Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ishu ya Viktor Gyokeres, Arteta awaonya wapinzani

ARTETA Pict

Muktasari:

  • Gyokeres, mwenye umri wa miaka 27, alisajiliwa na Arsenal akitokea Sporting Lisbon katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi mwaka huu, akigharimu Pauni 64  milioni.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta amewaonya wapinzani wa Arsenal katika michuano mbalimbali kuwa straika wao Viktor Gyokeres, ambaye hajafunga sana tangu kuanza kwa msimu, atakuwa mchezaji tofauti katika nusu ya pili ya msimu.

Gyokeres, mwenye umri wa miaka 27, alisajiliwa na Arsenal akitokea Sporting Lisbon katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi mwaka huu, akigharimu Pauni 64  milioni.

Hata hivyo, mdunguaji huyu wa kimataifa wa Sweden hajaonyesha kiwango kilichotarajiwa tangu awasili, akifunga mabao matano tu katika mechi 15 za Ligi Kuu England.

Mabao hayo alifunga dhidi ya Leeds United, Nottingham Forest na Burnley, ambazo zinazopambana katika sehemu ya chini ya jedwali na Everton ili nafasi ya 10.

Gyokeres alitolewa katika dakika ya 81  baada ya kupiga shuti moja tu katika mechi ya nyumbani dhidi ya Wolves, inayoshikilia mkia katika msimamo wa EPL.

Licha ya kutofunga mabao ya kutosha, Arteta anaamini mavitu ya mchezaji huyo wa zamani wa Coventry City yameanza kuonekana siku hadi siku ambapo anazoea mazingira.

Kabla ya Arsenal kusafiri kucheza dhidi ya Everton, katika mechi iliyomalizika kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0, Arteta amesema: "Kila mtu alikuwa na hamu kubwa kuona anasajiliwa katika timu. Tumefanikisha hilo. Tulisajili mchezaji mwenye rekodi ya nzuri ya ufungaji ambaye wakati anajiunga alihitaji kuzoea ligi. Hakuwa amefanya maandalizi ya mwanzo wa msimu.

"Wiki chache za mwanzo zilikuwa ngumu kwake kwa sababu kimwili hakuwa katika hali nzuri na alihitaji kuwa sawa kimwili ili kutupa tunachohitaji. Baada ya muda alianza kuonyesha kiwango chake taratibu, lakini bahati mbaya alipata majeraha lakini sasa amerejea. Nimeona mambo mengi chanya katika mechi mbili za mwisho alizocheza. Naamini ni suala la muda tu kabla hajatupa tunachohitaji. Sisi tunamuunga mkono."