Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kagere: Simba Day imenikumbusha...

KAGERE Pict


MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba, Meddie Kagere, amesema kutambuliwa kwake kama mmoja wa magwiji wa klabu hiyo ni heshima ambayo ataendelea kuithamini katika maisha yake yote.


Kagere alikuwapo katika tamasha la Simba Day lililofanyika Jumamosi ya Agosti 8, 2026 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, ambapo alipata nafasi ya kukutana na Wanasimba na kutambuliwa kwa mchango wake alioutoa wakati akiwa sehemu ya kikosi hicho.


Mshambuliaji huyo raia wa Rwanda, alicheza kwa misimu minne Simba, kuanzia 2018-2019 hadi 2021-2022, akifunga jumla ya mabao 65 katika Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kagere amesema kitendo cha Simba kumtambua hakitafuta nafasi katika kumbukumbu zake.

“Simba ni familia. Najisikia furaha kutambuliwa kama legendari. Naona jasho langu halikuenda bure, kwa sababu bado nipo kwenye mioyo ya mashabiki wa klabu hii,” amesema Kagere.

Ameongeza: “Tuzo niliyopewa naichukulia kwa heshima na uzito mkubwa. Imeweka kumbukumbu ambayo sitakaa niisahau. Nimepata faraja kubwa sana.”

Kagere amesema baada ya kupata mwaliko wa kushiriki Simba Day, hakusita, akieleza kuwa maisha aliyoyapitia ndani ya klabu hiyo pamoja na mapenzi aliyoyapata kutoka kwa mashabiki yalimfanya ajisikie sehemu ya familia hiyo.

Kagere amesema ushiriki wake katika tamasha hilo ulimrudisha kwenye kumbukumbu za mwaka 2018, wakati alipojiunga na Simba akitokea Gor Mahia ya Kenya.

Amesema alitambulishwa mbele ya mashabiki katika Simba Day 2018, jambo lililomfanya tukio la mwaka huu kuwa na maana kubwa kwake.

“Wakati najiunga kwa mara ya kwanza na Simba msimu wa 2018-2019 nikitokea Gor Mahia ya Kenya, nilitambulishwa katika tamasha la Simba Day. Hivyo nimejikuta nakumbuka mambo mengi sana,” amesema.

Kagere amesema siku hiyo ya kwanza ya kutambulishwa ilimsaidia kutambua ukubwa wa Simba na wajibu uliokuwa mbele yake.

“Binafsi ninachokikumbuka wakati natambulishwa, umati wa watu ulinipa picha ya kujua ukubwa wa kazi ambayo ilikuwa mbele yetu. Hivyo nikawa najituma zaidi katika mazoezi,” amesema.

Kagere, ambaye aliwahi kuwa miongoni mwa washambuliaji tegemeo wa Simba, amewataka wachezaji waliopo sasa kuhakikisha wanapambana kwa bidii ili waache historia itakayokumbukwa na mashabiki.

“Hilo ndilo ninaloweza kuwaambia wachezaji wa sasa; wapambane zaidi ili na wao waache alama zao za kukumbukwa.”

Katika misimu yake minne Simba, Kagere alifunga mabao 65 ya Ligi Kuu Bara, akifanya muda wake klabuni hapo kuwa wenye mafanikio makubwa zaidi.