Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbio za ubingwa EPL… Ukijichanganya, unachanganyikiwa!

MBIO Pict

Muktasari:

  • Kama kulihitajika uthibitisho wowote, basi ulikuwa namna ambavyo Man City ilivyopambana kurejea kwenye mchezo dhidi ya Liverpool na jinsi ilivyosherehekea baada ya mechi ilionyesha wazi umuhimu wake.

LONDON, ENGLAND: MBIO za ubingwa zina kila dalili ya kuwa za kihistoria. Na jambo ambalo sasa liko wazi kabisa ni kwamba Manchester City iko tayari kupambana na Arsenal hadi hatua ya mwisho.

Kama kulihitajika uthibitisho wowote, basi ulikuwa namna ambavyo Man City ilivyopambana kurejea kwenye mchezo dhidi ya Liverpool na jinsi ilivyosherehekea baada ya mechi ilionyesha wazi umuhimu wake.

Pep Guardiola alipunguza pengo la pointi hadi kufikia sita dhidi ya vinara Arsenal na kwa mechi 13 zilizosalia ni dhahiri kuwa kutakuwa na misukosuko mingi njiani.

Pointi tisa zingekuwa pengo kubwa sana, lakini sasa Man City ina matumaini halisi ya kuwafikia Arsenal katika wiki zijazo.

Arsenal inapaswa kusafiri kwenda Brentford, Alhamisi usiku mechi ambayo itakuwa ngumu sana na pengo linaweza kupungua hadi pointi tatu kwani Man City itaikaribisha Fulham, Jumatano usiku.

Kisha Man City itakutana na Newcastle United (nyumbani), ikifuatiwa na Leeds United (ugenini), Nottingham Forest (nyumbani) na West Ham (ugenini). Baada ya hapo, Man City itacheza na Arsenal kwenye fainali ya Kombe la Carabao huko Wembley, Machi 22 na bila shaka mshindi wa mchezo huo atapata morali na kujiamini zaidi.

Kwa upande mwingine, Arsenal baada ya safari yao ya Brentford, itakutana na Wolves (ugenini), Tottenham (ugenini), Chelsea (nyumbani), Brighton (ugenini) na Everton (nyumbani) kabla ya mchezo wa Wembley.

Inaonekana kama michezo ijayo ya Man City inaweza kuwapa faida kidogo na nafasi ya kupunguza pengo, lakini mbio hizi za ubingwa hakika bado zina purukushani nyingi.

Ndiyo maana msimu huu ni wa kusisimua na usiokuwa wa kukata tamaa. Ndiyo maana Man City walisherehekea kwa shangwe kubwa Anfield kwa sababu ushindi huo uliwaweka wazi bado wamo kwenye mbio.

Man City imekuwa na kiwango bora chini ya Guardiola na kinachovutia ni kwamba ipo kwenye vita ya ubingwa dhidi ya timu inayonolewa na aliyekuwa msaidizi wake, Mikel Arteta.