Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbappe apiga tizi kuiwahi Bayern

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo wa Ufaransa alishiriki mazoezi kikamilifu bila tatizo lolote, hatua iliyopunguza hofu iliyokuwepo kuhusu hali yake ya kiafya kutokana na jeraha la kichwani alilopata katika sare ya 1-1 dhidi ya Girona. Katika mchezo huo, Mbappé alipata jeraha juu kidogo ya jicho baada ya kugongana hewani.

MADRID, HISPANIA: NYOTA wa Real Madrid, Kylian Mbappé anatarajiwa kuanza katika mechi muhimu ya marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich utakaopigwa, Jumatano Aprili 15, 2026 usiku, katika Uwanja wa Allianz Arena.

Mshambuliaji huyo wa Ufaransa alishiriki mazoezi kikamilifu bila tatizo lolote, hatua iliyopunguza hofu iliyokuwepo kuhusu hali yake ya kiafya kutokana na jeraha la kichwani alilopata katika sare ya 1-1 dhidi ya Girona. Katika mchezo huo, Mbappé alipata jeraha juu kidogo ya jicho baada ya kugongana hewani.

Taarifa kutoka ndani ya klabu zinaeleza hali yake kwa sasa ipo vizuri, huku benchi la ufundi la Real Madrid likiendelea kumuangalia kwa karibu bila kumwekea vizuizi vikubwa kwenye mazoezi.

Kurejea kwake mazoezini ni ishara nzuri kwa kocha na mashabiki wa Real Madrid, hasa wakijiandaa na mechi hiyo ngumo ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Awali, Mbappe alichapisha taarifa kuhusu jeraha hilo na katika picha za mazoezini alionekana akiwa na plasta juu ya jicho huku akiendelea na mazoezi ya pamoja na wenzake.

Mshambuliaji huyo alipata jeraha hilo baada ya kupigwa kwa kiwiko katika paji la uso na beki wa Girona, Vitor Reis, hata hivyo, licha ya kuumia Madrid ilinyimwa penalti.

Real Madrid walishindwa kupata ushindi licha ya kuwa mbele awali katika Uwanja wa Santiago Bernabeu, baada ya kusawazishiwa bao la Federico Valverde, jambo lililopunguza matumaini yao ya ubingwa na kuwapa faida wapinzani wao wakubwa, Barcelona wanaoongoza kwa tofauti ya pointi tisa zikiwa zimesalia mechi saba kumalizika msimu.

Mchezaji huyo amefunga mabao 39 katika mechi 38 msimu huu kwenye mashindano yote akiwa na Real Madrid. Kati ya hayo, mabao 23 ya LaLiga yanamfanya kuwa kinara kwenye ligi hiyo. Ingawa kwa kiasi kikubwa amekuwa fiti msimu huu, tayari amekosa mechi sita kutokana na majeraha hasa kutokana na tatizo la goti lililokuwa linajirudia.