella na Konate wanaanza ukurasa mpya katika klabu hiyo, huku beki wa pembeni wa Hispania, Cucurella, tayari akitajwa miongoni mwa usajili bora wa Real Madrid katika dirisha hili la majira ya kiangazi.