Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbinu za Arteta zilivyoizamisha Everton ngumu Goodison Park

MBINU Pict

BAADA ya mapema jana Jumamosi Manchester City kukamilisha ushindi uliotarajiwa dhidi ya West Ham katika mechi ya Ligi Kuu y England (EPL), Arsenal ilijua ni ushindi pekee dhidi ya Everton ndio ungeirejesha kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kabla ya Sikukuu ya Krismasi.

Ingawa Everton imekuwa timu ngumu kuifunga chini ya Kocha David Moyes, lakini rekodi tamu za hivi karibuni kwa Gunners dhidi ya Toffees, ikiwa haijapoteza katika mechi tano zilizopita walizokutana katika Ligi Kuu, ziliwabeba mbele ya wenyeji wao hao na kutoka na ushindi wa bao 1-0.

Katika mechi hiyo ya jana, Everton ilikuwa inatafuta ushindi wao wa kwanza dhidi ya Arsenal tangu 2023.

Hata hivyo, timu ya Kaskazini mwa London ilikuwa imeshinda mechi tatu tu kati ya 13 za ugenini ilizocheza katika upande wa buluu wa Merseyside (sare 4, kufungwa 6) na ushindi mmoja tu kati ya saba za hivi karibuni, uliopatikana msimu wa 2023/24 kupitia bao la ushindi la Leandro Trossard.

Trossard, ambaye Mikel Arteta alimchagua badala ya Gabriel Martinelli kwa mechi ya jana Jumamosi, alikuwa amefunga (mabao mawili) au kusaidia (pasi moja ya bao) katika mabao matatu kati ya sita ya mwisho ya Arsenal dhidi ya Everton katika Ligi Kuu.

Tangu Februari 2023, Everton haikuwa imepata pointi tatu dhidi ya Arsenal katika Ligi, hivyo mechi hiyo ilikuwa muhimu kwao kama njia ya kuonyesha dhamira yao kwa msimu mzima.

Zaidi ya hayo, Everton ilikuwa imepoteza mechi tatu tu kati ya 17 za nyumbani katika Ligi Kuu (ikishinda 7, sare 7), ingawa vipigo viwili vilikuja katika mechi zao nne za mwisho (dhidi ya Tottenham na Newcastle).

MBI 01

GUNNER HAIJAFUNGWA MECHI 14 ZA JIONI

Kwa ushindi nne na vipigo viwili katika mechi zao sita za mwisho za Ligi, kikosi cha Moyes kilikuwa miongoni mwa timu zenye kiwango kizuri. Kwa upande mwingine, timu ya Arteta ilikuwa imeshinda tatu, sare mbili, na kupoteza moja katika mechi zao sita za hivi karibuni.

Arsenal ilikuwa haijapoteza katika mechi 14 za EPL zilizochezwa jioni, tangu ilipofungwa mabao 2-0 nyumbani na West Ham Desemba 2023.

Hata hivyo, Gunners ilikuwa imepoteza mechi nne kati ya sita ilizocheza ugenini katika uwanja mpya kwa mara ya kwanza (ikishinda 2). Uwanja wa Hill Dickinson ulikuwa wa 60 wa ugenini ilyiowahi kucheza katika Ligi Kuu.

Jambo lililompa Moyes wasiwasi ni kuwa wafungaji wa mabao mawili ya mwisho dhidi ya Arsenal, Idrissa Gueye na Iliman Ndiaye hawakuwepo kutokana na ushiriki wao wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 inayoanza usiku wa leo huko Morocco.

Hilo lilimaanisha wachezaji kama Jack Grealish, Charly Alcaraz na Dwight McNeil walilazimika kuchukua jukumu hilo.

MBI 02

MWANZO WA TAHADHARI

Mwanzo wa tahadhari kutoka kwa pande zote mbili uliifanya mechi ikose msisimko katika dakika 15 za mwanzo. Kwa kweli, hakuna mchezaji wa Arsenal aliyegusa mpira ndani ya eneo la hatari la Everton hadi muda huo.

Muda mfupi baadaye, mkono wa Jake O’Brien ulisababisha penalti na Viktor Gyökeres alipata nafasi ya kufunga na kweli aliitumia vyema kuandika bao lake la tano na kuwa mchezaji wa kwnza wa Gunners kufikisha idadi hiyo katika EPL msimu huu.

Huo ulikuwa mkwaju wa penalti wa 15 mfululizo kufungwa na Arsenal, mara ya mwisho Bukayo Saka kukosa penalti ikiwa ni Aprili 2023 dhidi ya West Ham.

Bao hilo lilikuwa la kwanza kwa mshambuliaji huyo wa Uswidi tangu mwanzo wa Novemba na la tano msimu huu kwenye Ligi Kuu, likimfanya kuwa mfungaji bora wa Arsenal msimu huu.

Ingawa bao lake ndilo lililotofautisha timu hizo, Gyökeres alikuwa amepiga pasi tatu tu kabla ya kwenda mapumziko, idadi ndogo kuliko mchezaji yeyote uwanjani, jambo linaloonekana kuwa kawaida katika maisha yake tangu atue Arsenal.

Mwisho wa mechi, alikuwa amegusa mpira mara 18 tu, idadi ambayo ilikuwa angalau 36 chini ya wachezaji wenzake wengine waliocheza tangu mwanzo.

MBI 03

HAKUNA SHUTI LA EVERTON 45 ZA KWANZA

Kwa kumiliki mpira kwa asilimia 70 kati ya dakika ya 15 na 30 za kipindi cha kwanza, Arsenal ilionekana kutawala mechi na kabla ya mapumziko ilipiga mashuti matatu zaidi.

Kwa upande wa wenyeji, Everton haikupiga shuti hata moja la kulenga lango wala la kukosa, hadi mapumziko, hii ikiwa ni mara ya pili tu tangu 2003/04 kwa hali hiyo kutokea katika mechi ya nyumbani ya Ligi Kuu.

MBI 05

UDHIBITI WA PASI KWA GUNNERS

Tofauti kubwa kati ya timu hizo ilikuwa ubora wa pasi. Wachezaji wa Arsenal walipigiana pasi kwa urahisi huku wengi wakifikia asilimia zaidi ya 90 ya pasi zilizokamilika, wakati Everton walishindwa kuvuka asilimia 75.

Declan Rice, Piero Hincapié na William Saliba walitawala takwimu za pasi, ingawa nyingi zilikuwa ni za kurudishiana au nyuma, Arsenal wakijaribu kuwachosha washambuliaji wa Everton.

Alcaraz baadaye alitolewa, licha ya kuwa ndiye mchezaji pekee wa Everton aliyeonyesha dhamira ya kushambulia. Alipiga mashuti matatu na kugusa mpira mara nne ndani ya eneo la Arsenal zaidi ya wachezaji wenzake.

MBI 04

1-0 TENA KWA GUNNERS

Mwisho wa mechi, Arsenal ilikuwa imepiga pasi 654, idadi kubwa zaidi msimu wa 2025/26, ikionyesha ubora wao katika mechi iliyotarajiwa kuwa ngumu sana ugenini.

Ingawa Everton ilipambana kwa nguvu, ikiongozwa na James Tarkowski na Michael Keane katika mapambano ya mtu kwa mtu, lakini walikosa ubora wa kushambulia unaohitajika kuifunga timu inayopigania ubingwa.

Everton sasa imeshindwa kufunga katika mechi sita kati ya 17, huku ni Wolves (10) na Nottingham Forest (8) pekee waliofeli kufunga mara nyingi zaidi msimu huu.

Kwa Arsenal, hiyo ilikuwa mechi yao ya tisa bila kufungwa bao katika mechi 17, zaidi ya timu yoyote katika EPL msimu huu wa 2025/26.

Kauli maarufu ya “1-0 kwa Arsenal” inaonekana kurejea tena, kwani huu ulikuwa ushindi wa nne kwa timu huyo kupata matokeo hayo msimu huu,  idadi kubwa kuliko timu nyingine yoyote.