Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sikia kituko cha LeBron

Muktasari:

  • LeBron James hana utamaduni huo na hatanunua bando ili tu afanye mawasiliano, badala yake amekuwa akitumia Wi-Fi ili kumrahisishia mawasiliano.

LOS ANGELES, MAREKANI: NANI kakuambia ukiwa bilionea ni lazima ununue bando? Lile la kutumia intaneti katika simu yako? Supastaa mpya katika kikosi cha Philadelphia 76ers kinachoshiriki Ligi ya Kikapu Marekani (NBA).

LeBron James hana utamaduni huo na hatanunua bando ili tu afanye mawasiliano, badala yake amekuwa akitumia Wi-Fi ili kumrahisishia mawasiliano.

Nyota huyo aliyetua 76ers hivi karibuni akitokea Los Angeles Lakers aliyoitumikia tangu 2018, anatajwa kuwa miongoni mwa wanamichezo mabilionea duniani akiwaacha mbali mastaa kibao wakiwamo wale wa soka, lakini hatumii pesa zake kununua bando isipokuwa muda tu wa maongezi katika simu yake. Utajiri wa LeBron unatajwa kuwa takriban Dola 1.3 bilioni.

LeBron James amepata mamia ya mamilioni ya dola katika kipindi cha kucheza kwake NBA na kujenga utajiri mkubwa, lakini bado hataki kukua huduma hiyo kutoka kwa watoa huduma kwa kutoapesa yake mfukoni.


Hata anapokuwa safarini mchezaji huyo kwa muda mrefu amekuwa akikwepa kulipia huduma ya intaneti ya simu (data roaming), badala yake kila anawapo safirini nje ya Marekani amekuwa akisubiri kufanya mawasiliano hadi atakapopata huduma ya Wi-Fi.

Tabia yake hiyo imefichuliwa na aliyekuwa mchezaji mwenzake, Dwyane Wade, ambaye alimtaja LeBron mara moja alipoulizwa ni mchezaji gani wa NBA anayemfahamu ambaye ni 'bahiri' zaidi katika matumizi ya fedha.

Alisema LeBron amekuwa akitumia pesa zake mara nyingi kufanyia matumizi mengineyo, lakini suala la intaneti halipi kipaumbele hadi anapokuwa katika eneo lenye huduma ya Wi-Fi, ikiwamo nyumbani, ofisini au nyumbani kwake, lakini siyo mahali pengine popote zaidi ya maeneo hayo.

Mchezaji mwenzake wa zamani waliyecheza pamoja Cleveland Cavaliers, Kevin Love, alidai LeBron huchukulia suala hilo kwa umakini, akikumbuka safari walizowahi kufanya kwenda Toronto, Canada ambapo nyota huyo alikuwa akiishi bila kutumia data za simu wakati wa safari kutoka uwanja wa ndege hadi hotelini, na alikuwa akiunganisha simu yake kwenye Wi-Fi ya hotelini kisha kuzima tena huduma hiyo wakati wa safari kuelekea uwanjani hadi atakapopata Wi-Fi.

Kwa mmoja wa wanamichezo wenye utajiri mkubwa zaidi duniani, kiasi alichokuwa akiokoa kilikuwa kidogo sana. Lakini James hakuona sababu ya kulipia huduma hiyo.

Hatimaye LeBron alithibitisha habari hiyo katika mahojiano na Rachel Nichols wa ESPN, alipoulizwa kuhusu huduma ya data katika simu, alisema: “Hapana, sifanyi hivyo.” Akimaanisha kwamba hanunui, kisha akafichua kwamba tabia hiyo ilihusisha pia matumizi mengine madogo.

“Situmii 'data roaming', sinunui bando,” alisema mchezaji huyo.

Nichols alipomkumbusha kwamba bila shaka alikuwa tajiri na angeweza kumudu gharama hizo, LeBron hakusita kujibu: “Sitalipia!”

Kuwa bilionea hakukubadilisha mtazamo wake, kinyume chake tofauti hiyo imezidi kuonekana kadiri miaka inavyokwenda.

Forbes ilimtangaza LeBron kuwa bilionea 2022, na kumfanya kuwa mchezaji wa kwanza aliyekuwa bado anacheza NBA kufikia kiwango hicho cha utajiri ambao umeendelea kuongezeka kupitia mishahara ya NBA, mikataba ya udhamini na uwekezaji mbalimbali.

Hata hivyo, kukataa kwake kulipia bando kumekuwa mojawapo wa mifano maarufu ya namna anavyoshughulikia baadhi ya matumizi yake ya fedha kwa mtazamo tofauti.

Love aliwahi kufanya mzaha kwamba kulikuwa na mantiki fulani katika tabia hiyo, akirejea msemo wa kifedha unaosema: “Tundu dogo linaweza kuizamisha meli kubwa.” Kwa LeBron, hata hivyo, sababu inaonekana kuwa rahisi zaidi, ana uwezo wa kulipia bando, lakini hataki.