Mbeumo, Manchester United mambo yazidi kuwa magumu
Muktasari:
- Mkataba wa sasa wa Mbeumo unatarajiwa kumalizika mwaka 2026 lakini una kipengele kinachoiwezesha Brentford kuurefusha kwa mwaka mmoja zaidi itahitaji.
MPANGO wa Manchester United kumsajili mshambuliaji wa Brentford na timu ya taifa ya Cameroon, Bryan Mbeumo, 25, umesimama kwa muda baada ya timu yake kuongeza bei hadi kufikia Pauni 70 milioni kutoka Pauni 65 milioni iliyokuwa inaihitaji hapo awali.
Dili linaonekana kuwa na ugumu sana kwa sababu Man United haitaki kulipa zaidi ya Pauni 65 milioni kwa ajili ya fundi huyu.
Mkataba wa sasa wa Mbeumo unatarajiwa kumalizika mwaka 2026 lakini una kipengele kinachoiwezesha Brentford kuurefusha kwa mwaka mmoja zaidi itahitaji.
Kwa mujibu wa ripoti, Mbeumo mwenyewe yupo tayari kujiunga na mashetani hao wekundu na amekataa timu zote zilizokuwa zinamhitaji lakini changamoto ni makubaliano ya ada ya uhamisho.
Awali kocha wake wa zamani wa Brentford, Thomas Frank ambaye kwa sasa amejiunga na Tottenham alipendekeza jina lake kwenye timu mpya lakini bado Mbeumo alikataa.
Man United inapambana kuishawishi Brentford ikubali ofa ya chini kwa sababu bajati yao dirisha hili siyo kubwa sana na inahitaji kuuza kwanza kabla ya kutumia.
Msimu uliomalizika Mbeumo alicheza mechi 38 za Ligi Kuu England na kufunga mabao 20.
Hugo Ekitike
LIVERPOOL imefungua mazungumzo na Eintracht Frankfurt ya kumsajili mshambuliaji wa klabu hiyo, Hugo Ekitike, 23, dirisha hili. Tovuti ya Sky Sports imefichua Frankfurt inahitaji zaidi ya Pauni 60 milioni kama ada yake ya uhamisho. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2029, msimu uliopita alicheza mechi 33 za michuano yote na kufunga mabao 15. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2029. Msimu uliopita alicheza mechi 48 za michuano yote na kufunga mabao 22.
Alejandro Garnacho
ASTON Villa ni miongoni mwa timu za Ligi Kuu England zinazohitaji kumsajili winga wa Manchester United na timu ya taifa ya Argentina, Alejandro Garnacho, 21, katika dirisha hili. Garnacho ni miongoni mwa wachezaji ambao wamepewa ruhusa ya kuondoka katika dirisha hili kwa sababu hayupo katika mipango ya Kocha Ruben Amorim. Mkataba wa sasa wa Garnacho ambaye anahusishwa sana na Napoli, unatarajiwa kumalizika mwaka 2028, msimu uliopita alicheza mechi 15 za Ligi Kuu England.
Nicolas Jackson
RASMI Manchester United imeanza kuwasiliana na wawakilishi wa mshambuliaji wa Chelsea, Nicolas Jackson, 24, dirisha hili ili kuboresha safu yao ya ushambuliaji. Mbali ya Man United, Nicolas pia anawindwa na Aston Villa na AC Milan ambazo zinataka kumsajili katika dirisha hili. Jackson ambaye msimu uliopita alicheza mechi 30 za Ligi Kuu England na kufunga mabao 10, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2033.
Granit Xhaka
LICHA ya kufikia makubaliano na NEOM ya Saudi Arabia, ripoti zinaeleza Sunderland imeanza mazungumzo na wawakilishi wa kiungo wa Bayer Leverkusen, Granit Xhaka, 32, kwa Hivi karibuni ilielezwa NEOM imemwekea ofa nono Xhaka na tayari amevutiwa nayo lakini kuingia kwa Sunderland kunaweza kubadilisha mawazo yake ingawa itatakiwa kuweka ofa ambayo itamshawishi.
Marcus Tavernier
WEST Ham imeongeza juhudi katika harakati zao za kumsajili kiungo wa Bournemouth, Marcus Tavernier, 26, dirisha hili. Benchi la ufundi linahitaji sana huduma ya Tavernier ili kuboresha eneo lao la kiungo ambalo lilikuwa na mapungufu makubwa msimu uliopita. Mkataba wa Tavernier unatarajiwa kumalizika mwaka 2028, msimu uliopita alicheza mechi 32 za michuano yote na kufunga mabao matatu.
Pervis Estupinan
MANCHESTER United imefanya mazungumzo na wawakilishi wa beki wa Brighton, Pervis Estupinan, 27, kujua ikiwa ipo tayari kumuuza dirisha hili. Mbali ya Man United, Estupinan pia anawindwa na baadhi ya timu za Saudi Arabia dirisha hili. Mataba wa Estupinan unatarajiwa kumalizika mwaka 2027, msimu uliopita alicheza mechi 36 za michuano yote.
Anton Stach
LEEDS United wamefikia makubaliano ya awali na kiungo wa Hoffenheim raia wa Ujerumani, Anton Stach, 26, ambaye kuna asilimia nyingi za kumpata dirisha hili. Tovuti ya Sky Sports imefichua kuwa Stach ameshawaambia hadi vigogo wa Hoffenheim kwamba anahitaji kuondoka na kupata changamoto mpya sehemu nyingine.