Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baada ya miaka 18 NBA Westbrook astaafu

Muktasari:

  • Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 ambaye aliwahi kushinda tuzo ya MVP ametangaza uamuzi huo kupitia video ya kuaga iliyosimuliwa na mwigizaji Michael B Jordan, na hivyo kufunga ukurasa wa moja ya safari zenye ubora katika kizazi chake.

NEW YORK, MAREKANI; NYOTA wa kikapu wa Sacramento Kings, Russel Westbrook ametangaza kustaafu baada ya kucheza kwa mafanikio makubwa NBA kwa kipindi cha miaka 18.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 ambaye aliwahi kushinda tuzo ya MVP ametangaza uamuzi huo kupitia video ya kuaga iliyosimuliwa na mwigizaji Michael B Jordan, na hivyo kufunga ukurasa wa moja ya safari zenye ubora katika kizazi chake.

“Wakati mwingine hata hujui kama tayari umeutazama mwisho,† Westbrook aliandika. “Ulipaswa kuwa pale. Na sasa yote yamekwisha.

Westbrook alianza kucheza NBA 2008 baada ya kuchaguliwa katika nafasi ya nne kwa ujumla katika drafti na Seattle SuperSonics ambayo  ilibadilika na kuitwa Oklahoma City kabla hajacheza mechi yake ya kwanza, na haraka akawa mmoja wa wachezaji muhimu wa Thunder.

Alitumia miaka 11 Oklahoma City, ambako alitengeneza ushirikiano na Kevin Durant na James Harden uwanjani na watatu hao waliisaidia Thunder kufika fainali za NBA 2012, ingawa walishindwa na Miami Heat.

Kilele cha mafanikio binafsi ya Westbrook kilifika miaka kadhaa baadaye, kwani katika msimu wa 2016/17 alifunga wastani wa pointi 31.6, ribaundi 10.7 na asisti 10.4 kwa kila mchezo, na kuwa mchezaji wa kwanza tangu Oscar Robertson kufikisha wastani wa ‘triple-double’ katika msimu mzima.

Alishinda tuzo ya MVP na kuweka rekodi ya NBA ya ‘triple-double’ 42 katika msimu huo na ikawa alama iliyotambulisha zaidi maisha yake  katika NBA. Mwaka 2021 alivunja rekodi ya muda mrefu ya Oscar Robertson ya ‘triple-double’ 181 katika historia ya NBA na hatimaye akafikisha jumla ya 209, rekodi ambayo ni kubwa zaidi katika historia ya ligi hiyo.

Pia akawa mchezaji wa pili baada ya LeBron James kufikisha angalau pointi 25,000 na asisti 10,000 katika mashindano hayo. Alichaguliwa mara tisa kwenye All-Star na mara tisa kwenye All-NBA. Westbrook alimaliza maisha yake NBA akiwa na pointi 27,176 na asisti 10,351.

Wastani wake wa maisha yote ya NBA wa pointi 20.9, asisti 8.0 na ribaundi 6.9 kwa kila mchezo unaonyesha kiwango bora alichokuwa nacho kwa karibu miongo miwili. Baada ya kuondoka Oklahoma City 2019, Westbrook alichezea Houston, Washington, Los Angeles Lakers, Los Angeles Clippers, Denver na Sacramento.

Licha ya kupewa nafasi ndogo zaidi kadiri miaka ilivyokwenda, aliendelea kuwa mchezaji mwenye ushawishi mkubwa kama mkongwe na kuendelea kutoa mchango mzuri uwanjani. Msimu wake wa mwisho wa NBA ulikuwa na Sacramento Kings, ambako alicheza mechi 64 na kupata wastani wa pointi 15.2, asisti 6.7 na ribaundi 5.4 kwa kila mchezo.

Hata hivyo, ubingwa wa NBA ndio tuzo kubwa iliyokosekana katika wasifu wake. Westbrook alifika fainali za NBA mara moja pekee, mwaka 2012.