Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba Queens bado utimamu

SIMBA Q Pict

Muktasari:

  • Simba Queens ipo nchini Kenya kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo, huku ikitumia mechi za kirafiki kupima hali ya kikosi chake baada ya kuanza maandalizi ya msimu mpya.

KAIMU Kocha Mkuu wa Simba Queens, Mohamed Mrishona ‘Xavi’ amesema mechi mbili za kirafiki walizocheza nchini Kenya zimewapa picha ya maeneo wanayotakiwa kuyafanyia kazi kabla ya kuanza kwa michuano ya CECAFA kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika itakayoanza Agosti 21, 2026 nchini Rwanda.

Simba Queens ipo nchini Kenya kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo, huku ikitumia mechi za kirafiki kupima hali ya kikosi chake baada ya kuanza maandalizi ya msimu mpya.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mrishona amesema suala la utimamu wa mwili ni moja ya maeneo wanayoyafanyia kazi kwa nguvu ili kuhakikisha wachezaji wanafikia kiwango kinachohitajika kwenye siku mbili zilizobaki kabla ya kuingia kwenye mashindano ya CECAFA.

SIMBA Q Pict

Mbali na utimamu wa mwili, kocha huyo amesema bado kuna kazi ya kutengeneza muunganiko wa timu, jambo ambalo amelieleza kuwa ni miongoni mwa mambo makubwa yaliyobaki kabla ya kuelekea Rwanda.

“Mechi hizi mbili zimetupa picha tofauti na tulivyoanza. Tumeona bado fitnesi ya wachezaji haiko sawa, hivyo tunapambana kuhakikisha wanafikia kiwango kizuri. Pia combination bado haijawa nzuri, hiyo ndiyo kazi kubwa iliyobaki,” amesema Mrishona. Baada ya mechi hizo, Simba Queens itakuwa na mechi nyingine dhidi ya Kibera Soccer, kisha itakaa siku moja nchini Kenya na kuanza safari ya kuelekea Rwanda kwa ajili ya kuanza rasmi mashindano hayo.

SIM 03

Timu hiyo imepangwa kundi C pamoja na Kenya Police Bullets ya Kenya na Top Girls ya Burundi, huku kundi A likiwa na Rayon Sports ya Rwanda, Yei Joints ya Sudan Kusini, Mafunzo SC ya Zanzibar na Denden FC ya Eritrea. Kundi B lipo na CBE ya Ethiopia, Kawempe Ladies ya Uganda na FC Ujeco ya Djibouti.

Tangu mashindano ya CECAFA yaanzishwe mwaka 2021 huku Vihiga Queens ikibeba ubingwa huo kwa mara ya kwanza, Simba Queens imeshiriki mara mbili, mwaka 2022 na 2024. Kwenye ushiriki wake wa kwanza, Simba Queens iliandika rekodi ya kuwa bingwa wa kwanza CECAFA kutoka Tanzania na kufuzu Ligi ya Mabingwa.