Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Memphis yagoma kumlipa marehemu

NBA Pict

Muktasari:

  • Kifo cha Clarke kinaendelea kuibua maswali katika ulimwengu wa mpira wa kikapu ndani na nje ya uwanja na taarifa za karibuni zilidai chanzo kilikuwa matumizi kupita kiasi ya dawa za kulevya yakihusisha mchanganyiko wa heroine na cocaine.

MEMPHIS, MAREKANI: MSHAHARA wa Dola 12.5 milioni wa staa wa zamani wa Ligi ya Kikapu Marekani (NBA), Brandon Clarke aliyefariki dunia Mei, mwaka huu akibakiza msimu mmoja katika mkataba wake hautalipwa na klabu yake ya Memphis Grizzlies.

Kifo cha Clarke kinaendelea kuibua maswali katika ulimwengu wa mpira wa kikapu ndani na nje ya uwanja na taarifa za karibuni zilidai chanzo kilikuwa matumizi kupita kiasi ya dawa za kulevya zenye mchanganyiko wa heroine na cocaine.

Mchezaji huyo aliyekuwa na umri wa miaka 29 wakati wa kifo chake, alikuwa amebakiza msimu mmoja katika mkataba alioutia saini 2022, huku akiwa bado anadai  mshahara wa Dola 12.5 milioni.

Hata hivyo, fedha hizo hazitalipwa moja kwa moja na Memphis Grizzlies kwa warithi wa Clarke, kwani mshahara uliobaki unalindwa na bima nje ya klabu.

NB 01

Hali hiyo imesababisha mkanganyiko baada ya wakala wa Clarke, Mark Bartelstein kupinga taarifa kwamba familia haitapata fedha ilizokuwa ikidai chini ya mkataba huo hasa baada ya klabu kujiweka kando. Bima pia imegoma kueleza lolote juu ya suala hilo.

Inaelezwa kwamba Grizzlies walikuwa tayari wamemlipa Clarke mshahara wake wa msimu wa 2025/26, ambao ulikuwa umemalizika wakati wa kifo chake. Malipo yaliyobaki kutoka kwa klabu yataendelea hadi Oktoba, ambapo uhusiano wa kimkataba utakoma.

Kwa mujibu wa Mkataba wa Pamoja wa Majadiliano (CBA) wa NBA, ajira ya  mchezaji hukoma anapofariki dunia. Hata hivyo, hilo halimaanishi kwamba warithi walioachwa hupoteza fedha zilizokuwa katika mkataba wake.

NB 02

Ripoti zinaonyesha kuwa Dola 12.5 milioni zilizokuwa zimebaki kama mshahara wa Clarke hazitatoka moja kwa moja kwenye orodha ya mishahara ya Grizzlies, wala hazitahesabiwa katika malipo ya mishahara ya klabu hiyo, licha ya kuwa sehemu ya mkataba kati ya mchezaji na klabu.  Badala yake, bima nje ya klabu ndiyo inayopaswa kulipa.

Mkataba wa pamoja wa NBA unaruhusu klabu kuweka bima kwenye mikataba ya wachezaji dhidi ya vifo, fedha ambazo hulipwa endapo atafariki dunia.

Hata hivyo, huenda chanzo cha kifo chake kiliporitiwa kuwa matumizi kupita kiasi ya dawa za kulevya, kikaathiri malipo hayo kutokana na  masharti ya bima yake kuwa na vipengele vinavyoweza kuzuia au kuyapunguza. Kw sasa hakuna dalili kwamba familia ya Clarke itapoteza fedha chini ya mkataba wake.

NB 03

Kabla ya kifo majeraha yaliathiri uchezaji wake, kwani alipata jeraha la kuchanika kwa misuli ya mguu mwaka 2023, kabla ya baadaye kupata jeraha la nyuma ya goti la kulia 2025. Clarke alimaliza maisha yake ya uchezaji NBA akiwa amecheza michezo 309 ya msimu wa kawaida, akifunga wastani wa pointi 10.2 na ribaundi 5.5 kwa mchezo.

Kifo chake kilikuwa cha kwanza cha mchezaji aliyekuwa bado anacheza NBA tangu Bryce Dejean-Jones aliyefariki 2016 akiwa mchezaji wa New Orleans Pelicans.